the-sniper
Senior Member
- Oct 5, 2014
- 168
- 238
Umeongea kiume sana na umemaliza yote kwenye hilo.Asikuongopee mtu sista, mwanaume akusamehe hicho kitu kwakuomba msamaha, labda sijui awe Mungu kamwambia mwenyewe. Lasivyo, ni mtu akae muda mrefu sana asahau hilo jambo na maumivu ila still akiibuka maumivu yanamuanza upya vilevile. Mwanaume anasubiria mpaka watoto wanafikia miaka 30 anafungua kesi ya mtoto sio wake maana mkewe alicheat miaka 30 iliyopita sembuse hiyo ya juzi
. Yaani that is from a man's perspective, usitegemee hata siku moja asahau hicho kitu labda awe amemshinda kiuchumi jamaa hivyo atakuwa hanachakumfanya mbali na hapo unampeleka jamaa kwenye kilio chake. Wanaume wanasemwa hawana grudges ila kwahili I assure you hakuna mwanaume asiyeweka grudge na litamchoma hata baada ya kupata kisasi chake ndio maana wengi huishia kujiua hata baada ya kulipiza.
Tukirudi kwa muanzisha uzi, MOSI kama una uhakika huwezi kumudu gharama za kupotezea vitu vyako (vyote au baadhi) badala yake unalazimika kuvifuata basi usitumie njia "rasmi" bali tafuta wenye mamlaka rasmi kwa njia isiyo rasmi uongozane nao ili mzee akileta hoja ya RB waipangue. Hapa namaanisha men in uniform mfano mgambo/askari wa jiji ambao umemalizana nao pembeni kama "wana".
PILI tambua kuwa hata ukifanikiwa kwenye hilo la kwanza huyo mzee hataacha kukuvizia kwa namna tofauti hasa ukizingatia hujui ana mishe gani hapo mjini. Dalili zinaashiria ni mtu kazi na sio ajabu yupo hapa JF anatafuta sumu tunazokupa aziandalie antidote. Muhimu ni kuchukua tahadhari kali zaidi hata kinga za kiimani kama unaziamini.
MWISHO naweka bayana maslahi yangu kuwa umemkosea sana huyo mzee hivyo akifanikiwa kukufanyia chochote alichokusudia kama kisasi sitamhukumu. Ni vile tu sina desturi ya kumlaumu mtu kwa kitu alichokifanya tayari sababu it can't be undone. Vijana tudhibiti mihemko tukiaminiwa tujiaminishe yatatukuta makubwa


