Ziara ya Rais Samia nchini India kuleta mageuzi ya kiuchumi Tanzania

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Historia inaonesha Tanzania na India zimekuwa nchi zenye mahusiano mazuri hususani katika kuendeleza miradi ya kimaendeleo. India ni moja ya Mataifa yanayokuwa kwa haraka sana kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikumbukwe India ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, inakadiriwa kuwa na watu 1,428,627,663, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazokuwa pia, ikiwa na idadi ya watu 61,714,120 kulingana na sensa ya mwaka 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan , anatarajia kufanya ziara ya siku nne, kuanzia tarehe 08 - 11 Oktoba 2023 nchini India. Hii inakuwa na mara ya kwanza kwa kiongozi mkuu (Rais) wa nchi hiyo kumkaribisha Rais wa Tanzania kufanya ziara nchini kwake. Ziara hiyo inaenda kuleta manufaa makubwa kwa Taifa letu kulingana na maendeleo yaliyopo nchini India.

Rais Dkt Samia akiendelea kuifungua nchi, tunatazamia kuona mabadiliko yakitoka katika sekta zote zitakazoguswa katika ziara hiyo. Tanzania ikiwa bado inaendelea kujikwamua katika wimbi la umasikini, magojwa pamoja na ukosefu wa baadhi ya huduma, ziara hii inaenda kugusa katika sekta ya viwanda, afya, kilimo, maji na usafiri wa majini. Lengo la kuzipa vipaumbele sekta hizi, ni kutokana na ufanisi unaoonekana kufanywa na nchi ya India katika kutatua changamoto zake katika nyanja hizo.

Sekta ya afya itaguswa katika ziara hiyo, tukitarajia kuanzishwa taasisi ya upandikizaji wa figo, kiwanda cha kutengeneza chanjo ya binadamu na wanyama, kuongeza ushirikiano kati ya hospitali za Tanzania na India, ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo na utaalamu na weledi wa matibabu katika taasisi zetu. Taasisi itakayoanzishwa itajikita pia, kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na magonjwa yanayosababisha figo kushindwa kufanya kazi. Kupitia sekta ya afya, tutavutia wagonjwa kutoka Mataifa ya jirani kuja Tanzania kupata huduma ya matibabu na kupelekea nchi yetu kupata pesa za kigeni. Ikiwa kupandikiza figo ni shilingi Milioni 30 hadi 40 kwa mtu mmoja.

Kutokana na mahusiano mazuri ya kidipromasia na kiuchumi baina ya nchi hizi, tumekuwa na mpango wa kubadilishana utaalamu kupitia sekta ya elimu. Haipingiki kuwa India ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa katika elimu ya tehama, ambapo tutaona baada ya ziara hiyo kuwepo na mabadiliko katika matumizi ya teknolojia katika mifumo ya kufundishia hususani kutumia mifumo ya e-education katika mitaala yetu.

Rais Dkt Samia amekuwa na kiongozi mwenye kupenda matokeo katika kipindi hiki cha uongozi wake, ameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazovutia sana wawekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwa nia pamoja na kuwekeza katika viwanda pamoja na uchumi wa buluu. Hii imepelekea kuwepo na matumizi bora ya bandari zetu kuingiza mizigo na kusafirisha mizigo kwa Mataifa mbalimbali na kupelekea usafiri wa majini kuwa chanzo cha kuingiza fedha za kigeni nchini.

Kupitia sekta ya kilimo, Tanzania itakuwa ndiyo mnufaika wa kwanza kutokana programu inazoziendesha ikiwemo BBT yenye lengo la kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana. Kutokana na unadhifu wa kukuwa kwa kilimo India, Tanzania inaenda kujifunza namna bora ya kuandaa mbegu bora pamoja na kufanya kilimo cha kisasa. Dunia ya leo imefanya kilimo kuwa ni miongoni mwa chanzo cha kukuza uchumi wa Mataifa yao.

Mathalani, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayosafirisha mazao ya majini kwenda nje ya nchi, miongoni mwa Mataifa yanayonufaika na mazao hayo ni pamoja na India ambayo imekuwa ni sehemu tunapouza mazao mengi ya majini. Ziara hiyo itapelekea kupanua soko la mazao hayo na kulifanya Taifa letu kuingiza fedha nyingi za kigeni pamoja na kukuza biashara.

Ndugu Watanzania kuanzia tarehe 8 hadi 11 mwezi huu tufuatilie vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuona namna Rais wetu anavyopambana kutuletea maendeleo, ili mara baada ya ziara hiyo tuwe na uwezo wa kuona umuhimu wa kuwajibika katika nafasi zetu ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wetu.
20231007_094129.jpg
20231006_103918.jpg
 
Chuma kimejaa kinaozea ardhini waiteni Mittal Steel au TATA waje wawekekeze tupate ajira.

5312513203_448ae28866_b.jpg

Au mnaona raha tukishinda kwenye Bao?
 
Dah huyu Samia anarubuniwa na mataifa mengine anakubali, hapo anadhani anawasogeza karibu kumbe wao ndio wanamsogeza karibu kisha wachukue kilicho chetu. Mwanamke ni Mwanamke tu
 
Subirini pande la ardhi likamegwe tena. Mara hii watakao hamishwa sinji ni Wazaramo au Wasukuma!!!
 
Historia inaonesha Tanzania na India zimekuwa nchi zenye mahusiano mazuri hususani katika kuendeleza miradi ya kimaendeleo. India ni moja ya Mataifa yanayokuwa kwa haraka sana kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikumbukwe India ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, inakadiriwa kuwa na watu 1,428,627,663, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazokuwa pia, ikiwa na idadi ya watu 61,714,120 kulingana na sensa ya mwaka 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan , anatarajia kufanya ziara ya siku nne, kuanzia tarehe 08 - 11 Oktoba 2023 nchini India. Hii inakuwa na mara ya kwanza kwa kiongozi mkuu (Rais) wa nchi hiyo kumkaribisha Rais wa Tanzania kufanya ziara nchini kwake. Ziara hiyo inaenda kuleta manufaa makubwa kwa Taifa letu kulingana na maendeleo yaliyopo nchini India.

Rais Dkt Samia akiendelea kuifungua nchi, tunatazamia kuona mabadiliko yakitoka katika sekta zote zitakazoguswa katika ziara hiyo. Tanzania ikiwa bado inaendelea kujikwamua katika wimbi la umasikini, magojwa pamoja na ukosefu wa baadhi ya huduma, ziara hii inaenda kugusa katika sekta ya viwanda, afya, kilimo, maji na usafiri wa majini. Lengo la kuzipa vipaumbele sekta hizi, ni kutokana na ufanisi unaoonekana kufanywa na nchi ya India katika kutatua changamoto zake katika nyanja hizo.

Sekta ya afya itaguswa katika ziara hiyo, tukitarajia kuanzishwa taasisi ya upandikizaji wa figo, kiwanda cha kutengeneza chanjo ya binadamu na wanyama, kuongeza ushirikiano kati ya hospitali za Tanzania na India, ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo na utaalamu na weledi wa matibabu katika taasisi zetu. Taasisi itakayoanzishwa itajikita pia, kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na magonjwa yanayosababisha figo kushindwa kufanya kazi. Kupitia sekta ya afya, tutavutia wagonjwa kutoka Mataifa ya jirani kuja Tanzania kupata huduma ya matibabu na kupelekea nchi yetu kupata pesa za kigeni. Ikiwa kupandikiza figo ni shilingi Milioni 30 hadi 40 kwa mtu mmoja.

Kutokana na mahusiano mazuri ya kidipromasia na kiuchumi baina ya nchi hizi, tumekuwa na mpango wa kubadilishana utaalamu kupitia sekta ya elimu. Haipingiki kuwa India ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa katika elimu ya tehama, ambapo tutaona baada ya ziara hiyo kuwepo na mabadiliko katika matumizi ya teknolojia katika mifumo ya kufundishia hususani kutumia mifumo ya e-education katika mitaala yetu.

Rais Dkt Samia amekuwa na kiongozi mwenye kupenda matokeo katika kipindi hiki cha uongozi wake, ameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazovutia sana wawekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwa nia pamoja na kuwekeza katika viwanda pamoja na uchumi wa buluu. Hii imepelekea kuwepo na matumizi bora ya bandari zetu kuingiza mizigo na kusafirisha mizigo kwa Mataifa mbalimbali na kupelekea usafiri wa majini kuwa chanzo cha kuingiza fedha za kigeni nchini.

Kupitia sekta ya kilimo, Tanzania itakuwa ndiyo mnufaika wa kwanza kutokana programu inazoziendesha ikiwemo BBT yenye lengo la kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana. Kutokana na unadhifu wa kukuwa kwa kilimo India, Tanzania inaenda kujifunza namna bora ya kuandaa mbegu bora pamoja na kufanya kilimo cha kisasa. Dunia ya leo imefanya kilimo kuwa ni miongoni mwa chanzo cha kukuza uchumi wa Mataifa yao.

Mathalani, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayosafirisha mazao ya majini kwenda nje ya nchi, miongoni mwa Mataifa yanayonufaika na mazao hayo ni pamoja na India ambayo imekuwa ni sehemu tunapouza mazao mengi ya majini. Ziara hiyo itapelekea kupanua soko la mazao hayo na kulifanya Taifa letu kuingiza fedha nyingi za kigeni pamoja na kukuza biashara.

Ndugu Watanzania kuanzia tarehe 8 hadi 11 mwezi huu tufuatilie vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuona namna Rais wetu anavyopambana kutuletea maendeleo, ili mara baada ya ziara hiyo tuwe na uwezo wa kuona umuhimu wa kuwajibika katika nafasi zetu ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wetu.View attachment 2774182View attachment 2774183
Aise. Ingekuwa ziara ni Mageuzi ya kiuchumi katika nchi yetu basi awamu ya nne tungeyapata. Ni mjinga pekee na mzalendo Tumbo ndiyo anaweza amini hivyo. Korea kaskazini ipo mbali Sana kiuchumi lakini husikii wala kuona viongozi wao Wana zurura ulaya na Afrika ovyo. Sisi wetu kafanya ziara nyingi ulaya,Amerika na Asia, na Hali kama ilivyo hivi. Umeme mgawo,mafuta juu, wizi na ufisadi upo na SGR ndo hivyo Tena. Tanzania inaweza iambia Nini India kwenye mkataba na uwekezaji kwao. Zaidi wahindi wamemuarika wakampige mikataba ya fursa yeye akaishie kuomba msaada. Tazama nchi yetu inadaiwa karibia na nchi zote za ulaya, Amerika na sasa Asia. Tunakwenda wap?
 
Hizi ni porojo za miaka yote.
 
Kwani ameenda India kujenga viwanda vya serikali huko? Sasa mageuzi ya kiuchumi Tanzania na ziara ya Samia nchini India wapi na wapi?
 
Wewe bado rudi chekechea uanzie huko labda akili zitaamka, mambo ya uhusiano na protokoli za kimataifa waachie wanazimudu. Huna habari kuna mengi Tanazania inafaidika na India na mengi yanawezekana mbeleni na yote hayo ufunguo wake ni mawasiliano kwa ngazi za juu za serikali.
 
Ubongo wako umewekeza zaidi ktk kuomboomba. Yaani unaamini nchi itapiga hatua kiuchumi kwa kutembeza bakuli?? Shubamiti!!
 
Aise. Ingekuwa ziara ni Mageuzi ya kiuchumi katika nchi yetu basi awamu ya nne tungeyapata. Ni mjinga pekee na mzalendo Tumbo ndiyo anaweza amini hivyo. Korea kaskazini ipo mbali Sana kiuchumi lakini husikii wala kuona viongozi wao Wana zurura ulaya na Afrika ovyo. Sisi wetu kafanya ziara nyingi ulaya,Amerika na Asia, na Hali kama ilivyo hivi. Umeme mgawo,mafuta juu, wizi na ufisadi upo na SGR ndo hivyo Tena. Tanzania inaweza iambia Nini India kwenye mkataba na uwekezaji kwao. Zaidi wahindi wamemuarika wakampige mikataba ya fursa yeye akaishie kuomba msaada. Tazama nchi yetu inadaiwa karibia na nchi zote za ulaya, Amerika na sasa Asia. Tunakwenda wap?
Nchi ya vituko duniani ni Tanzania pekee.
TAZARA imeendelea kuharibika tumeshindwa kabisa kuisimamia.
Pale makao makuu pamekuwa Pagala na admin ipo wanalipwa mshahara.
 
Historia inaonesha Tanzania na India zimekuwa nchi zenye mahusiano mazuri hususani katika kuendeleza miradi ya kimaendeleo. India ni moja ya Mataifa yanayokuwa kwa haraka sana kimaendeleo katika sekta mbalimbali, ikumbukwe India ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, inakadiriwa kuwa na watu 1,428,627,663, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zinazokuwa pia, ikiwa na idadi ya watu 61,714,120 kulingana na sensa ya mwaka 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan , anatarajia kufanya ziara ya siku nne, kuanzia tarehe 08 - 11 Oktoba 2023 nchini India. Hii inakuwa na mara ya kwanza kwa kiongozi mkuu (Rais) wa nchi hiyo kumkaribisha Rais wa Tanzania kufanya ziara nchini kwake. Ziara hiyo inaenda kuleta manufaa makubwa kwa Taifa letu kulingana na maendeleo yaliyopo nchini India.

Rais Dkt Samia akiendelea kuifungua nchi, tunatazamia kuona mabadiliko yakitoka katika sekta zote zitakazoguswa katika ziara hiyo. Tanzania ikiwa bado inaendelea kujikwamua katika wimbi la umasikini, magojwa pamoja na ukosefu wa baadhi ya huduma, ziara hii inaenda kugusa katika sekta ya viwanda, afya, kilimo, maji na usafiri wa majini. Lengo la kuzipa vipaumbele sekta hizi, ni kutokana na ufanisi unaoonekana kufanywa na nchi ya India katika kutatua changamoto zake katika nyanja hizo.

Sekta ya afya itaguswa katika ziara hiyo, tukitarajia kuanzishwa taasisi ya upandikizaji wa figo, kiwanda cha kutengeneza chanjo ya binadamu na wanyama, kuongeza ushirikiano kati ya hospitali za Tanzania na India, ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo na utaalamu na weledi wa matibabu katika taasisi zetu. Taasisi itakayoanzishwa itajikita pia, kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na magonjwa yanayosababisha figo kushindwa kufanya kazi. Kupitia sekta ya afya, tutavutia wagonjwa kutoka Mataifa ya jirani kuja Tanzania kupata huduma ya matibabu na kupelekea nchi yetu kupata pesa za kigeni. Ikiwa kupandikiza figo ni shilingi Milioni 30 hadi 40 kwa mtu mmoja.

Kutokana na mahusiano mazuri ya kidipromasia na kiuchumi baina ya nchi hizi, tumekuwa na mpango wa kubadilishana utaalamu kupitia sekta ya elimu. Haipingiki kuwa India ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa katika elimu ya tehama, ambapo tutaona baada ya ziara hiyo kuwepo na mabadiliko katika matumizi ya teknolojia katika mifumo ya kufundishia hususani kutumia mifumo ya e-education katika mitaala yetu.

Rais Dkt Samia amekuwa na kiongozi mwenye kupenda matokeo katika kipindi hiki cha uongozi wake, ameifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazovutia sana wawekezaji katika sekta mbalimbali, ikiwa nia pamoja na kuwekeza katika viwanda pamoja na uchumi wa buluu. Hii imepelekea kuwepo na matumizi bora ya bandari zetu kuingiza mizigo na kusafirisha mizigo kwa Mataifa mbalimbali na kupelekea usafiri wa majini kuwa chanzo cha kuingiza fedha za kigeni nchini.

Kupitia sekta ya kilimo, Tanzania itakuwa ndiyo mnufaika wa kwanza kutokana programu inazoziendesha ikiwemo BBT yenye lengo la kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana. Kutokana na unadhifu wa kukuwa kwa kilimo India, Tanzania inaenda kujifunza namna bora ya kuandaa mbegu bora pamoja na kufanya kilimo cha kisasa. Dunia ya leo imefanya kilimo kuwa ni miongoni mwa chanzo cha kukuza uchumi wa Mataifa yao.

Mathalani, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayosafirisha mazao ya majini kwenda nje ya nchi, miongoni mwa Mataifa yanayonufaika na mazao hayo ni pamoja na India ambayo imekuwa ni sehemu tunapouza mazao mengi ya majini. Ziara hiyo itapelekea kupanua soko la mazao hayo na kulifanya Taifa letu kuingiza fedha nyingi za kigeni pamoja na kukuza biashara.

Ndugu Watanzania kuanzia tarehe 8 hadi 11 mwezi huu tufuatilie vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuona namna Rais wetu anavyopambana kutuletea maendeleo, ili mara baada ya ziara hiyo tuwe na uwezo wa kuona umuhimu wa kuwajibika katika nafasi zetu ili kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wetu.View attachment 2774182View attachment 2774183
Maendeleo yataletwa na Mtanzania sio mgeni.
Msipende kuidhalilisha nchi na wananchi..
India ina nini ya kuizidi Tz
Punguzeni ujinga. Yaani kila ziara ya Mkulu basi ameenda kulia shida..
Umaskini wa Mwafrika ni ujinga
 
Hivi kuna haja gani ya kusafiri kila kukicha wakati mawasikiano yameboreshwa sana siku hizi sa 100 ikulu na mondi ikulu mbona hatuoni nchi za wezetu ulaya na amerika arabuni wakifanya hivyo?ni africa tu
 
cc237ccb-bd95-4201-9412-4579a3624be3.jpg

Viwanda vya Kutengeneza simu na Vifaa vya Kieletroniki vitajengwa

kilimo (masoko ya mazao kutoka kwenda )

Nyongeza ya nafasi 1000 za masomo India (Scholarship)

Kuanzishwa kwa Mradi mkubwa wa Maji kutoka Ziwa Victoria na kuyasambaza katika Miji 24

Kuanzisha Karakana ya Usafiri wa Vyombo vya Majini

Kuanzishwa kwa Taasisi ya Upandikizaji wa Figo nchini pia Kiwanda cha Kutengeneza Chanjo ya Binadamu na Wanyama

Biashara kati ya Tanzania na India zitatumia fedha za ndani.
 
Back
Top Bottom