Najuta kuwa na huyu mwanaume katika maisha yangu. Ameharibu ndoto zangu, najiona si binadamu tena

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
54,745
2,000
Mwanaume uliyeandikiwa na Mungu atakuja kwa wakati wake, usilazimishe mapenzi. Jirani yetu alimpa mimba house girl wa mtu, mkaka alikuwa mwanafunzi wa Civil Engineering mwaka wa mwisho.

Dada alifukuzwa kwa boss wake, alimuendea mhusika. Yule kaka akimuweka binti guest mpaka anapata chumba. Walianza maisha vyombo wanaweka kwenye basin hawana hata kabati.

Baada ya kumaliza chuo yule kaka alipata kazi na walipata nyumba nzima walitokea kuwa jirani zetu. Yule dada alitusimulia walikotoka. Wakati huo akijifunza kuendesha gari mume wake alimnunulia.
 

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
5,072
2,000
Mwanaume uliyeandikiwa na Mungu atakuja kwa wakati wake, usilazimishe mapenzi. Jirani yetu alimpa mimba house girl wa mtu, mkaka alikua mwanafunzi wa Civil Engineering mwaka wa mwisho.

Dada alifukuzwa kwa boss wake, alimuendea mhusika. Yule kaka akimuweka binti guest mpaka anapata chumba. Walianza maisha vyombo wanaweka kwenye basin hawana hata kabati.

Baada ya kumaliza chuo yule kaka alipata kazi na wakipangisha nyumba nzima walitokea kuwa jirani zetu. Yule dada alitusimulia walikotoka. Wakati huo akijifunza kuendesha gari mume wake alimnunulia.
Mwanamke muongo wewe
 

amu

JF-Expert Member
Aug 8, 2012
15,512
2,000
Wewe embu acha hizo, soma nakuambia soma nakuambia soma endelea na degree yako, na ukimaliza degree specialise kwenye fani yako kuwa proffessional

Hakikisha una life time qualification, hakikisha jina lako linaanza na tittle kama vile "wakili msomi Ma BOBO " au "engineer Ma BOBO " .

Achana na huyo mburukenge kwa sasa, hasira hamishia kwenye kutengeneza maisha yako.

Dogo tengeneza career yako itakulinda na kukusaidia.

Kwa sasa huyo mburukenge msahau kabisa muhimu ahudumie mwanae tu, wakati wako ukifika utapata bonge la bwana na utafurahia mapenzi na maisha kwa ujumla.
 

Seth saint

JF-Expert Member
Oct 27, 2020
419
1,000
Pole sana kwa unayopitia ndugu!

Napenda tu nkupe ushauri huu kama utaona ni mzuri na unaweza kusaidia basi jaribu kufanya hivi

Umesema umeona Mwenyezi Mungu akitenda katika masomo yako ndio maana umekuja hapa JF kutoa ushuhuda eti? ndio ametenda sasa fanya hivi

Katika maombi yako ya kila siku mueleze Mungu kwamba unahitaji kuendelea na safari muonyeshe yakuwa unaye mtoto ambaye unampenda mwambie kuwa unahitaji kuona akiwa na furaha vivyo hivyo kwako. Basi yeye atakupatia faraja katika namna yake na atakuimalisha pia

Ombi langu ni kuwa usimweleze ya kuwa ni mtu gani wamuitaji nasema hivi kwa sababu yeye alishaandika stori nzuri ya maisha yako ata kabla ya wewe kuwepo hapa

Unachokiona kwa sasa huenda yasiwe mateso labda ni ukurasa tu katika kitabu cha maisha yako lipokee tu hili najua zipo bado kurasa nyingi tu zenye tumaini, faraja na ushindi .

Mwisho kabisa fanya ibada kwenye Mwenyezi Mungu mueleze kila hatua uliyopo mwonyeshe jitihada zako katika kukabili kila unalopitia na kuwa mwenye subra

Poleni sana na Asanteni!
 

molwe

JF-Expert Member
Jan 10, 2015
322
500
Sad! Cha kufanya uambie Moyo wako Mungu ndio kila kitu kwangu!! Then please somaa!! Ulizaliwa na Baba na Mama yako na wao ipo siku watakuacha na kurudi kwa muumba wao, sembuse mtu uliekutana nae ukiwa mtu mzimaa!! Nakushauri focus mbelee!! Mungu Baba yetu na akufanyie wepesii!!
 

Humilis

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
681
1,000
Pole sana lakini utateseka maisha yako yote kama una mentality ya mwanaume 'amekuzalisha',amekuharibia maisha,amekuharibia ndoto zako...hukuzaa kwa kushikiwa panga,au hukuingia kwenye hayo mahusiano kwa kutekwa na kulazimishwa...kubali pia hukuchagua mtu sahihi,hukuzaa na mtu sahihi,na hukufanya maamuzi mengi yasiyo sahihi yaliyokufikisha hapo.Wajibika kwa kukubali na kurekebisha makosa yako na usonge mbele.
 

DIKE

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
365
250
Achana nae huyo sio riziki yako. Futa namba zake unfriend katika social network ili usione maisha yake mapya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom