Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,204
Reaction score
144,095
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
 
kaka zaman bata zilikua kama zote bwana... watu wanapak magari yao wanapanda daladala unsema hali sio mbaya..watu kila jumamos walikua wanaenda minada ya nyama lakin sasa hv waulize hao masai anaishia kuuza mbuzi 20 out of 100@day?aka sitak kukubaliana na hoja yako😥
walokua wanapenda kupiga pamba ss hv hawavai kivile.. khaa
 
Maisha lazima yaendelee watu hawaezi acha kula
Ila wanachokula sasa ndo tatizo......
Wengi wanakula ili wasife
 
Umenikumbusha Dr Slaa alivyodai aishi kwa mihogo wakati alikuwa analipwa mshahara sh 7 milioni!
 
Neno, japo Wenye hekima na wazalendo wa kweli hawasubiri taifa likwame Kabisa, wapo makini na kuonya kila dalili mbaya kwa uchumi wetu,ustawi na umoja wa taifa letu.
Ki ukweli hali inazidi kuwa mbaya, uwezo watu kununua unazidi kupungua( purchasing power)
Bei bidhaa isipokuwa chakula zinapaa kila uchao mfano vifaa ujenzi,bidhaa za mafuta
" were in right truck" " no free lunch" tupambane
 
Mtu yuko ughaibuni anawasemea watu waliopo Manzese,Matombo,Mwemberadu na kwingineko matakoni mwa Tanzania, ili hali hata yeye mwenyewe akija Tanzania anafikia kwenye hotels za nyota kadhaa na baadhi ya ndugu zake anawakwepa kuchoshwa na mizinga!!!

Miafrika ndivyo tulivyo indeed, na unafiki ni mojawapo wa adui mkuu kabisa kwa Taifa hili na vizazi vijavyo!!
 
Attachments

kaka zaman bata zilikua kama zote bwana... watu wanapak magari yao wanapanda daladala unsema hali sio mbaya..watu kila jumamos walikua wanaenda minada ya nyama lakin sasa hv waulize hao masai anaishia kuuza mbuzi 20 out of 100@day?aka sitak kukubaliana na hoja yako😥
walokua wanapenda kupiga pamba ss hv hawavai kivile.. khaa

Nabisha!

Jumanne naenda mnadani pale Kidinda.

Najua watu watajaa mpaka pomoni.

Mbuzi watachinjwa, nyama zitachomwa na kuliwa papo hapo, na Balimi zitanyweka.

Kuhusu watu kuacha magari yao na kupanda daladala....

Watu huwa na sababu nyingi tu za kufanya hivyo:

Wengine kupanda daladala ni kufanya mazoezi.

Wengine hupanda daladala kwa sababu ya convenience.

Wengine hupanda daladala just for the hell of it.

Wengine hupanda daladala kwa sababu hawapendi kuendesha magari yao maana uendeshaji wa Dar, kwa mfano, unahitaji uwe na moyo mgumu kweli kweli.

Licha ya hayo, mbona foleni jijini Dar hazijapungua sasa kama watu wameacha kuendesha magari yao na kuamua kupanda daladala kwa sababu ya ugumu wa maisha?

Hela za nauli za kupandia daladala wanazitoa wapi?

Bado nabisha. Hali si mbaya kama tunavyoaminishwa.

Hali ingekuwa ni mbaya kihivyo basi hata wewe usingepata hela ya kununulia salio uje hapa JF na kutoa maoni yako kama ilivyo kwa wengine wanaotoa mawazo yao kwingineko huko mtandaoni.

Nabisha.
 
Kumbe na wew uliwahahi kupanga foleni ya "kaya", kumbe umekula chumvi kidogo. Serikari ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni muunganiko wa nchi tatu Tanganyika, Zanzibar na Mitandaoni. Sasa hawa wakazi wa nchi ya Mitandaoni ndio hawaridhishi sana na mwenendo wa Jamhuri ya Muungano
 
Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Hiki ni kitendawili ambacho kupata jibu halisi sii rahisi. Ila nadhani wanaolia hali ngumu ni wale wazee wa dili mbofu mbofu.
 
Back
Top Bottom