Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Inakuhusu? Tuulize sisi tunayoishi hiyo hali, mimi mstahafu nadaiwa kodi ya miezi mitatu sasa pension hakuna na haijulikani. Fikiria msongo nilio nao.
 
Ni kweli kabisa Nyani. Maisha ya watanzania ni yale yale wakati wa Kikwete na ndiyo hayo hayo wakati huu. Hakuna kilichobadilika. Labda niseme kelele nyingi unazozisoma hapa nyingi zinatoka kwa wale watu amabao walikuwa wanaishi kijanja janja na sasa inawawia vigumu. Mimi sina chama chochote cha siasa na wala sitakaa niwe mwanasiasa hivyo ninaposema ni wale waliokuwa wanaishi kijanja sipigi siasa. Kundi hili limebeba watu wa kada mbalimbali na karibia wote ni watumiaji wazuri wa Internet ndio maana unaona kelele zimekuwa nyingi.
Kumbe nyie mlikuwa mnaishi kijingajinga? Shauri yenu, nakuhakikishia tutatoboa tu. Nawashukuru kwa kutukomazi. Ujue maji yanafuata mkondo, huwezi yazuia kwa kiganja.
 
Nyani Ngabu hivi kitengo kinakutumia kiasi gani kwa mwezi, huko nyuma hukua hivyo, bei ya sukari unaijua?
Bei mafuta (yote) unaijua?
Bei ya dola unaijua?
Vyote hivyo vimepanda watumishi wamebakia pale alipowakuta
 
Mbona mimi ni mtu mwenye maisha ya kawaida kabisa na naona anachokisema mwanzisha thread kina ukweli?

Msaidie kujibu hili swali yeye limemshinda

Umeongea bila fact hata moja ama kweli huu Uzi huu waajabu.

1. Tuambie Lita moja ya petrol ni Tsh ngapi? Kwanini na ina-impact gani kwa maisha ya mtanzania ukizingatia yafuatayo

a) ongezeko la mishahara sambamba na ongezeko la bei ya petrol

Kikwete ilikuwa Tsh ngapi Vs sasa ya Pombe

Mishahara imepanda kwa uwianogani?

Nitakuuliza swali la pili ukijibu hilo
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Angalau umejionea mwenyewe watu wa hasa JF walivyo wapotoshaji hasa akina Quinine Sky Eclat Salary Slip Erythrocyte Retired na wengine wengi
 
Msaidie kujibu hili swali yeye limemshinda

Umeongea bila fact hata moja ama kweli huu Uzi huu waajabu.

1. Tuambie Lita moja ya petrol ni Tsh ngapi? Kwanini na ina-impact gani kwa maisha ya mtanzania ukizingatia yafuatayo

a) ongezeko la mishahara sambamba na ongezeko la bei ya petrol

Kikwete ilikuwa Tsh ngapi Vs sasa ya Pombe

Mishahara imepanda kwa uwianogani?

Nitakuuliza swali la pili ukijibu hilo
hivi unaamini katika mabadiliko?
 
Nkafikiri tangu uanze kukaa Marekani labda akili yako itaanza kucharge kumbe ndo yale Yale maviii matupu
One can take a Nyantuzu out of the bush but never ever can one take the bush out of a Nyantuzu and you can take that to the bank!
 
Kumbe nyie mlikuwa mnaishi kijingajinga? Shauri yenu, nakuhakikishia tutatoboa tu. Nawashukuru kwa kutukomazi. Ujue maji yanafuata mkondo, huwezi yazuia kwa kiganja.
Ni kweli ulivyosema. Kwa maisha ya Bongo kama hufanyi safari za nje zisizo na tija unaishi kijinga jinga. Kama hufanyi vikao hewa na kujilundikia posho unaishi kijinga jinga. Kwa kifupi kwenye nchi yetu neno ''ujanja'' na neno ''ujinga'' lina maana zaidi ya kwenye kamusi.
 
Msaidie kujibu hili swali yeye limemshinda

Umeongea bila fact hata moja ama kweli huu Uzi huu waajabu.

1. Tuambie Lita moja ya petrol ni Tsh ngapi? Kwanini na ina-impact gani kwa maisha ya mtanzania ukizingatia yafuatayo

a) ongezeko la mishahara sambamba na ongezeko la bei ya petrol

Kikwete ilikuwa Tsh ngapi Vs sasa ya Pombe

Mishahara imepanda kwa uwianogani?

Nitakuuliza swali la pili ukijibu hilo
Na mimi nijibu hili wakati natayarisha jibu la swali lako.
1. Bei ya petrol wakati wa Mwinyi, Mkapa ilikuwa sh ngapi vs wakati wa Kikwete!
 
Lakini kura hizo hizo kama atashinda:

[emoji830]Mbowe
[emoji830]Mdee
[emoji830]Sugu
[emoji830]Msigwa
[emoji830]Mnyika
[emoji830]Bulaya
[emoji830]Nassari
[emoji830]Lema
[emoji830]Zitto

Zinakuwa kura halali sio?

Kura zinakuwa za kuiba kama CCM ikishinda, lakini upinzani wakishinda zinakuwa halali?

Unaona ubongo wako ulivyoathirika na hizi feel-good propaganda zenu?

Na safari hii, baada ya 2020 ruzuku ndio itakuwa mwisho. Tafuteni vibarua vingine.

Anashinda kupitia wapi segerea?

Upumbavu mwingine usiozingatia facts na bases zinazo determine ushindi wa kipolisi, mahakama na tume

Mnaudhi sana kuacha akili zenu miguuni nakutumia njaa kufikiri
 
Mbona mimi ni mtu mwenye maisha ya kawaida kabisa na naona anachokisema mwanzisha thread kina ukweli?
huwezi kuona tatizo kwa kuwa kwa post hii tu umeshaingiza siku. nyie si mnalipwa kwa kutetea kila kitu
 
Kpind cha JK Sidhani kama mkopo wa elimu ya juu wakiomb kwa gharama kufikia elf 35. na pia watu walikuwa wanapata wengi ila sasa wengi wanakosa pia walopata asilimia chache tu. Mshukur mungu ila mazingir magumu sana.
 
huwezi kuona tatizo kwa kuwa kwa post hii tu umeshaingiza siku. nyie si mnalipwa kwa kutetea kila kitu
Hunijui. Mimi husimamia ukweli na si mfuata mkumbo! Mkumbo ninaoukataa ni kuunga tela na kusema kuwa maisha ya mtanzania wa kawaida yaliwahi kuwa mazuri na sasa ni mabaya!
 
Ni kweli ulivyosema. Kwa maisha ya Bongo kama hufanyi safari za nje zisizo na tija unaishi kijinga jinga. Kama hufanyi vikao hewa na kujilundikia posho unaishi kijinga jinga. Kwa kifupi kwenye nchi yetu neno ''ujanja'' na neno ''ujinga'' lina maana zaidi ya kwenye kamusi.
Nazungumnzia pension ambayo nilikuwa nakatwa toka kwenye mshahara kila mwezi kwa ajili ya maisha ya kustahafu. Awamu hii wameichota yote hawana jinsi ya kuirudisha sisi mtaani ndiyo sasa tunaishi kiujanja ujanja kuwakwepa wanaotudai.
 
Anashinda kupitia wapi segerea?

Upumbavu mwingine usiozingatia facts na bases zinazo determine ushindi wa kipolisi, mahakama na tume

Mnaudhi sana kuacha akili zenu miguuni nakutumia njaa kufikiri
Upinzani hauna sera mbadala kwa sasa.

Kila kukicha wanarukia matukio ya serikali.

Kwenye uchaguzi kwa nini wachaguliwe?
Ili walete nini?

Huu upinzani wa sasa unafaa kufa kabisa ili upinzani madhubuti uibuke.

Tunahitaji upinzani mzuri. Hawa wa sasa malengo yao ni

[emoji830]Kuingia ikulu
[emoji830]Kukusanya ruzuku
[emoji830]Kupeana kula.

Hizi sio ajenda za kumshawishi mTanzania leo amteme Magufuli.
 
Mugabe hakuwahi kukiri watu wake walikuwa wanakula nyasi kama unavo claim wewe!. Au ni habari za mitandaoni nazo?

Ushamaliza kumvisha nguo mzee wako asubuhi hii zamu yako ishaisha, msubiri mwenzako aje mupekezane shift.
 
Na mimi nijibu hili wakati natayarisha jibu la swali lako.
1. Bei ya petrol wakati wa Mwinyi, Mkapa ilikuwa sh ngapi vs wakati wa Kikwete!

Ukisikia uwezo mdogo wa watanzania kufikiria ndo huu

1. Hoja yenu inaongelea nini?

2. Zipo facts zakutafsiri hicho mlichokileta? Zipi?

3. Nani anatakiwa kutetea hii hoja yakipumbavu wewe utushawishi au Mimi kukuuliza wewe?

Nitakujibu kifupi ukishindwa kunielewa wewe mwehu

Kila kipindi kulikuwa na gradual salaries increment hence life balance existed

Sasa hivi is one way fusing no balance to the citizens side.
 
Upinzani hauna sera mbadala kwa sasa.

Kila kukicha wanarukia matukio ya serikali.

Kwenye uchaguzi kwa nini wachaguliwe?
Ili walete nini?

Huu upinzani wa sasa unafaa kufa kabisa ili upinzani madhubuti uibuke.

Tunahitaji upinzani mzuri. Hawa wa sasa malengo yao ni

[emoji830]Kuingia ikulu
[emoji830]Kukusanya ruzuku
[emoji830]Kupeana kula.

Hizi sio ajenda za kumshawishi mTanzania leo amteme Magufuli.

Mzee wa BRN huwezi elewa ninachokieleza
 
Back
Top Bottom