WoS utamaduni huu haukuwahi kuwapo katika miziki yetu(ya dansi) kabla ya wakongo kuingia katika muziki hapa nchini ndio maana inawapa shida sana watu wengine. Lakini ukweli ni kwamba tabia hii ya kutaja majina ni aina fulani ya matangazo na inawasaidia sana wanaotajwa kwenye biashara wanazozifanya. Kwa mfano hao wote uliowataja ukiacha Jack Pemba ni wafanya biashara na kwa namna moja au nyingine mafanikio yao yametokana na kuimbwa. Kwa mfano biashara za mamaa Dotnata umeweza kumsaidia kupata kazi nyingi kwa urahisi kwenye biashara yake catering na decoration. Kifupi faida wanazo zipata ni kubwa sana ukilinganisha na gharama wanazotumia. jaribu kuwaza hiyo air time anayopata mtu kama ndama angekuwa amelipia tangazo redioni ingekuwaje? Kwa watu wengine pia inawajengea umaarufu wanaoutumia kwenye siasa, mfano said ntimizi aliweza kuwashinda wagombea wengine wa uenyekiti wa vijana mkoa wa dar kwa kuwa wapiga kura walikuwa wanalijua jina lake kabla. Nafikiri utaratibu huu si mbaya ukilinganisha faida na hasara zake pia unasaidia kuwalipa wasanii wetu ukizingatia muziki hapa nchini haulipi na hata hizo radio station huwa zinafaidika kutokana na huo muziki bila kurudisha fadhira kwa wana muziki lakini bila kujua wapiga matangazo ya biashara humo humo.KUHUSU kuifanyia kitu jamii hilo ni suala binafsi kwani hata sisi ambao hatutajwi tunaifanyia nini jamii? kwani Pretty na mwanajamii one wanatofauti gani mamaa Dotnanta?