Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Hi
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia miimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM Nimeoa na niina watoto wawili huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikuaa zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return.Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie.Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari.Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha.Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo.Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba.Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini.Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena.Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali

Ushauri wangu, kama unampenda mkeo, waite familia waweze kukusaidia, between upande wako na mkeo, halafu hayo matatizo yote ukawaeleza kuweza kupata ukweli na solution,
Jengine hilo la mkeo kwenda kumuona mtoto wake bila ya taarifa yako ni kosa kubwa sana, mi suala hilo naweza kuvunja mguu wa mke wangu na aninusuru, nimeowa kama wewe na mke wangu ana watoto wawili ambao wanaishi na baba yao na mimi ninao wangu wawili, ila mke wangu anapo taka kuwaona hao watoto nakwenda kuwachukua mwenyewe au tunaletewa tukiwa pamoja na mke wangu,hio ndio heshima.
Lakini zaidi maamuzi unayo wewe, pain unayo wewe, ila usikaribie zinaa, hilo sio solutions bali ni matatizo zaidi ki saikology na kwa mungu
 
Pole sana beste ushauri wangu mwache ila tunza watoto wako na kuhusu kuwa na mwingine Fanya uchunguz WA kina na pia hakikisha anajali watoto wako na familia yako. Mweke waz una watoto na una taka Mke anaetaka kuishi na watoto na sii vinginevyo chunguza had kwa wazaz wake kama ana malez mazur
 
Achana nae oa Mtanzania mwenzako, achana na huyo chotara wa kiarabu, aende kwa mwarabu Mwenzake
 
Uamuzi uliofanya sasa ni mzuri na sahihi japokuwa ulikuwa umechelewa,kwa sababu kipindi kile kile ulichogundua kuwa ana mtoto hata kama harusi ni masaa mawili mbele ungevunja mahusiano hayo kuliko sasa...

kama aliweza kukuficha hilo hadi wakat umenogewa amekuficha mangapi na wakat ambao wanaenda mtembelea mtt wao shule halafu huna taarifa unajua wameshakuchakachua mara ngapi??

shukuru hujapata magonjwa ila chapa lapa hapo...thats why huwa sishaur mtu kuoa mwanamke aliyezaa haswa kama huyo jamaa aliyemzalisha yupo dunian,nikujipa maumivu na mateso yanayoweza kukwepwa...

Pia uelewe hata huko kusilimu na kuingia dini yako ni geresha tu. Siku ukimrusha nje jioni yake utamkuta msikitini nawe utabaki na vyeti vyako vya ndoa.
 
si mlikubaliana kwamba ada ya mtoto wake atalipa mwenyewe kabla hamjaoana? sasa nini tena achana nae uyo
 
wazo unaloliwaza mwanzo ndo jibu sahihi.... go a head bro, hapo hupendwi chukua jirani yako haraka... ila hakikisha kwanza kama ataweza kuwalea twins wako, sahau kabisa ilo kahaba la kiarabu: aksante.
 
Baba mkataa pema piga chini hiyo maneno kamata chuma kipya!
 
Ni kosa ambalo sitakuja fanya.
Kuoa mwenye mtoto hapana aiseee maana mbeleni ni matatizo

Temea mate chini my dia omba yasikukute, wasichna wote waliozaa hawana tabia mbaya, na ninyi wanaume ndo mnaowazalisha na kisha kutelekezana. Pole mtoa mada, nakushauri ukae nae umwambie dukuduku lako kuwa hukupendezwa na vitendo vya yeye kwenda na baba wa mtoto shule bila kukutaarifu na pia kuhusu ada mtoto msaidiane kwani maisha yasasa ni kusadiana, angalia atakachokujibu pamoja na mtendo yake then ndo uchuje wewe kam wewe. Asante
 
Temea mate chini my dia omba yasikukute, wasichna wote waliozaa hawana tabia mbaya, na ninyi wanaume ndo mnaowazalisha na kisha kutelekezana. Pole mtoa mada, nakushauri ukae nae umwambie dukuduku lako kuwa hukupendezwa na vitendo vya yeye kwenda na baba wa mtoto shule bila kukutaarifu na pia kuhusu ada mtoto msaidiane kwani maisha yasasa ni kusadiana, angalia atakachokujibu pamoja na mtendo yake then ndo uchuje wewe kam wewe. Asante

"Tema mate chini" hivi huwa ina maana gani kusema hivyo? Ni mkwara au kiapo ama nn?
 
Pole sana Mkuu, kwa maoni yangu uamuzi uliofanya wa kuvunja ndoa ni mzuri. Huyo mama wa kiarabu alikuwa anacheza kote kote huku na kule bila kukutaarifu wewe kwa kuwa alijua ungekuja juu. Kumkuta yeye na huyo aliyezaa naye shuleni na pia kuambiwa walikuwa wakienda pamoja kama familia inayoishi pamoja ni ushahidi tosha kwamba alikuwa anacheza nyuma ya mgongo wako. Kata mti wa fitina na utupe jongoo na mti wake.

Kabisa mkuu. Uaminifu pamoja na nawasiliano ya hapa na pale katika mambo muhimu kama hayo ni Lazima kwenye ndoa au hata mahusiano yalokuwa serious. Sasa tangia mwanzo mtu amemmficha kwanza kama ana mtt mpk alipotaka mwenyewe ndo akamwambia. Then bado anaendelea kufichaficha. Si ajabu hata amepanga amfanye bushoke kumbe huku anaendelea na baba mtt .

Sisi wanawake vitimbi vyetu vinamshinda hata sheitani
 
pole sana kaka.kwa ushauri wangu sioni km ni sahihi kumuacha mkeo kwa kunogewa na penzi jipya.una uhakika gani km huyo mpya uliyempata hatakuja badilika na kuwa tatizo zaidi ya mke wako??.kaa chini na mkeo mpe masharti kuwa km ataendelea kuwa na mahusiano na ex wake ajue ndoa utavunja.na pili simamia msimamo wako khs kutohusika na huduma za mtoto wa nje.nawe kuwa makini na kufanya uchunguz km ukiona bado wanadate na ex wake hapo unaweza kusign out.
 
Bibie ara 1 ada nilipe mimi baba mtoto aende shule kumtazama tena na mke wangu lohoo majanga.Kwanza kubali kataa paulsen.paulsen ni ----- mtozeni ningekuwa mimi hakika ndoa ingevunjika mara baada ya kuwakuta pamoja na baada ya kupata taarifa toka kwa Mwl kwamba wanakuja wote wawili kumwangalia mtoto.

Nimategemeo yangu Paulsen utachukua hatua stahiki haraka bila kuchelewa huyu mwanamke alikuwa anakuchezea muda mrefu.

Mi nitafika hata miaka 50 nje ya ndoa SIZAIIII! Nyie mtoto unavomnyakwa shida baadae anageuka kama kikwazooo! Wanaume mna gubu nyieee, mbona mitoto yenu mnazaa nje mnalelewa?

Hata unune vipi, japo tunashukuru unamuhudumia lakini wewe sio biological father kwake. Biological father japo hana hio ada lakini ana haki ya kumuona mwanae.

Kwa hio huyo dada atakusaidia nini kwa mfano ZAIDI YA KUKUCHUNA? Hata ukimuoa huyo mpora mabwana za watu visa viko pale pale. Hivi hujiulizi kakubali wewe mwenye mke, ukimuoa hato mbwato na mabwana za watu? Unaruka mkojo unanda kukanyaga mavi.
 
Last edited by a moderator:
Rudi mwanzo wa picha, utagundua hata pesa ya ma2miz jamaa alikuwa analamba asilimia kadhaa... Kumbuka mwanamke mweny akili ni mzaz wako pekee, wengne n majambaz. Mteme huyo jambaz mkuu ana meng ya kufanya kwako ikiwemo hasara.
 
Mi nitafika hata miaka 50 nje ya ndoa SIZAIIII! Nyie mtoto unavomnyakwa shida baadae anageuka kama kikwazooo! Wanaume mna gubu nyieee, mbona mitoto yenu mnazaa nje mnalelewa?

Hata unune vipi, japo tunashukuru unamuhudumia lakini wewe sio biological father kwake. Biological father japo hana hio ada lakini ana haki ya kumuona mwanae.

Kwa hio huyo dada atakusaidia nini kwa mfano ZAIDI YA KUKUCHUNA? Hata ukimuoa huyo mpora mabwana za watu visa viko pale pale. Hivi hujiulizi kakubali wewe mwenye mke, ukimuoa hato mbwato na mabwana za watu? Unaruka mkojo unanda kukanyaga mavi.

Nisingelazimisha baba Wa mtoto alipe ada kama najua hana uwezo:-

Mkataba ni baba Wa mtoto kulipa ada, wanaume wengi tukiona mzazi mwenzio kaolewa basi unaona kazi ya matunzo sio take tena
Huyu jamaa amekua akimwambia mke hivyo Mara nyingi na mke hulalamika kuhusu hilo Mara nyingi

Kuhusu kumuona mwanae anaruhusiwa na kuna makubaliano kuhusu hilo ila sio kwa siri na taarifa iwepo
Na kwa nini anikasirikie kila ananiponiona ikiwa ni pamoja na siku ya visiting day?

Nilitegemea tuwe na ukaribu ikiwezekana kushirikishana ktk social events n k na sio uadui

Sijawahi kutaka nitambuliwe kama baba Wa mtoto maana Nina Wa kwangu, ndio maana sikutaka hata akae na sisi
Mtoto Wa form one ni mkubwa anapaswa kuishi kwa baba ake

Kama kuna kukwama kifedha tunasaidiana where necessary

Shortly, you have a point but you are far away disconnected from reality, anyway thank for ur advise
 
kaa na wanafamilia mliweke sawa tatizo hilo kumbuka ushazaa naye watoto tena mapacha na utakapo anzisha familia nyingne fikilia na watoto wako wataishi vip bila uwepo wa mama/baba kuwa karibu nao?.

usikurupuke kuanzisha mahusiano mengne wakat bado unatatizo unaweza ukakutwa na tatizo kama hilo hilo. kuwa makini
 
Back
Top Bottom