Mifumo ya kidunia ilishaamua mwanaume aishi kwa kukandamizwa na kufanyiwa ulaghai/ udanganyifu

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,417
9,806
Chukulia mfano suala la sex, ile ni starehe ya wote lakini dunia imekua brainwashed kwa kuaminishwa mwanaume anafanyiwa favor ambayo in return inatakiwa kulipia posho, hii posho ya sex wadada wa mjini siku hizi wanaiita matunzo.

Mambo yapo ivyo karibu kila nyanja zinazohusu masuala ya kijinsia na mahusiano. Taasisi zinatetea haki za watoto ukiangalia mkazo mkubwa wameuweka kwa watoto wa kike.

Wanandoa mkiachana kama mali ni za mwanaume zinapigwa pasu kwa pasu ila kama ni za mwanamke hapo mwanaume hapati chochote. Wanasema sababu ni kwamba mwanamke ana haki ya kufidiwa muda na jitihada zake kipindi cha ndoa cha kushangaza muda na gharama alizotumia mwanaume kwenye ndoa iyo iyo hapati fidia yoyote.

Ukiangalia mchakato mzima before, during and after marriage mnufaika mkubwa ni mwanamke lakini jamii imetengenezewa fikra ionekane ananufaika ni mwanaume, ndo hapo mwanaume anatishiwa akiwa bachelor atakapoumwa hakuna wa kumuuguza utafikiri uko kwenye ndoa wanaumwa wanaume tu.

Kwenye suala la DNA napo nishawahi kusikia majibu yakionesha mtoto sio wa mwanaume husika basi mwanaume uyo atadanganywa kuwa ni mtoto wake, wanasema wanalinda masilahi ya mtoto.

Ukija kwenye nasaa za kimaisha tunaambiwa mwanaume kaumbiwa mateso mara kitanda hakizai halamu. Kwamba nibebe mzigo ninaoweza kuuepuka kwa sababu mimi mwanaume? kwamba mwanamke afanye umalaya wake nilee mtoto sio wangu, eti kitanda hakizai halamu.! That is totally bullshit.

Yapo mengi sana yanamkandamiza mwanaume lakini dunia imepotoshwa yaonekane ni kawaida tu. Suala hili halikuonekana tatizo uko zamani kwa sababu mwanamke alikua inferior na mtiifu sana kwa mwanaume.

Kutokana na sera ya 50/50 kushika hatamu kwa sasa wanawake wamekua wabinafsi, wamepandindikizwa chuki na feminists kwamba wanaume ndio wabaya wao hii imewafanya kuwa na roho za kikatili mbaya zaidi washaona mifumo ya kidunia ina loopholes ambazo wakizitumia kimkakati zinaweza kuwapa pesa rahisi au kupata huruma kwa mabaya waliyoyafanya.

Mifano ipo mingi familia ya mzee mengi nusura ipigwe na kitu kizito na klyn, ukiangalia kwa jicho la kosheria inawezekana klyn inawezekana akawa sawa lakini kwa utashi wa kiubinadamu akaonekana ni matapeli.

Dunia ya sasa kwa mwanaume yoyote mwenye ndoto kubwa za kufika mbali kiuchumi basi ndoa ni mtego ambao unaweza kuja kuiangusha himaya yako aliyoijenga kwa miongo mingi.

Kupitia sera ya 50/50 wanawake washapewa access zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa binafsi sioni kama kuna haja tena ya kuwapa victim status kama zamani.

Mifumo ifumuliwe mwanamke nae aangaliwe kama predator kama ilo haliwezekani basi ni wajibu wetu wanaume kuishi na wanawake kwa tahadhari kubwa sana ili tusitumike kama levarage.

Mwanaume tambua ya kwamba mpenzi sio mama yako atakaekua upande wako katika kila hali siku zote za maisha yake. Mpenzi anaweza kusitisha mahusiano muda wowote bila kujali umejitoa au umempambania kwa kiasi gani na hakuna utakachoweza kumfanya.

Hivyo basi ukiamua kumwinua mpenzi wako(kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea nyumba n.k) basi fanya hivyo kwa kiasi ambacho unaweza kuhimili maumivu ya kukipoteza.

Mwanaume usiweke malengo yako kwa mpenzi/mke, hitaji lako kwa mwanamke liishie kwenye kampani ya kijinsia na kuendeleza kizazi chako tu.
 
Usihofu, nature itajishape tu kubalance mambo, kila kitu kina matokeo yake.

Mfano, sasa hivi kuna idadi ya vijana wapo tu wanamaliza vyuo hawana kazi. Kazi zinashikwa na mabinti. Baada ya muda jamii inakuwa na wanaume masikini na wanawake wenye uwezo kiuchumi. Nini kinafata?

Uhaba wa wanaume wenye uwezo wa kumtunza mwanamke, uwepo wa vijana mlenda mlenda na legelege na tegemezi, ongezeko la single mothers, jamii itaanza kuona umuhimu wa uwepo wa wanaume.

Ulinzi wa mtoto wa kiume utaongezeka. Semina za malezi ya mtoto wa kiume na kelele za muandae baba ajae zinashamiri, ajira zitamtazama mwanaume n.k n.k Ni suala la muda tu.
 
Nature find its way always, in the end mwanaume atarudi on top
 
Ndo maana hakuna sababu ya kupanic. Wajibu wetu kama wazazi ni kuhakikisha binti zetu wanaelewa wajibu wao katika jamii na vijana wetu waelewe wajibu wao katika jamii.

Lakini tusisahau kumwezesha binti sababu vijana mlenda mlenda ni wengi sana sasa, ikitokea bahati mbaya akaolewa na mmojawapo au akaolewa akaachwa au akazalishwa na kutelekezwa basi asishindwe kulea mjukuu wako.
 
Hivi watu huwa mnafuatilia Historia ?

Sikubalini na mambo ya 50/50 mimi ni mfuasi wa uwezo wa mtu no matter jinsia yake kama anaweza shughuli fulani basi na apewe kipaumbele......,. Vilevile kuna kazi / shughuli zipo favoured kwa mwanamke au mwanaume kuliko mwanamke....

Lakini historically mfumo dume umemuandama Mwanamke katika mambo mengi sana... hakupewa / na bado kuna Imani hazimpi haki sawa na mwanamme sababu ni mwanamke (kumbuka sisemi upendeleo bali haki sawa) Hivi unajua hata kwenye mambo ya kupiga kura ni miaka gani amepewa hii ruhusa ? Hivi unajua wanasayansi kama Mary Curie walipata shida kiasi gani sababu ni wanawake au wengine wanaume kuchukua credit zao sababu jamii isingewasikiliza sababu ya jinsia zao ?

Kama jamii tunapoanza kushindana na wanawake au wanawake kushindana na wanaume badala ya kusaidiana kupambana na mazingira ni kupotokoa kifikra (na kama ukiniuliza wote tuna mchango mkubwa sana)
 
Ndo maana hakuna sababu ya kupanic. Wajibu wetu kama wazazi ni kuhakikisha binti zetu wanaelewa wajibu wao katika jamii na vijana wetu waelewe wajibu wao katika jamii.

Lakini tusisahau kumwezesha binti sababu vijana mlenda mlenda ni wengi sana sasa, ikitokea bahati mbaya akaolewa na mmojawapo au akaolewa akaachwa au akazalishwa na kutelekezwa basi asishindwe kulea mjukuu wako.
Hii kumwezesha binti, kwanini usiwawezeshe wote? Both gender wa kiume na wa kike? Why always wa kike tu?
 
Nature find its way always, in the end mwanaume atarudi on top
Halafu huwa siamini kuna aliyeko top. Naamini kuna wajibu wa mwanaume na wa mwanamke.

Mwanaume kuwa kiongozi wa familia na mhusika wa kufanya maamuzi ya mwisho hakumfanyi kuwa top, ni jukumu lake tu.

Mwanamke kumlea mwanaume na watoto hakumfanyi kuwa weak, ni jukumu lake tu. Ts all about mgawanyo wa majukumu sio masuala ya kuwa top au weak.

Ni sawa na kusema shingo haina umuhimu kama kichwa.
 
Chukulia mfano suala la sex, ile ni starehe ya wote lakini dunia imekua brainwashed kwa kuaminishwa mwanaume anafanyiwa favor ambayo in return inatakiwa kulipia posho, hii posho ya sex wadada wa mjini siku hizi wanaiita matunzo.

Mambo yapo ivyo karibu kila nyanja zinazohusu masuala ya kijinsia na mahusiano. Taasisi zinatetea haki za watoto ukiangalia mkazo mkubwa wameuweka kwa watoto wa kike.

Wanandoa mkiachana kama mali ni za mwanaume zinapigwa pasu kwa pasu ila kama ni za mwanamke hapo mwanaume hapati chochote. Wanasema sababu ni kwamba mwanamke ana haki ya kufidiwa muda na jitihada zake kipindi cha ndoa cha kushangaza muda na gharama alizotumia mwanaume kwenye ndoa iyo iyo hapati fidia yoyote.

Ukiangalia mchakato mzima before, during and after marriage mnufaika mkubwa ni mwanamke lakini jamii imetengenezewa fikra ionekane ananufaika ni mwanaume, ndo hapo mwanaume anatishiwa akiwa bachelor atakapoumwa hakuna wa kumuuguza utafikiri uko kwenye ndoa wanaumwa wanaume tu.

Kwenye suala la DNA napo nishawahi kusikia majibu yakionesha mtoto sio wa mwanaume husika basi mwanaume uyo atadanganywa kuwa ni mtoto wake, wanasema wanalinda masilahi ya mtoto.

Ukija kwenye nasaa za kimaisha tunaambiwa mwanaume kaumbiwa mateso mara kitanda hakizai halamu. Kwamba nibebe mzigo ninaoweza kuuepuka kwa sababu mimi mwanaume? kwamba mwanamke afanye umalaya wake nilee mtoto sio wangu, eti kitanda hakizai halamu.! That is totally bullshit.

Yapo mengi sana yanamkandamiza mwanaume lakini dunia imepotoshwa yaonekane ni kawaida tu. Suala hili halikuonekana tatizo uko zamani kwa sababu mwanamke alikua inferior na mtiifu sana kwa mwanaume.

Kutokana na sera ya 50/50 kushika hatamu kwa sasa wanawake wamekua wabinafsi, wamepandindikizwa chuki na feminists kwamba wanaume ndio wabaya wao hii imewafanya kuwa na roho za kikatili mbaya zaidi washaona mifumo ya kidunia ina loopholes ambazo wakizitumia kimkakati zinaweza kuwapa pesa rahisi au kupata huruma kwa mabaya waliyoyafanya.

Mifano ipo mingi familia ya mzee mengi nusura ipigwe na kitu kizito na klyn, ukiangalia kwa jicho la kosheria inawezekana klyn inawezekana akawa sawa lakini kwa utashi wa kiubinadamu akaonekana ni matapeli.

Dunia ya sasa kwa mwanaume yoyote mwenye ndoto kubwa za kufika mbali kiuchumi basi ndoa ni mtego ambao unaweza kuja kuiangusha himaya yako aliyoijenga kwa miongo mingi.

Kupitia sera ya 50/50 wanawake washapewa access zote za kiuchumi, kijamii na kisiasa binafsi sioni kama kuna haja tena ya kuwapa victim status kama zamani.

Mifumo ifumuliwe mwanamke nae aangaliwe kama predator kama ilo haliwezekani basi ni wajibu wetu wanaume kuishi na wanawake kwa tahadhari kubwa sana ili tusitumike kama levarage.

Mwanaume tambua ya kwamba mpenzi sio mama yako atakaekua upande wako katika kila hali siku zote za maisha yake. Mpenzi anaweza kusitisha mahusiano muda wowote bila kujali umejitoa au umempambania kwa kiasi gani na hakuna utakachoweza kumfanya.

Hivyo basi ukiamua kumwinua mpenzi wako(kumsomesha, kumfungulia biashara, kumtafutia kazi, kumjengea nyumba n.k) basi fanya hivyo kwa kiasi ambacho unaweza kuhimili maumivu ya kukipoteza.

Mwanaume usiweke malengo yako kwa mpenzi/mke, hitaji lako kwa mwanamke liishie kwenye kampani ya kijinsia na kuendeleza kizazi chako tu.
Uwezo wetu wa kufikiri unaweza kutufikisha mbali sana kama tukifocus kwenye sehemu sahihi. Kila ltu ana uhuru wa kuamua vipaumbele vyake katika maisha yake. Mwanaume hautakiwi kufocus kwenye ngono, au starehe hivo vitu mwachie mwanamke. Mwanaume ukipoteza focus, unaridhika na uwezo wako wa kukabili matatizo unapungua. Focus kwenye kujiongezea thamani watakusumbua mpaka utawakataa. Mwanamke hauhitaji kumuinua, ukiwa mwanaume wa thamani yeye mwenyewe atajua kuwa kuwa na wewe umeshamwinua. Kinachoangamiza afrika ni kuwa hakuna Jando na Unyago tena ndio maana vijana wengi wanapotea.
 
Hii kumwezesha binti, kwanini usiwawezeshe wote? Both gender wa kiume na wa kike? Why always wa kike tu?
Sababu ni Jamii imeshazalisha vijana legelege, wavivu na wasiojali. Vijana wa .com wa kula kimasihara na kukimbia.

Hawa ni vijana wasiotaka majukumu. Iwapo binti yako atajikuta katika mikono ya kijana wa aina hii, akazalishwa, kijana akakimbia, nani atamtunza yule mtoto iwapo mwanamke hana skills za kutafuta kipato?

Sijasema kijana asiwezeshwe, ila binti asiachwe sababu kuna vijana wa sasa hata wenye uwezo wasiojali kuhusu damu zao. Wanazalisha wanakimbia na roho haziwasuti.
 
Hivi watu huwa mnafuatilia Historia ?

Sikubalini na mambo ya 50/50 mimi ni mfuasi wa uwezo wa mtu no matter jinsia yake kama anaweza shughuli fulani basi na apewe kipaumbele......,. Vilevile kuna kazi / shughuli zipo favoured kwa mwanamke au mwanaume kuliko mwanamke....

Lakini historically mfumo dume umemuandama Mwanamke katika mambo mengi sana... hakupewa / na bado kuna Imani hazimpi haki sawa na mwanamme sababu ni mwanamke (kumbuka sisemi upendeleo basi haki sawa) Hivi unajua hata kwenye mambo ya kupiga kura ni miaka gani amepewa hii ruhusa ? Hivi unajua wanasayansi kama Mary Curie walipata shida kiasi gani sababu ni wanawake au wengine wanaume kuchukua credit zao sababu jamii isingewasikiliza sababu ya jinsia zao ?

Kama jamii tunapoanza kushindana na wanawake au wanawake kushindana na wanaume badala ya kusaidiana kupambana na mazingira ni kupotokoa kifikra (na kama ukiniuliza wote tuna mchango mkubwa sana)
Ukiziangalia kwa undani hizi movements za 50/50, women empowerment and the likes utaona kinachoenezwa sio usawa bali ni ubinafsi na chuki za kijinsia. Siku moja niliona habari wanawake wanasema kiwanda chao wana sera ya kuajiri wanawake tu kama chachu ya kuaminisha jamii wanawake wanaweza na wapo proud kabisa kwa kufanya ivyo na watu wengi wanakawapongeza kwenye comments, ukiangalia kazi zinazofanyika hapo hazina uhusiano wa kijinsia, nikajiuliza hii ingekua kinyume chake kwamba wanaume ndio wanafanye je wasingesakamwa kwamba ni wabaguzi wa kijinsia? ndipo nikagundua hili suala la 50/50 kuna sehemu wanawake hawajalielewa. 50/50 maana yake wote mpewe access sawa sawa halafu mwenye uwezo apate shida ni kwamba wanawake wanataka usawa halafu katika kinyang'anyiro cha fursa wanataka waonewe huruma au wapewe upendeleo
 
Back
Top Bottom