Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].

Please please Nyani Ngabu....acha kutusemea unataka tufanye maandamano ambayo yatasababisha mauaji nchini ndo uamini kwamba hali ni mbaya??? Niishie hapa maana ulivyonikera naacha akiba 75%
 
Mbona hata misibani watu huwa tunakula, kunywa, kuimba na hata kucheza. Kwahiyo hayo yakitokea ndio kusema hakuna msiba?! Tathmini ya kiwango cha chini sana hiyo
 
Uliza swali lako sio kucheza michezo ya kitoto.

Wewe ni mpumbavu fullstop

Umeuliza maana ya BRN

Umepewa jibu ni matokeo makubwa sasa ,unalalama am playing games with you! Ridiculous.

BRN = Big Result Now

Mnajifanya kutetea serikali hata kauli mbinu zake hamzijuwi so what?
 
Haiwahusu waliostahafu mwaka huu tu. Mimi nina zaidi ya miaka 7 toka nistahafu. Nilikuwa napokea pension yangu vizuri bila matatizo. Matatizo yameanza Sept baada ya mambo ya kishenzi kuanza kutumika August.

Ni bahati mbaya sana kuwa na watu wasiotumia viungo sahihi kufikiri. Ile roho mbaya ya kuwa mimi hainigusi ni hulka mbaya sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hadi wastaafu wanaongea Lugha moja ma wafanyakazi sasa...eeeh shikamoo jiwee[emoji114][emoji114][emoji114][emoji114][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wewe ni mpumbavu fullstop

Umeuliza maana ya BRN

Umepewa jibu ni matokeo makubwa sasa ,unalalama am playing games with you! Ridiculous.

BRN = Big Result Now

Mnajifanya kutetea serikali hata kauli mbinu zake hamzijuwi so what?
BRN iliishia wapi hivi????[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
What was your point telling me about BRN in the first place?

I am not a mind reader.

Maybe your friends my understand your cryptic messages. Not me.

So, let's try this again.

Why did you bring BRN in the first place?

Simple question.
 
Mkuu ccm noma sana inatuendesha hovyohovyo sababu tuliowengi tuko wajinga na wapumbavu

Big result now
Mkukuta
Mkurabita
Kilimo kwanza
Hapa kazi tu etc

Hizi zote tunaingizwa machakani zinakufaga vifo vya kutoweka bila feedback
 
Maisha sio kula tu kuna mambo mengine mengi. Kula lazima watu wale hata kama hali ni ngumu hilo halikwepeki.
ww umeanza dar na unasema na mikoa mingine? Mikoa ip?

Toka nje ya dar nenda mbali zaid. Hali inatofautiana na mikoa na mikoa.
Halaf watanzania wanatabia ya kulalamikia ndani kwa ndani.. yes huko nje wanaweza wasiseme lakin wakalalamikia kwenye mitandao.
Nini wanachokula sasa hivi ambacho walikuwa hawakili zamani?
 
What was your point telling me about BRN in the first place?

I am not a mind reader.

Maybe your friends my understand your cryptic messages. Not me.

So, let's try this again.

Why did you bring BRN in the first place?

Simple question.

Because is related to someone like you.
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Tatizo sio ww Tatizo ni Buku 7
 
Do you have something you want to tell me or you want me to read your mind?

I don't read minds these days.

I fully agree with BRN mindset, you can't.

For you, this is my last replay and you don't deserve any!
 
Mkuu ccm noma sana inatuendesha hovyohovyo sababu tuliowengi tuko wajinga na wapumbavu

Big result now
Mkukuta
Mkurabita
Kilimo kwanza
Hapa kazi tu etc

Hizi zote tunaingizwa machakani zinakufaga vifo vya kutoweka bila feedback
Yaniii jamaa wanaona wananchi wote sisi mazwazwaaa...
 
We ulitegemea watu wasivae mkuu hali ni mbaya ila ubaya kiasi gani ni siri ya kila moja.
 
Kwa wafanyakazi ukiona mtu analialia saaaana jua tu alikuwa haishi kwa kipato halali kwa asilimia kubwa, either alikuwa sehemu ya kupiga rushwa rushwa ndogo ndogo au na kubwa, au alizoea safari na vikao vya kulipwa visivyo na tija kwa taasisi na taifa, wenyewe wanamsemo wao kutafuta ada ya watoto ikifika december top layer yote ilikuwa nje ya nchi kwenye kuudhuria vikozi vya junior staff au kula bata tu.

Tunajua mishahara haitoshi lakini watu wanaishi maisha ya kusadikika sana. Tena mtu huyo hana hata genge la kumiongezea kipato.

Kwa wafanyabiashara hali inaweza kuwa ngumu, kwani kodi wanabanwa sana wengi walizoea njia za panya na wazee wa kukusanya kodi siku hizi wanatarget tu kichwani. Pia wateja wamekuwa na akili ya kutumia pesa siyo mambo ya zungusha meza zote tena!

Kwa wamiliki wa magari bila shaka hali ni ngumu mafuta yamepanda sana bei, japo load licence ilitolewa na kusukumizwa kwenye lita ya mafuta imeongeza mbinyo.

Bila kusahau wahitimu wa vyuo wanakatwa 15% kwa sasa
 
Back
Top Bottom