Najuta kuifahamu stand ya Mwenge

Najuta kuifahamu stand ya Mwenge

Mwenge stendi ni noma sana. Pana vibaka waliokubuhu kwa wizi
 
Mi huwa natembea na bisbis...
Hiyo haisaidii. hata ukitembea na mguu wa kuku (bastola) watakuibia tu. Kumbuka silaha huwa inakuwa na msaada pale unapojua kuwa una adui anaye kufuatilia au anaye kuvamia. Lakini kama ni uvamizi wa ghafla au kuviziwa hata uwe na bastola umelala nayo watakuibia pamoja na bastola yako
 
Ulijisahau mno mkuu,anyway ndio mjini siku ingine utakuwa makini.
Next time mvizie mtu utue funzo hapo,niliwahi mvunja mtu mkono kama navunja muwa Sumbawanga.
 
daaah umenikumbusha mbali kweli nakumbuka kuna siku nipo kituoni mwenge nagombania gari za mbezi kimara kuna teja alitaka kuniiibia simu yangu nashukuru mungu siku hyo nilivaa zile suruali tight aka model basi katika kukurushani pale mlangoni teja akaingiza mkono wake mfukoni mwangu na kuishika simu hahaha mkono ukashindwa kutoka bwana nikamdaka hivo hivo mkono upp mfukoni kisha nikashuka naye unajua kilichotokea?? baadhi ya wenzie walijaribu kuja kuamlia walipoona mwili tu wakagwaya kumbe mwili wenyewe upepo tu sina hata zoezi hahahaha
 
Tanzania hatuna plans thats why kila kitu hovyo hovyo. Hebu fikiria mama mjauzito au mzee au mama mwenye mtoto mdogo eti naye agombanie daladala. Inasikitisha sana.
South Africa wao wanapanga foleni kuingia ktk daladala na hakuna konda kwa kila daladala zaidi ya dreva tu. Abilia wanakusanya nauli na kurudishiana chenchi wao kwa wao then wanampatia dreva nauli yake. Dreva anajua kwa trip moja ni sh.ngapi ukizingatia hakuna abiria anayesimama.
Tanzania ni kichwa cha mwemdawazimu, hata vitu vidogo tu tunavyoweza kufanya vinatushinda kabisaaaaa.
 
Back
Top Bottom