Najuta kuifahamu stand ya Mwenge

Najuta kuifahamu stand ya Mwenge

binafsi nikiwa mazingira hatarishi vitu vya thamani nahamishia ghorofani, mtu kugusa mfuko wangu wa shati inabidi ajitoe muhanga haswaa!
 
Hahah mwana wa abajato acha woga. Mimi toka mwana 2012 huwa nikipanda daladala nina i phone 4 nai pa na sijawahi kuibiwa . Sijisifii manake najua wanaweza kuniotea kama walivyoweza kunipiga passport ila hii ya kupanda dala dala na pp kijiti manake unawaogopa na mbinu zao huzijui

Hamna wewe...si kwamba nawaogopa. Ni kwamba hao jamaa ni lazima uwe dakika tano mbele yao la sivyo ukijifanya gangwe eti huwaogopi unaweza kula hasara ya kijinga ambayo ingeweza kabisa kuepukika.

Kukurukakara za kudandia daladala unazijua lakini?
 
Kuna jamaa yangu moja tulikuwa tumepanga nyumba moja pande za Tangi bovu. Yeye alikuwa ni mtu wa viwanjana sana. Siku moja mida mibovu kashuka pale mwenye. Wahuni wakamdandia, walimpiga roba moja matata sana wakampora kila kitu. Kurudi home akaamka kidogo afadhali. Ile kufika usiku wa saa saba siku iliyofuata aliamka akatumsha wapangaji wenzeke akawa anatueleza aoni vizuri, anaona giza tu, shingo imekataa kugeuka. Usiku huo huo tukamkimbiza masana hospital. Mwenge toka zamani ni noma.
 
10.jpg
 
Jana katika mizunguko yangu, nimetoka banana Ukongo mida ya jioni kuelekea Bunju. Kufika Mwenge kukawa na usafiri wa shida sana. Mara gari ya Bunju hiyo.

Abaria tukaanza kufanya mahaba ya kuikumbatia gari toka lango la kungilia mpaka karibu na yanapo paki mabasi ya Tegeta, Bunju ndani ya kituo cha mwenge, sababu konda aligoma kufungua mlango tupande pale yanapo ingilia mabasi.

Baada ya mlango kufunguliwa likatokea purukushani la kufa mtu kuakikisha kila moja anawahi siti. Ile kufika ndani tu najikagua mifukoni Simu yangu holaa, nikaseach mpaka mifuko ya nyuma holaaa.

Najiangalia mfuko mwingine elfu hamsini hola. Nikachoka ghafla nikafa kiumee kimya kimya huku nikipata upweke wa kukosa kuperuzi JF. kwa bahati nzuri mfuko wa shati kulikuwa na ATM card na elfu mbili.

Ndugu zangu, Naaaaaaaajuuuuuuuuuutttttaaaa kuuuuuuuuiiiifahammuuuu Mweengeee Stand.

Pole sana mkuu.
Kinachowafanya watanzania msipange foleni wakati wa kupanda daladala ni kitu gani?
Mbona sisi Nairobi tunapanga foleni kupanda matatu?
Mtaendelea kuibiwa sana hadi mtakapobadilika.
Badilikeni
 
Ah wapi! Mi mtoto wa town wewe. Mwana Abajaro wa zamani. Nimezipiga sana na Kiboko Msheli.

Mbinu zote wanazozitumia nazijua. Sipandi daladala na chochote cha thamani zaidi ya pipi kijiti.

Ha ha ha ha, haya mtoto wa Abuja (sinza kwa wajanja)ila mitandao ya simu kila siku inakupiga 250 za nyimbo na sms za ujanjanujanja!! ha ha ha!
 
Vijana hawana ajira, kwa kipindi hichi wameamuwa kwa dhati kabisa kujikita katika hajira hii.
 
Ah wapi! Mi mtoto wa town wewe. Mwana Abajaro wa zamani. Nimezipiga sana na Kiboko Msheli.

Mbinu zote wanazozitumia nazijua. Sipandi daladala na chochote cha thamani zaidi ya pipi kijiti.
hehehehe wanasema boni hia hia......Mwenge nilikua najiachia sana kabla sijawa na usafiri binafsi wa mkopo wapiga ndole wote wale wanafyata....Ishu ni kujielewa tu sio unakua unajiachia kama upo sebuleni kwako lazima wakulize.
 
Ha ha ha ha, haya mtoto wa Abuja (sinza kwa wajanja)ila mitandao ya simu kila siku inakupiga 250 za nyimbo na sms za ujanjanujanja!! ha ha ha!
Mimi nliwaambia watoe manyimbo nyimbo yao kwenye line yangu
 
hehehehe wanasema boni hia hia......Mwenge nilikua najiachia sana kabla sijawa na usafiri binafsi wa mkopo wapiga ndole wote wale wanafyata....Ishu ni kujielewa tu sio unakua unajiachia kama upo sebuleni kwako lazima wakulize.

Hahaaa
 
Kwa stand ya mwenge inakufahamu wewe?usijute kuifahamu mwenge stand juta kupandia gari maeneo hayo

Pole lakini mkuu
 
Mjini bana ukilizwa huwa unajicheka mwenyewe na kuona wapi ulipokosea
 
Jana katika mizunguko yangu, nimetoka banana Ukongo mida ya jioni kuelekea Bunju. Kufika Mwenge kukawa na usafiri wa shida sana. Mara gari ya Bunju hiyo.

Abaria tukaanza kufanya mahaba ya kuikumbatia gari toka lango la kungilia mpaka karibu na yanapo paki mabasi ya Tegeta, Bunju ndani ya kituo cha mwenge, sababu konda aligoma kufungua mlango tupande pale yanapo ingilia mabasi.

Baada ya mlango kufunguliwa likatokea purukushani la kufa mtu kuakikisha kila moja anawahi siti. Ile kufika ndani tu najikagua mifukoni Simu yangu holaa, nikaseach mpaka mifuko ya nyuma holaaa.

Najiangalia mfuko mwingine elfu hamsini hola. Nikachoka ghafla nikafa kiumee kimya kimya huku nikipata upweke wa kukosa kuperuzi JF. kwa bahati nzuri mfuko wa shati kulikuwa na ATM card na elfu mbili.

Ndugu zangu, Naaaaaaaajuuuuuuuuuutttttaaaa kuuuuuuuuiiiifahammuuuu Mweengeee Stand.

Halafu Vibaka Wa Pale Mwenge Wanakula Na Askari Wa Kile Kituo Kidogo Cha Pale Mwenge,
 
Pole sana Mkuu,

Inakera na kukasirisha sana kuibiwa tena ukiwa umechoka
 
Mmenikumbusha nilipotaka kuibiwa mtaa wa Kongo,muuza mitumba mmoja akajifanya nimemkanyaga akaning'ang'ania na wenzake wakaja kunizonga.Hawakuamini nilipowahika mashati nikawavuta wote mbele yangu nikachimba mkwara kwa sauti ya juu.."Hatufahamiani humu mtasambaa sasa hivi..."
Wakaomba radhi kiaina nikawaacha.
Sipati picha wangejua kuwa sikuwa na lolote la kuwafanya ingekuwaje
 
Back
Top Bottom