Najuta kumtia umasikini Mama yangu

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
9,679
12,248
Mimi ni kijana Ambae nimezaliwa mwanzoni mwa mwaka 1990. Hapa hapa kwenye jiji la MAKONDA. Japo Baba na Mama yangu Kila mmoja ni mwenyeji wa mkoa wake.

Mama yangu alibahatika kusoma Hadi darasa la 7. Alifanikiwa kusoma typing enzi hizo ilikuwa hot sana kozi hiyo kama ilivyo computer siku hizi. Alisomeshwa hiyo kozi ili atafutiwe kazi ukizingatia kuwa mjomba wake alikuwa na cheo kikubwa TU wizara ya AFYA {R.I.P BABU}

Bahati haikuwa yake kwani katika harakati hizo za kutafutiwa kazi ikagundulika kuwa yeye Mama ni mjamzito. Hapo ndipo maisha yake yalipoanza kuwa ya kawaida nadhani mimba hiyo ilimtoa kabisa kwenye reli😭😭😭

Wenzie aliosoma nao enzi hizo Wana maisha mazuri na majina makubwa mfano Mtendaji mkuu wa NMB. Mh Ruth Zaipuna amesoma na mama yangu darasa Moja.

Nisingekuwa mimi kuja Duniani pengine mama yangu hivi sasa angekuwa mbali sana kimaisha.

Ujio wangu hapa Dunia umefanya mama amekuwa na maisha ya kawaida sana. Amehangaika sana na kwa kiasi Fulani Bado ananihangaikia😭😭😭

Nina huzuni sana licha ya kuwa nimesoma lakini elimu yangu haijanisaidia. Ni kama ubongo wangu umefungwa minyororo nashindwa Cha kufanya😭😭😭

Screenshot_20230815-184933.jpg


Na umri wangu huu nikiumwa ikahitaji milioni 1 TU haki vile nitakufa huku najiona. Umri wa mama yangu unaenda Kwa Kasi itafikia kipindi ataitaji msaada wangu.

Na Mimi Bado najitafuta japo namuomba sana Mungu anisaidie nijipate haraka. Na Nina muomba sana Mungu asimchukue mama yangu kabla sijajipata. Na ni Bora anichukue Mimi kwanza japo natamani sana siku Mungu atakayonichukua anichukue nikiwa nimemuacha Mama yangu pazuri 😭😭😭

Mwenzenu najuta sana kumpa mama yangu UMASIKINI​
 
Kila jambo lina sababu yake,huwezi kujua hiyo kazi kama angeipata ni nini kinge enda kumtokea,huenda Mungu alimnusuru ili asiende kufanya hiyo kazi kwa nia njema kabisa,

Endelea kupambana na usimtupe Mama yako,kwa muda huu ambao hujajipata,kaa na Mama karibu yake na umuongeleshe mambo yatakayo mfurahisha,usipende kusikitika mbele yake au kulaumu ugumu wa maisha mbele yako,mpe hope kua hivi karibuni mambo yatakua mazuri na atasahau machungu yaliyopita,

Vipi mshua wako yeye bado yupo?
 
Kwa asilimia mia moja aliye husika na mateso ya mama ni baba yako. Wewe ni matokeo ya baba yako mjinga.
Simama imara upambane kimaisha, mafanikio yanahitaji kujitoa akili.

Umesema yule Mtendaji wa Nmb alifanyaje na mama? Kujitoa akili kunalipa, muombe mama akusogeze, huyo dada yupo karibu sana na wahindi.
 
Aisee, mda mwingine na mimi napata haya mawazo.....

nimekuelewa sana, pole

jua tu kwamba mbali na yote hayo, mama yako hajutii uwepo wako kwenye maisha yake
Sidhani kama ajutii japo aniambii ila dah. Inatia hudhuni imagine marafiki zangu niliosoma nao 75% wanaajira zinazoeleweka.

Inafikia kipindi mama nikimpigia simu ananiambia mtafute rafiki yako Fulani pengine anaweza kukuunganishia kazi.

Huku huyo rafiki yangu nikiwa Sina mawasiliano nae yoyote SI unajua tena Kila hatua mtu anayo piga anakuwa na marafiki wapya.

Nina miaka 30+ lakini Bado 75% ya maisha yangu IPO mikononi Kwa mama.​
 
Back
Top Bottom