Duh,
Umenikumbusha waay back in the days.Enzi za dotcom bubble tunawezesha taifa kuingia mtandaoni.
Napanda basi Mwenge kwenda kazini Posta asubuhi, basi mminyo mminyo hivyo hivyo, kujistukia sina wallet.
Nikajisemea mwenyewe "I have never been pickpocketed in my life, and I ain't starting now".
Basi nikapiga mkwala basi zima likawa lina mtafaruku. Huku kichwani napiga mahesabu ya kukumbuka movements zote za kuingia kwenye basi, nikakumbuka kama kulikuwa na kimkono kimepita hivi. Lakini wakati wa kugombea kupanda basi mminyo mminyo you can't tell, unaweza kufikiri ni movement tu ya kugombea basi, kumbe watu wapo kazini.
Basi katika mtafaruku wa kuamua iweje, gari liende polisi au vipi, nikaona kuna watu wanaanza kushuka.
Ikawa kama inazidisha mtafaruku, this is a crime scene, mnaruhusu vipi watu waondoke?
Mahesabu yangu ya kijasisi yakaniambia nicheze na hawa wanaotoka. Nikataka kubanana nao, nikasema hatoki mtu gari linaenda polisi hili. Enzi hizo Kiranga Kiranga kweli huyu wa leo katulia kidogo.
Basi kuna kitu kikaniambia niangalie chini ya gari.
Kuangalia chini ya DCM, hamadi, wallet limelala limefuba vilevile.
Nikaingia chini sikuamini macho yangu.
Inaonekana kuna mjuba kati ya wale waliokuwa wanatoka aliinyai halafu mkwala wa kwenda polisi ulivyotanda akaamua kuiminya chini hapo kuondoa ushahidi.
Nikachukua wallet yangu nikapanda basi jingine.
Toka siku hiyo wallet inakaa kwenye deep pockets, kama nina overcoat kamwe haikai kwenye overcoat.