Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Najuta kuoa mwanamke mwenye mtoto

Umelibeba furushi hilo. Mapenzi upofu lakini lazima ujiwekee vigezo kabla ya kuanza kutafuta mwenza.
 
Mi nitafika hata miaka 50 nje ya ndoa SIZAIIII! Nyie mtoto unavomnyakwa shida baadae anageuka kama kikwazooo! Wanaume mna gubu nyieee, mbona mitoto yenu mnazaa nje mnalelewa?

Hata unune vipi, japo tunashukuru unamuhudumia lakini wewe sio biological father kwake. Biological father japo hana hio ada lakini ana haki ya kumuona mwanae.

Kwa hio huyo dada atakusaidia nini kwa mfano ZAIDI YA KUKUCHUNA? Hata ukimuoa huyo mpora mabwana za watu visa viko pale pale. Hivi hujiulizi kakubali wewe mwenye mke, ukimuoa hato mbwato na mabwana za watu? Unaruka mkojo unanda kukanyaga mavi.
 
Pole sana mkuu. Ni kweli baadhi ya wanandoa ambao mwanzo walikuwa na wapenzi na hadi kuzaa nao watoto pindi wanapoolewa/kuoa tena bado huwa na mahusiano na hao wapenzi wao wa zamani. Hii hutokana na sababu kwamba wanakuwa waliachana huku wakiwa bado wanapendana kwa kiasi fulani.

Km ni kweli una ushahidi tosha kuwa anatoka kimapenzi na mpenz wake wa zamani na kwa kuwa hadi maandiko matakatifu toka kwenye biblia yanasena mtu hatamwacha mwenzi wake ila tu ikiwa ni kwa sababu ya UZINZI.

Kaa naye umuulize na muongee vizuri. Kama atakiri na kukuomba msamaha basi MSAMEHE. Kama hatakiri basi ruhusu nafsi yako ifanye maamuzi
 
Damu ni nzito kuliko maji aisee. Mwanamke akishazaa yule motto atakuwa kiunganishi kati ya mwanaume na mwanamke hata kama wameachana ipo siku watakutana na kukumbushia Enzi zao tu.

Nyie wote mliooa wanawake wenye watoto na wanaume wengine imekula kwenu. Kubalini kusaidiwa mara moja moja kwa sababu huwezi kujua walianzia wapi mpaka wakazaa mtoto.
 
Ni kosa ambalo sitakuja fanya.
Kuoa mwenye mtoto hapana aiseee maana mbeleni ni matatizo
kwani wangapi wameoa wanawake wa kawaida tu ila still ndoa zao zimejaa mapichapicha kama filamu ya nsyuka?....mkuu cha msingi ni kuomba tu kupata mwanamke anaejielewa....kuna watu wameoa wanawake wenye watt na ndoa zao zina amani,wanaishi bila matatizo
 
Utaaacha wangapi bro dawa ni kusuhisha tatizo kama mwarabu atajirekebisha endelea kuishi nae fikiria watoto wko msamehe tu.
 
Ulikosea toka mwanzo ulipoendelea kulipa ada hata baada ya kujua njemba mwenzako hukutana na mkeo kwa siri. Hilo tu lingetosha kumtimua. Sasa mkuu achana na mambo ya wanawake. Huyo mwarabu akitaka kurudi sawa, ila ada ya mwanae usilipe. Arudi ajili ya watoto wenu tu. Kuhusu jirani endelea kula starehe usithubutu kuvuta ndani. Concentrate kwenye career yako na maisha yako na wanao. FULLSTOP.
 
umepoteza hamu kwa mke wako kutokana na vitu alivyokufanyia au baada ya kunogewa na penzi la jirani?..umejiridhisha kuwa huyo jirani ana mapnz ya dhati?asije nae akawa ameamua kukamata fursa tu...jaribu kufix ndoa yako kwanza mkuu..ikishindikana piga chini ndo ujimuvuzishe kwa jirani..unachofanya sasa ni uchepukaji ambao mkeo akijua inaweza ikawa ndo fimbo ya kukuchapia..
 
kwani wangapi wameoa wanawake wa kawaida tu ila still ndoa zao zimejaa mapichapicha kama filamu ya nsyuka?....mkuu cha msingi ni kuomba tu kupata mwanamke anaejielewa....kuna watu wameoa wanawake wenye watt na ndoa zao zina amani,wanaishi bila matatizo

Ni kweli kabisa wengi wanakosea kuhukumu watu wote kwa kosa la mtu mmoja huyu jamaa alipagawishwa na mvuto wa binti na kwa kweli hakufanya maamuzi ya busara na hakuwa na msimamo alipaswa achunguze mahusiano ya huyo mwanamke na ex wake....na mipaka ilitakiwa iwekwe tangia mwanzo sasa hivi naona mambo yamekuwa msawajiko na yeye anaharibu zaidi kucheat!!
 
Nyinyi baadhi ya wanaume nyinyi! unaanzaje kufikiria kumuoa mwanamke ambaye tayari amezaa nje? anyway bwana mkubwa pole sana kwasababu haukulifahamu hill kabla,wasichana no weeengi mno was kutosha kabisa kuoa hata ukitaka wanne utawapata ila mind you,hawa maconcubines hawa ambao mnapokutana wanasema hili ila mkishakaa wanageuka kama bendera msijaribu, usiijaribu ndoa yako ni sumu,ndoa haijaribiwi jamani
 
Piga chini mdau
Waarabu siyo watu angalia wasije kukunyonya damu
We jipigie tu jiran huyo
 
Wewe na huyo mkeo mlikua hampendani tu. Kama mngekua na mapenzi ya kweli yote uliyosema yasingetokea. Watu wanaoa wanawake wana watoto hata wawili na wanakaa raha mustarehe wanazaa na kujukuu
 
Back
Top Bottom