Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Apr 17, 2015
10
64
Waheshimiwa habari za mida,

Mimi ni IT specialist kwenye shirika moja lisilo la kiserikali mshahara wangu ni wa kati si mkubwa sana wala si mdogo sana. Lakini pia mimi ni lecturer part time nafundisha jioni wafanyakazi katika chuo kimoja hapa DSM, Nimeoa na nina watoto wawili, huyu mke wangu ni chotara wa Kiarabu.

Wakati tumeanza kudate hakuniambia kama ana mtoto na kwa kweli alivyo mzuri sikutilia shaka kama ana mtoto maana hata nyonyo zake zilikua zimesimama kama mtoto anaebalehe.Baadae mapenzi yaliponoga ndipo akaniambia kuwa ana mtoto alie darasa la kwanza yupo kwa mama mzazi yaani bibi wa mtoto.

Kwa kuwa nilikua tayari nimezama kwenye mahaba mazito ikabidi nikubali tu maana by that time nilishatangaza ndoa ilikua ni point of no return. Ila mchumba alinihakikishia kuwa mtoto wake hatakua kikwazo kwenye ndoa yetu na kwamba huduma zote za malezi ikiwa ni pamoja na shule, malazi, maradhi na mengineyo yatakua chini ya baba wa mtoto.

Huo ndio ukawa mkataba wetu na kwamba mtoto ataishi kwa bibi na baadae atahamia kwa baba mzazi ambae ni Mwarabu mwenzie. Akabadli dini kuja ukristo tukafunga ndoa haikua shida maana mama ake pia ni mkristo baba ndio muislam na aliwatelekeza siku nyingi.

Miezi sita baada ya ndoa akamleta mtoto kwetu kuishi permanent kinyume na mkataba wetu, anyway nikawa na roho ya utu nikasema haina shida kuepusha shari. Mtoto wake alipofika darasa la nne wakampeleka boarding sisi hapo tuna watoto wawili mapacha wa miaka minne kasoro nadhani mimi ndie nililipa ada ya boarding.

Siku moja katikati ya wiki nilibeba mahitaji kadhaa nikampelekea yule mtoto shuleni, niliomba wakaniruhusu kuingia pale Surprisingly Matron akaniambia huyo mtoto mbona ana vitu vya kutosha. Mama yake na baba yake walikua hapa juzi siku tano hivi zimepita. Akaniuliza kwani wewe ni nani wa mtoto nikamweleza, akashangaa akaniambia mbona walikua wamekaa na mtoto kama ni familia inayoishi pamoja.

Akanipa kama umbea flani hivi nilishangaa kwa kuwa mke wangu hakuniambia kama alienda kwa mtoto na mzazi mwenzie alikuwepo. Visiting day moja nikaenda na watoto wangu kumuona mwenzao, mke wangu aliondoka mapema akatangulia tulipofika pale tukakuta jamaa nae yupo wamekaa na mtoto na wife.

Mshikaji akaaga bila kunisalimia akaondoka zake nilishindwa kumwelewa, nikazuga tukaendelea na mengine hatimae yule mtoto akamaliza la saba. Mama yake akamtafutia shule nzuri sana yenye matokeo mazuri kila mwaka kimbembe kikaja kwenye ada, mimi nikamwambia mwisho wangu ilikua ni la saba.

Sasa walipe wenyewe maana watoto wangu pia wameanza shule ya Mapadre Lieberman ada wote wawili ni million sita kwa mwaka bado nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo nalipa mimi ingawa ana mkopo asilimia ishirini. Bado gharama za uendeshaji familia za kila siku, hivyo nikamwambia sitaweza kulipa, ni vema babaake ajipange kulipa.

Wakuu kwa kauli yangu hiyo ulizuka mgogoro mkubwa, Huduma zote muhimu nilisitishiwa pamoja na za chumbani akaondoka akarudi kwao kwa mwezi mzima baada ya kusuluhishwa akarudi mimi nikashikilia msimamo kuwa silipi ada.

Hivi karibuni wakati hayupo nimeingia kwenye mapenzi na mdada jirani yangu amepanga upande anaishi na ndugu, wife amerudi sina hamu nae tena. Huyu mdada jirani nimekua nikimpa lift asubuhi kwa muda mrefu sasa na ndipo tukaelewana na anajua matatizo yetu, alikua akitusaidia sana nyumbani wakati wife ameondoka.

Nimedhamiria kumuacha wife mazima nimeshachoka, juzi baba amekuja akaniambia nilikushangaa ulipojifanya mjuaji kuoa mwanamke mwenye mtoto tukakuzuia ukalazimisha sasa umeyaona.

Wakuu nipo njia panda, ushauri tafadhali
 
Pole sana Mkuu, kwa maoni yangu uamuzi uliofanya wa kuvunja ndoa ni mzuri. Huyo mama wa kiarabu alikuwa anacheza kote kote huku na kule bila kukutaarifu wewe kwa kuwa alijua ungekuja juu. Kumkuta yeye na huyo aliyezaa naye shuleni na pia kuambiwa walikuwa wakienda pamoja kama familia inayoishi pamoja ni ushahidi tosha kwamba alikuwa anacheza nyuma ya mgongo wako. Kata mti wa fitina na utupe jongoo na mti wake.
 
Hiki kimbembe si mchezo!Wewe umelemaa mpaka mkeo anakupanda kichwani mkuu??Na kwanini umlipie wewe ada huyo mtoto wa kufikia wakati babaake mzazi yupo??

Ingelikuwa baba mzazi hayupo kwenye picha ningeelewa lakini mtu anajileta anapotaka halafu mwanawe ashindwe kumuhudumia huyo mke wako ni mwanamke hovyo nae hajielewi kabisa anacheza faul kotekote bana!!Na ww kwasababu umegombana na mkeo usihalalishe uzinzi wako huijui miiko ya ndoa yako??

Nadhani huyo mwanamke keshakujua anaweza kukupelekesha atakavyo na ndo maana anakufanya hivo inabidi mkae na umuwekee mipaka imara kama baba mtoto anataka kutoa huduma ipitie kwako,na mkeo mpige marufuku kupanga miadi na ex wake bila uwepo wako ni lazima akushurikishe kwenye kila kitu.Na kama hawezi hayo abebe virago na asirudi this time!!
 
Ni baadhi Mkuu si wote wako hivyo, kwa mfano unaweza kujenga penzi zito na dada ambaye yule aliyezaa naye hayuko tena duniani, ila ni mtihani mgumu kusema kweli kwa sababu baadhi ya wanaume hawapendi kumuona mzazi mwenzao akiishi katika raha na starehe hivyo watata futa sababu za kuanzisha tafrani ambazo bila shaka zitakugusa wewe kama mume na kuiona ndoa yote chungu.

Ni kosa ambalo sitakuja fanya.
Kuoa mwenye mtoto hapana aiseee maana mbeleni ni matatizo
 
Back
Top Bottom