"Nakupenda sana Jack Pemba, SIYO SIRI!"

"Nakupenda sana Jack Pemba, SIYO SIRI!"

Siyo siri... napenda sana wimbo wa Safari siyo Kifo wa Akudo - lakini maneno yake huwa yananifanya nishangae kidogo... yaani wanaume wazima wanamsifia mwanaume mwenzao Jack Pemba mwanzo hadi mwisho!
Atakuwa kawalipa kiasi gani?

mkono mtupu haulambwi
 
Ni kweli kabisa mtu mwenye akili zake timamu hawezi kujiita eti Ndama Mtoto wa ng'ombe.....

achana na pesa msindima,pesa NI SABUNI YA ROHO!jina lolote lile unajiita,na dharau zozote zile unazifanya.

nitakupa stori kina msanii mmoja maarufu wa muziki wa kizazi kipya 'KIJANA KABISA' anatembelea starlet,alipata mafanikio ya ghafla kaacha shule,amenunua nyumba TABATA!AKAAMUA KUKAA NA MAMA YAKE KWENYE NYUMBA HIYO

anachokifanya kwakweli HAPANA!hata kama ni hela.dogo ANABADILISHA WANAWAKE KAMA CH****I mbele ya macho ya mama yake mzazi.

PESA HIYO BWANA!

kuna paapaa mmoja anajiita ABDULI DOLE
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET), Asha Baraka ameishutumu Bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’ kuwa inafanya mapambano ya kichawi dhidi yake...

Asha ambaye kampuni yake inamiliki bendi mbili, African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Vibration Sound, alisema kuwa matukio ya uchawi yapo kwenye muziki wa dansi na kwamba hali ni mbaya.

Katika ‘intavyuu’ na mwandishi wetu Jumanne wiki hii, Asha alisema kuwa bendi yake ya Twanga Pepeta imekuwa ikipigwa ‘juju’ kwenye maonesho mbalimbali inayofanya ili ‘kuipoteza’ kibiashara.

Alisema: “Hata kabla ya uzinduzi wetu wa albamu ya Mwana Dar es Salaam hivi karibuni, tulikuta mayai yamevunjwa, tunakutana na vitu mbalimbali vinavyoashiria mambo ya kishirikina kwenye maonesho yetu.”

Aidha, Asha bila kutaja jina la Akudo alisema: “Mfano ni bendi moja ambayo ilionekana ikifanya mambo ya kichawi, hiki ni kitu cha ajabu sana, tupo kwenye muziki siku nyingi lakini hili linashangaza.

“Siwezi kuitaja bendi yenyewe lakini kila kitu kilifanyika kweupe, watu waliona. Hii ni kurogana ingawa mimi siamini kama uchawi unaweza kusaidia, muziki ni kipaji na mazoezi, kwahiyo kama huwezi utabaki kuwa hivyo.
“Hata uvae hirizi mia, lakini kama hauna kipaji wala mazoezi, huwezi kuimba wala kucheza kama Luiza (Mbutu). Mambo ya uchawi yapo, yanatokea mengi lakini hilo halitufanyi tutishike.”

Hata hivyo, wakati Asha akigoma kulianika jina la Wazee wa Masauti, uchunguzi wa Ijumaa umebaini kuwa bendi inayotajwa kumwaga uchawi kweupe ni Akudo na ilionekana hivi karibuni.

Maelezo ya vyanzo vyetu katika uchunguzi huo, yanaitaja Akudo kwamba Ijumaa iliyopita kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam majira ya jioni walimwaga kimiminika ukumbini hivyo kutafsiriwa kuwa walikuwa wanaroga.

“Kuna mtu mmoja ambaye tunajua kabisa alitumwa na Akudo, akiwa na dumu lenye majimaji alianza kuyamwaga kwenye kona tofauti ukumbini, hii sisi tuliona ni uchawi,” alisema mhudumu mmoja wa Mango kwa sharti la kutotajwa gazetini.

Mhudumu huyo aliongeza: “Bendi nyingi zinafanya maonesho yao hapa lakini hatujawahi kuona kitu kama hiki. Mimi nina muda mrefu hapa, hata siku moja sijawahi kushuhudia mambo kama haya, hii haifai kabisa.”

Katika kunogesha habari hiyo, mwandishi wetu aliongea na baadhi ya wanamuziki wa Twanga ambao waliishutumu Akudo kwa vitendo vya uchawi na kuongeza kuwa wanairoga bendi yao ili ‘kupora’ mashabiki.

Baada ya kuzinasa ‘nondo’ hizo, gazeti hili lilifanya ‘spesho intavyuu’ na Meneja wa Akudo, Michael Andrew ambaye alikiri kumwaga kimiminika Mango Garden.

Akipangua hoja ya uchawi, Michael alisema kuwa kimiminika kilichomwagwa ukumbini ni maji ya kawaida na walifanya vile makusudi ili kumtisha Asha ambaye alikuwa na njama za kuathiri ‘shoo’ yao.

“Tulipata taarifa kuwa Asha alikuwepo ukumbini tangu asubuhi na hakutaka kuondoka. Mpaka jioni inafika yeye yupo tu, unadhani alikuwa anataka nini kama si kututia hasara? Aling’angania ukumbini ili kutuwekea gundu watu wasiingie.
“Sisi tuliliona hilo, kwahiyo tukaona uamuzi wa busara ni kumtumia mtu amwage maji ili Asha akiona ajue ni dawa aondoke, hivyo ile ilikuwa ni gia ya kumuondoa Asha, lakini hatujaroga kabisa. Kwanza tumroge nani? Akudo ipo juu sana,” alisema Michael.

Globalpublishers

Haya nayo sijui yana ukweli? Jamani hizi bendi zina ushirikina pia?
 
Asante Burn kwa kuonyesha upande chanya wa kuimbwa.Sasa inakuwaje wengi wa wanoimbwa siyo wale wenye biashara zinazoeleweka?Na ninajua kuwa wanazo pesa za kutosha kujitangaza.Kwa wanasiasa kama Ntimizi, hicho ni kitu kingine kwa sababu miaka ya nyuma miziki ya Tanzania ilijaa kuimba wanasiasa - Nyerere, Karume, Aboud Jumbe, Kawawa, mama Maria Nyerere,mara Dr Kleruu n.k. hadi lilkuwa ina bore!

Sijui unamaana gani unaposema za kueleweka lakini kwa mfano wako Papaa Musofe anauza Magari pia na commision agent, Ndama nauza magari pia analeta spea anauza madini(hii ilikuwa zamani sina uhakika kama bado), akina muzamir ni mule mule.Hizi biashara za vijana zinamuelekeo wa kufanana sana. Hilo la wanasiasa sijui kwa nini umelitofautisha na hili la wafanya biashara kwani msingi wake mkubwa ni huohuo kujijengea umaarufu.Swali la Kizushi: kwa wanaume kuimba mume wangu Jack pemba inakushangaza vipi akina joti wanaoigiza kama wanawake kila siku?vipi tusiwe na wanaume wanao igiza nafasi za wanawake kwenye sanaa za kuigiza?
 
LOL
Inafurahisha na kunichekesha sana ndugu yangu..hasa pale niko na mume wangu halafu anasikia im singing along with wazee wa masauti...NAKUPENDA SANA MUME WANGU JACK PEMBA! ( do u get the joke?)
 
LOL
Inafurahisha na kunichekesha sana ndugu yangu..hasa pale niko na mume wangu halafu anasikia im singing along with wazee wa masauti...NAKUPENDA SANA MUME WANGU JACK PEMBA! ( do u get the joke?)

Inachekesha sana na si tu kuchekesha hata baba watoto anaweza kuona huyu mwanamke vipi,anamsifia mwanaume asiyemjua mbele yangu,nadhani atapata maswali mengi kama hivi huyu anaemtaja ni bora zaidi kuliko mimi,maana yawezekana unapoanza kuimba NAKUPENDA SANA MUME WANGU yeye atategemea ni yeye umemwambia mara anasikia JACK PEMBA,unajua kwa wale wanaume ambao kwa kweli mioyo yao ni midogo na hawana uvumilivu waweza jikuta unatandikwa kibao bila kutegemea.
 
Inachekesha sana na si tu kuchekesha hata baba watoto anaweza kuona huyu mwanamke vipi,anamsifia mwanaume asiyemjua mbele yangu,nadhani atapata maswali mengi kama hivi huyu anaemtaja ni bora zaidi kuliko mimi,maana yawezekana unapoanza kuimba NAKUPENDA SANA MUME WANGU yeye atategemea ni yeye umemwambia mara anasikia JACK PEMBA,unajua kwa wale wanaume ambao kwa kweli mioyo yao ni midogo na hawana uvumilivu waweza jikuta unatandikwa kibao bila kutegemea.[/QUOTE]

Msindima, umenipata kabisa shosti!
Ndicho hasa kinanichekesha zaidi......watu wako bize...utaona hata wanaume (baadhi yao) wanaitikiwa kibwagizo hicho kwa furaha kabisa hahahahahah huku wengine wanakuwa wameuchuna utadhani wamelazimishwa kucheza ..ukizingatia anaeimbwa ni PDG mhhh.
 
Naomba ufafanuzi hapa ina maana ili uimbwe unatoa pesa? Mmmhh jamani na hawa nao wanataka kuimbwa ili wapate nini?mbona sijawahi kusikia mchango wa hawa watu kwenye jamii? au ni kutafuta tu umaarufu usiokuwa na maana?

...wanatafuta u -Bongo Celebrity kwa nguvu zote! si kwenye nyimbo tu, hata ukiperuzi kwenye blog ya michuzi, utawakuta kina "wadau wa ughaibuni"

...aibu tupu wallahi! 😀
 
Nakupenda kama ndama anavyompenda mama yake "NDAMA MTOTO WA NGOMBE."
Mwanzoni nilidhani walikuwa wanaimanisha hivyo kumbe walikuwa wanamaanisha mtu aitwae Ndama Mtoto wa Ngombe! Majina mengine hata kama ni kiyapresida yanatoa picha halisi ya huyo mtu alivyo. Kama umeenda shule huwezi kukubali kitwa Ndama Na mama yako ni Ng'ombe . AKA?
 
huyu mdogo aliyekuwa anadharauliwa ni yupi?

Kwa hiyo alikua anamdharau mdogo wake kisa kutajwa kwenye hizo nyimbo? Mmhh jamani sifa zingine za kijinga kweli,huu umaarufu tunaouvuta kwa kamba mbona una mambo! na nilisema utakuta hawa watu hawana msaada kwa jamii au hata kwa ndugu zao,mtu unafikia una mdharau mdogo wako kweli ni akili hiyo?
 
tunaomba jina la huyo mdogo mtu,maana tunahisi hizi habari nyingine ni za kizushi
 
huyu mdogo aliyekuwa anadharauliwa ni yupi?
tunaomba jina la huyo mdogo mtu,maana tunahisi hizi habari nyingine ni za kizushi

...Mkuu 'komalia' hivyo hivyo,...niliwahi pia kusikia Jack Pemba anamletea nyodo mama yake, ...ilikuwa habari ya kusikitisha sana nikikumbukia maisha yao ya utotoni mitaa ya Boy scout na Don Bosco japo sikuweza zifuatilia tena.
 
Walimuigiza Jack kwenye ze comedy - kuonyesha mama yake akiishi maisha duni wakati yeye anaishi maisha ya kifahari ughaibuni.
 
Lakini WOS cha kukumbusha Jack Pemba hivi sasa amefulia totaly mpaka anaona aibu kutoka alikuwa anamzalau mdogo wake sasa yupo TBT pale aibu kafulia.

watu wanaonyanyuka in dubious ways lazima wafulie tu!

Komredi Fidel na WoS, kufulia ni sawa na kuchezea shilingi ****** kisha ikadumbukia, a.k.a kulosti, au? hebu nielewesheni naona neno linapanda chati sana hili, mara DECI waambiwe 'wamefulia',,,,,daaamn
 
Nakupenda kama ndama anavyompenda mama yake "NDAMA MTOTO WA NGOMBE."
Mwanzoni nilidhani walikuwa wanaimanisha hivyo kumbe walikuwa wanamaanisha mtu aitwae Ndama Mtoto wa Ngombe! Majina mengine hata kama ni kiyapresida yanatoa picha halisi ya huyo mtu alivyo. Kama umeenda shule huwezi kukubali kitwa Ndama Na mama yako ni Ng'ombe . AKA?

tena mkuu hivi hiki kibwagizo si kipo kwenye ule waimbo wa Christian Bella....'yako wapi mapenzi'?
Mi ndo leo najua kumbe ni jina la mtu!
 
Komredi Fidel na WoS, kufulia ni sawa na kuchezea shilingi ****** kisha ikadumbukia, a.k.a kulosti, au? hebu nielewesheni naona neno linapanda chati sana hili, mara DECI waambiwe 'wamefulia',,,,,daaamn

Hujakosea..... ni pale unapodondoka toka juu hadi chini.
Kama ulikuwa na hali nzuri..ukabweteka na baadae ukajakuishia kubaya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom