Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

kaa na wanafamilia mliweke sawa tatizo hilo kumbuka ushazaa naye watoto tena mapacha na utakapo anzisha familia nyingne fikilia na watoto wako wataishi vip bila uwepo wa mama/baba kuwa karibu nao?.

usikurupuke kuanzisha mahusiano mengne wakat bado unatatizo unaweza ukakutwa na tatizo kama hilo hilo. kuwa makini

Sakata hili Lina muda mrefu sana ndugu, tumeshasuluhishwa mpaka basi
Yet ugomvi unarudi pale pale
 
Nisingelazimisha baba Wa mtoto alipe ada kama najua hana uwezo:-

Mkataba ni baba Wa mtoto kulipa ada, wanaume wengi tukiona mzazi mwenzio kaolewa basi unaona kazi ya matunzo sio take tena
Huyu jamaa amekua akimwambia mke hivyo Mara nyingi na mke hulalamika kuhusu hilo Mara nyingi

Kuhusu kumuona mwanae anaruhusiwa na kuna makubaliano kuhusu hilo ila sio kwa siri na taarifa iwepo
Na kwa nini anikasirikie kila ananiponiona ikiwa ni pamoja na siku ya visiting day?

Nilitegemea tuwe na ukaribu ikiwezekana kushirikishana ktk social events n k na sio uadui

Sijawahi kutaka nitambuliwe kama baba Wa mtoto maana Nina Wa kwangu, ndio maana sikutaka hata akae na sisi
Mtoto Wa form one ni mkubwa anapaswa kuishi kwa baba ake

Kama kuna kukwama kifedha tunasaidiana where necessary

Shortly, you have a point but you are far away disconnected from reality, anyway thank for ur advise
hapa kila mtu ana mawazo yake kulingana na uzoefu au kuona jirani yake,unaweza kuoa huyo jirani ila nae akizaa anaweza kubagua watoto, pia huyo wa kwanza atakuwa na jambo na huyo alie zaa nae, maana asingeenda kimya shule bila ufahamu wako, muhimu ni wewe unajisikiaje kwa sasa, fata fikra zako na zitakuwa sahihi!!
 
Ni kosa ambalo sitakuja fanya.
Kuoa mwenye mtoto hapana aiseee maana mbeleni ni matatizo

Omba sana Mungu maana uchakachuaji siku hizi wanawake wanatumia mbinu nyingi wasionekane wamezaa, Mojawapo akijifungua hanyonyeshi mtoto bali anampa maziwa ya kopo, hali hii humfanya matiti yasichuke. Wengine hupaka dawa kufanya uzazi uwe tight. Wengi wao huishi mbali na watoto wao na wakikutana na watoto wanamwita dada wakati yeye ni mama aliyemzaa. Oa mtu unayemjua angalau background yake toka utotoni.
 
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali

mimi nikushauri mdogo wangu,sio vyema kumwacha huyo mke wako,kwa njia moja au nyingine dini haituruhusu kuachana,pili tafakari sana juu ya watoto wako je! wataathirika kwa kiasi gani?

unajua kabla ujachukua maamuzi yeyote maishani ni vyema ukaesabu gharama ya jambo unalotaka kulifanya ili mwisho wa siku usije ukajuta kwa maamuzi yako,wewe kama wewe utafurai kwa kupata penzi jipya lakini jiulize hili swali je!na huyo mwanamke akija kusababisha madhara makubwa juu ya watoto wako,utakua umetibu tatizo au umezidisha tatizo?jiulize haya maswali kwanza kabla hujachukua maamuzi ya kumwacha mkeo;

mimi na kushauri mkalishe mke wako,myazungumze na kutafuta suluhu kuliko kumwacha na kuoa mwanamke mwingine, ukipenda boga penda na ua lake,kumbuka siku mnafunga ndoa,ulisema nitakupenda kwenye shida na raha tabu na magonjwa,kifo ndio kitutenganishe,je! hayo umeyasahau mdogo wangu?

upendo wa kweli upimwa katika kasoro na mapungufu,
husimwache mkeo tafuta suluhisho Mungu akuongoze;
 
Ninavyoelewa, mwanamke mwenye mtoto ni shida kwani bado yule mzazi mwenzie anahusika nae katika kulea mtoto ikiwa ni pamoja na kupata haki ya penzi. Na ni rahis kumpa nafasi hiyo kama nija ya kupata matumizi ya mtoto. Na wakati mwingine mzazi mwenzie anatumia kigezo cha matumizi ya mtoto kulazimisha tendo la ndoa.
 
Umemzungusha sana, kafanywa 'mume bwe.ge'

Hiki kimbembe si mchezo!Wewe umelemaa mpaka mkeo anakupanda kichwani mkuu??Na kwanini umlipie wewe ada huyo mtoto wa kufikia wakati babaake mzazi yupo??

.Ingelikuwa baba mzazi hayupo kwenye picha ningeelewa lakini mtu anajileta anapotaka halafu mwanawe ashindwe kumuhudumia huyo mke wako ni mwanamke hovyo nae hajielewi kabisa anacheza faul kotekote bana!!Na ww kwasababu umegombana na mkeo usihalalishe uzinzi wako huijui miiko ya ndoa yako??

Nadhani huyo mwanamke keshakujua anaweza kukupelekesha utakavyo na ndo maana anakufanya hivo inabidi mkae na umuwekee mipaka imara kama baba mtoto anataka kutoa huduma ipitie kwako,na mkeo mpige marufuku kupanga miadi na ex wake bila uwepo wako ni lazima akushurikishe kwenye kila kitu.Na kama hawezi hayo abebe virago na asirudi this time!!
 
Mi nitafika hata miaka 50 nje ya ndoa SIZAIIII! Nyie mtoto unavomnyakwa shida baadae anageuka kama kikwazooo! Wanaume mna gubu nyieee, mbona mitoto yenu mnazaa nje mnalelewa?

Hata unune vipi, japo tunashukuru unamuhudumia lakini wewe sio biological father kwake. Biological father japo hana hio ada lakini ana haki ya kumuona mwanae.

Kwa hio huyo dada atakusaidia nini kwa mfano ZAIDI YA KUKUCHUNA? Hata ukimuoa huyo mpora mabwana za watu visa viko pale pale. Hivi hujiulizi kakubali wewe mwenye mke, ukimuoa hato mbwato na mabwana za watu? Unaruka mkojo unanda kukanyaga mavi.

Sawa sawa lara...huyu jamaa amuweke chini mke wake ajue tatizo lake ni nini

Lakini always haya matatizo chanzo chake huwa kama kitandani hapako vizuri

Kama ameshindwa kazi ya kunako 6*6 haya ndiyo matokeo

Mke wako ukimtimizia vizuri kitandani na matumizi ya kawaida kamwe hawezi toka nje

Jitathimini mkuu

Huyo jirani anakuchuna tu
 
Daah mm niliyakimbia haya nilimkuta binti anamtoto nikampenda ila nilikuja kuzaa nae ila kabla ya kuoa nikahis kuna madudu hapa yatafanyika au yanafanyika nikamsepa bora nikaoa ila namtumia matumizi tu ya mtoto pole broo
 
Duu? Umeenda mbali mkuu
Nikusahihishe tu kwa yafuatayo:-

Argument yangu kubwa ni kuhusu ada ya mtoto na si babake kumuona
Nimeanza kumlipia mtoto akiwa standard 4 ungependa nikutajie gharama?
Ni kubwa mno, sasa anaingia sekondari mimi pia watoto wangu wanatakiwa ada six million wote wawili
Baba Wa mtoto ana uwezo na anawalipia watoto aliozaa na mkewe iweje adhindwe huyu Wa nje?

Kuhusu kitandani mungu akusamehe, siwezi kujisemea mwenyewe ila tu niseme sio kila tatizo kwenye ndoa limetokana na mtu kushindwa kumridhisha mwenzie
Maana umesema kwa uhakika kabisa as if tunaishi pamoja unatufaham kwa undani.

Nakusamehe in advance for this irritating comment
N.b hakuna pahala nimelalamikia usaliti nimeeleza kwa kina kuwa ugomvi wetu ni ada ya mtoto wake na mzazi mwenzie,
Mengine ni Maelezo ya kukusaidia kuelewa uzito Wa tatizo ili ushauri accordingly
 
Mkuu look at the bigger picture

Hapo kuna Usaliti...Kama huuoni labda ni kwa namna wewe ulivyoiandika hii stori inatufanya tufikirie hilo.

Why akufiche kwenda kuonana na baba Mtoto?

Hapo kuna tatizo...na tatizo hili ni la ndani...la kwenye pichu...ndio limesababisha haya yote....

Kaa na mke wako...Usimwache mke wako.....hadi pale inapobidi sana....utawatesa watoto mno.....Msimamo wako usilipe tena ada....Ulikosea tangu mwanzo wewe mwenyewe kukiuka hayo makubaliano na kuanza kulipa....Yo have set the precedence......

Usimwache mkeo isipokua tu utakapothibitisha kuna zinaa
 
tatizo ni huyo mwanamke kufanya mambo na mzazi mwenzake bila kukkwambia kwanza muulize wife anamsimamo gani then fanya maamuzi kumbuka pia una watoto so kuwa na hekma katik kuamua
 
Daah mm niliyakimbia haya nilimkuta binti anamtoto nikampenda ila nilikuja kuzaa nae ila kabla ya kuoa nikahis kuna madudu hapa yatafanyika au yanafanyika nikamsepa bora nikaoa ila namtumia matumizi tu ya mtoto pole broo

Hapa kuna kitu cha kujifunza katika hili. Duh hata mimi kuna rafiki yangu yupo ktk mchakato wa kuoa mke aliye kwisha zaa na jamaa mwingine. Anahitaji kushauriwa.
 
Eeeehh wanawakee Pasua vichwa aisee......Ila wachki watoto wako kwa maitaji mazuri km shule Nk,
 
Hivi ndugu mlipokuwa mnachumbiana ulimwonesha msimamo gani? Au ndio nyie ndio wale mnaoigiza maisha ya soap opera? Kwa taarifa yako mchoro wote tangu kuhamishiwa mtoto kwako na wewe kumsomesha ulipangwa na mme mwenza wewe ukitumika kama zuzu na ATM. Na inawezekana kabisa hata hao watoto wengine unaowaita wa kwako kuna mkono wake huyo mme mwenza wako na yumkini huko kuonekana kama mtu na mke hakuishii kwenye kumtembelea mtoto peke yake. Fanya uchunguzi utajua Mengi zaidi. Kumbuka kuwa walioanzisha mfumo dume hawakuwa wajinga kama wanaharakati wanavyotaka kuaminisha watu.
 
Mkuu look at the bigger picture

Hapo kuna Usaliti...Kama huuoni labda ni kwa namna wewe ulivyoiandika hii stori inatufanya tufikirie hilo.

Why akufiche kwenda kuonana na baba Mtoto?

Hapo kuna tatizo...na tatizo hili ni la ndani...la kwenye pichu...ndio limesababisha haya yote....

Kaa na mke wako...Usimwache mke wako.....hadi pale inapobidi sana....utawatesa watoto mno.....Msimamo wako usilipe tena ada....Ulikosea tangu mwanzo wewe mwenyewe kukiuka hayo makubaliano na kuanza kulipa....Yo have set the precedence......

Usimwache mkeo isipokua tu utakapothibitisha kuna zinaa

Well, kwa nn unasema nisimwache mke wangu hadi nithibitishe amezini wakati juu umesema in a big picture kuna zinaa?

Kumwacha mke wangu kunatokana na kushindwana kwetu juu ya gharama za malezi ya huyo mto, kuzini hata asingekua na huyo mtoto anaweza kuzini tu
Na pengine hata humu ndani watu wengi wana migogoro ya uzinzi wanajua wenyewe inavyotatulika
Hakuna mtu kati yetu alieoa au kuolewa anaweza kusimama kifua mbele kusema kuwa mwezie ni mwaminifu 100%

Tunaishi kwa imani tu na wenzetu
Ivyo ndugu addict namuacha mke wangu kwa kuushindwa mgogoro niliohangaika nao kwa miaka kadhaa Wa mtoto wake

Huyu mtoto amegeuka mwiba kwa maisha yangu na watoto wangu tumekwenda kila sehemu unayoijua kusuluhishwa imeshindikana
Hivyo simuachi mke wangu kwa uzinzi namuacha kwa kuwa mtoto wake kawa kikwazo cha furaha ya familia yangu

Wachangiaji wengi wameshauri sawa sawa na nilivyoamua
Huyo mtoto bado ana safari ndefu ya maisha ina maana tutasumbuana siku zote za maisha ya huyu mtoto

Kama ingekua ni uzinzi pekee na si mtoto basi wala usingeniona hapa nawashirikisha katika hili
 
some people in this thread are INSENSITIVE,INCONSIDERATE and IGNORANT.....
 
Hivi ndugu mlipokuwa mnachumbiana ulimwonesha msimamo gani? Au ndio nyie ndio wale mnaoigiza maisha ya soap opera? Kwa taarifa yako mchoro wote tangu kuhamishiwa mtoto kwako na wewe kumsomesha ulipangwa na mme mwenza wewe ukitumika kama zuzu na ATM. Na inawezekana kabisa hata hao watoto wengine unaowaita wa kwako kuna mkono wake huyo mme mwenza wako na yumkini huko kuonekana kama mtu na mke hakuishii kwenye kumtembelea mtoto peke yake. Fanya uchunguzi utajua Mengi zaidi. Kumbuka kuwa walioanzisha mfumo dume hawakuwa wajinga kama wanaharakati wanavyotaka kuaminisha watu.

Mkuu hata ukimfaham mwanamke kwa miaka kumi anaweza ficha vitu kadhaa na usivifahamu
Hivyo nakubaliana na ww ila tu unaweza chunguza hata miaka mia na usielewe
Watoto wangu tunafanana ukiwaona unaweza kukimbia mbio, na kwetu gumbo zima tumepata mapacha ikiwemo Mimi na hadi Dada zetu
 
Dah, naanza kuogopa, wangu kasema kaongea na mama mkwe wake wa zamani wa aliyezaa naye, na wamecheka sana.
 
Back
Top Bottom