Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Apr 21, 2015
11
0
Haujakosea kabisa, Mimi ni below 25, mimi sikubahatika kwenda shule shule ilinishinda kabisaaaa, Mimi sijaoa na sitegemei kuoa leo sababu ya kutooa ni kama haya yaliyomkuta huyu boya, pia mimi naamini katika watoto family yangu na ndugu zangu ni wanangu sio mke.

Kitu kingine dadangu naomba tu unizoee,mimi nna tatizo la kupenda kusema ukweli siwezagi kuongea ili anayeniskiza afurahie na nimekulia uswahilini haswa hivyo ata lugha yangu inaweza kuwa ni tatizo na kibaya zaidi siwezi kuigiza u gentle wakati mimi ni mtoto wa paka naomba tu unizoee ndio dunia ilivyo auwezi kukutana na watu wa aina yako lazima ukute watu tofauti usiowapenda kama mimi.

Kuna watu umu walikuwa wananichukia kupita maelezo ikawa wakiniona mpaka roho zinashtuka kama wameona jini ila baadae taratibu wakanizoea maisha yanaendelea. So ata usiponikubali wachache wanaonikubali wananitosha ndio pamoja na ujinga wangu nnapata likes za kutosha.

Najua pengine nilichocomment kimegusa hali halisi ya maisha yako ila inabidi ujifunze unapokuwa single mother ukapata mtu akakustili akakuweka ndani mpaka mwanao akakutunzia usije ukaanza kumdharau ukaanza kumpanda kichwani ukiona mwanaume kakuoa demu mwenye mtoto ujue kakupa thamani kubwa sana. Otherwise siku akifanya maamuzi hatorudi nyuma na ndio utakuwa mwisho wa kumfanya mjinga, hapo ss urudi kwa ex wako unaejifanya wampenda sana au urudi home ukamsaidie mama kukaanga vitumbua na toto lako linalolelewa na baba wa kambo huku baba yake yupo mzima wa afya mtoto anatunziwa na mbunye bado unampelekea.

Dawa ni kupiga chini tu!
Afadhali nimejua naongea na mjinga, ningejua mapema nisingehangaika
 
Ledwin

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
225
195
Mkuu hata ukimfaham mwanamke kwa miaka kumi anaweza ficha vitu kadhaa na usivifahamu

Mi naomba usimwache mke wako,kwanza achana na huyo jirani AKA MCHEPUKO,Samehe kuwa karibu nae,washirikishe viongozi wa dini,kuhusu kulipa ada huo ni uamuzi wako,ila ningekua mimi ningelipa mtoto asome ,mtoto hana kosa.kwanza kwenda boarding akiwa mdogo hiyo nayo ni tabukidogo.
 
SUZANE

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
742
225
jamani maisha ni magumu ndio maana hata mwenyewe amezaa watoto 2 ili awape huduma zote muhimu!

nakushauri somesha wanao bwana huyo ana bb yk.

kuhusu mahusiano, hapo ndio pagumu ila utashinda tu, usiogope
 
matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,190
1,250
Afadhali nimejua naongea na mjinga, ningejua mapema nisingehangaika
Ata mimi nilitaka kushangaa mama uleyeenda shule kujibizana na mimi.

Ata hivyo bado ujanitendea haki kuniita mjinga, Mimi sio mjinga peke yake mimi ni mjinga mpumbavu. Yani nimechanganya vyote ujinga na upumbavu, so watu kama sisi uitwa wajinga wapumbavu au ukitaka kuokoa muda niite punguwani. Sababu mjinga aliyechanganyika na upumbavu uwa anaitwa punguwani.

Nitendee haki mkuu, niite punguwani.
 
salimkabora

JF-Expert Member
Nov 10, 2012
2,445
1,225
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali
Wewe tafuta mke uoe hata kama sio huyo jirani yako achana na huyo gold digger; faida ya watoto unayo inatosha ukimuendekeza huyo shombe atajakuuwa, hata roho ya kibinadamu hana kabisa na anakuvaa na kukuvua kama koti kuukuu. Mtakutana shuleni kusalimia watoto na utaendelea kuchapa tu kama mwenzio ukitaka
 
Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
13,231
2,000
Mimi mwaka jana kidogo niingie mkenge huo huo, mzee wangu hataki mimi nitafute mke, eti wale wote ninaowatafuta mm hawaamini, sasa akamtafuta mwalimu mmoja wa primary akaniunganisha naye, nikaona haina tabu, nikaongea naye kwa simu, akasema niende kwao tukutane kwao na siku hyo hyo nijitambulishe na nitoe posa!!

( Ni*doubt sana) nikamwambia mzee yy akasema haina shida niende, binti ni mnyantuzu, kazuri sana yan afu kamepanda hewani, kufika kwao, tukala, tukajitambulisha na kutoa posa, tukaaga kuwa tukalale na mwenzangu niliyeenda naye, wazo likaniijia kuwa nifanye uchunguzi juu ya huyo binti na familia yao, wewe!!

ndo nikaambiwa kuwa huyo binti ana mtoto mmoja wa kiume!!! hadi leo sikuwahi kurudi huko, ila mzee alisema kuwa nimuoe tu huyo haina shida, nilikataa kata kata, sioni binti mwenye mtoto hata siku moja...

mkuu pole sana...
Ahaaaaa
Umenifanya nicheke mwee!!!
 
Christine1

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
13,231
2,000
...........huwa sielewi hapo nilipoweka nyekundu, yaani ndoa ni karaha hakuna raha halafu msiachane kwa kisingizio cha ndoa ya kanisa.
Hivi ndoa ni ya watu wawili au kanisa? Haya ni mambo ya kizamani sana aiseee!!
Ni kweli biblia hairuhusu isipokuwa kwa uzinzi na baadhi ya sbb ndoa inavunjwa!ndo maana wanasema maneno hayo...

Japokuwa ckuhizi hayo yamekuwa maneno tu hayatekekezwi wengi tu wanavunja mahakamani na wanaoa na kuolewa upya!!
 
kisungu

JF-Expert Member
Feb 20, 2013
789
225
Kuna majibu matatu, A.muache B, Oa mwingine, C Usimwache.
Kwa upande wangu naona umeshachagua B.
 
skipper

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
660
170
kwanza alikuficha ok may be sio ishu, ila kwa nini aende kuonana na mzazi mwenzie kwa njia za panya....af anakutisha akuone eti kaenda kwao.....kama vipi asepe ila maamuzi ni yako
 
Masterkey

JF-Expert Member
May 5, 2014
1,342
2,000
Mimi hata ndoa ikiwa kesho yani, nikigundua taarifa muhimu kama hiyo, nasamehe kila kitu....
 
jembe_jembe

Senior Member
Apr 14, 2015
176
195
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali

Mkuu, waarabu wamelegea, machotara ndiyo usiseme, sasa ukipata mwenye mkorogo wa vyote viwili yaani mwarabu aliyekua chotara inakua ni sheedar, ungejua ungeomba ushauri kabla. Yote tisa, mmeshaoana na mna watotot, usitake kuisambaratisha familia yako haraka haraka, tafuta kwanza suluhu za makubaliano ikishindikana ndiyo talaka ifuate ni muhimu pia kusingatia maadili ya kidini pamoja na lugha ya kitabia ya huyo mwenzako.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom