Nakataa kabisa, hali sivyo kama inavyodaiwa

Huku mitandaoni sasa kumeshakuwa ni sehemu ya uhalisia mbadala [alternate reality].

Ukiishi huku utaambiwa na kuaminishwa kuwa huku uraiani sasa hivi hakukaliki. Utaaminishwa [na kama ukiwa mjinga, mvivu, na zuzu, utaishia kuamini kweli] hali ya maisha ni mbaya mno. Hayo utayoaminishwa yatakufanya ujenge taswira nyingi mno kichwani.

Unaweza ukapata taswira ya kwamba sasa hivi Watanzania wengi wanalala njaa. Watanzania hawana nguo za kuvaa. Maduka hayana bidhaa. Watu wanakula nyasi na panya kama ilivyokuwa huko Zimbabwe miaka kadhaa iliyopita. Watoto wa shule hawana kalamu wala daftari. Watu hawanywi pombe. Hawali kitimoto. Hawaogi. Hawana magari. Hawachepuki. Na mengineyo lukuki.

Lakini mtu ukiachana na hayo maneno ya kwenye mitandao na uingie mwenyewe uraiani ujionee na upate tajiriba ya uhalisia wa mambo, utaishia kuhitimisha kuwa huko kwenye mitandao kuna upotoshaji na utiaji chumvi mkubwa sana.

Tembea tu huku na kule jijini Dar, nenda mikoa mingine na wilaya zake, utaona maisha ya watu yanaenda tu kama ilivyo siku zote.

Mara umekutana na msafara wa harusi. Umekaa kwa Mangi unakunywa Konyagi yako ya kupimiwa mara ghafla unaona kigoma kinapita na watu, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto, wanajiachia tu.

Sasa kama uko ni mtu wa tafakuri, utajiuliza, ‘mh...hivi hiyo hali mbaya inayozungumziwa huko kwenye mitandao ndo ipi hasa’?

Kwa hiyo, kusema ukweli mimi nakataa kabisa. Nabisha. Nasema hali si mbaya. Hali iko vile vile tu ambavyo imekuwa karibu siku zote, ukiondoa labda enzi zile ambapo watu tulikuwa tunaenda kupanga mstari kwenye maduka ya ugawaji kununua mikate ya Siha, sukari, sabuni za Mbuni na Mbunju, na mahitaji mengine.

Zaidi ya hapo, kelele kelele za huko mitandaoni hazina mashiko. Ni za watu wanaotapa tapa tu. Wafamaji.

Wakatabahu,

Alhaji N. Ngabu [emoji6].
Wabongo watakuchosha..sasa hvi hapa nipo Karatu kikazi,ktk ngome ya wananchi wa upinzani,nipo nakunywa kahawa pembeni kabisa ya soko...wanalalamika maisha ni magumu lakini

1. Hapo sokoni naona watu wanatoka na mafuko ya ndizi wanaenda kuchanganya na utumbo wa ngombe wale

2. Ktk nchi hata siku moja sijaona mtoto au binadamu mkubwa ameanguka na kufa njaa tena pasipo kusaidiwa na watu wengine yamkini nao wana njaa,sijawhi ona na ninafanya kazi ya mashirika napiga kijiji kwa kijiji,wilaya kwa wilaya,mkoa to mko lakini sijawahi kukutana na hali kama ya Zimbabwe au Malawi watu wanakula udongo

3. WaTanzania tuna dhambi ya kulalamika kupita kiasi bila kufanya uchunguzi kwamba ni kweli shida walizo nazo kuna nchi ambayo watu wanaishi tu bila kuhangaika kutafuta hapa duniani?

4. Wanakoona wamefanikiwa huko ulaya zile wanaona kwenye utandawazi ni maisha yao na wao wana magumu yao,na ukitaka kujua kua nako kuna maisha magumu watu waende wakaone,wale wanalazimika kulala kwa masaa hata mawili tu per day ili kuwafanya waweze kumudu gharama za maisha

5. WaTanzania wengi wanalalamika na wako kwenye drafti mtaani na wanaamini ikifika 18:00pm ni muda wa kwenda kulala ilihali huko wanakoona wamefanikiwa ndo kwanza wanafungua laptop

6. Ukimwambia mTanzania hvyo anakimbilia kusema Serikali haituandalii mazingira,mazingira gani mtu una akili,nguvu na aridhi kubwa lakini huna maarifa unasubiri watu wengine wafikiri dhidi yako na weww umekaa tu.

7. Tujaribu kufikiri kwa kina,kuthubutu kuanza na kutengeneza akili ya mpango kazi ndipo twende kwenye ofisi za serikali tuone kweli kama hazitusaidii..mimi nasema zinasaidia maana tumeona kwa macho yetu,watu wanadhani serikali itaanza kukusanya watu mtaani kwamba njooni ofisini mchukue hela.

Tutahangaika sana maana tutarithisha kizazi cha kulalamika tu. Kuna uzao uliozaliwa kuanzia mwaka 1980 kuja huku kina kelele sana na hakina uwezo wa kutengeneza mipango kazi ya kuelekea kwenye mfanikio
 
dah aisee karatu hapo kuna ustaz anauza alkasusu saf sana karibu na stend.nikishangaaga tu lodge za karatu milango ya bafu ni magrili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom