Najua Wajua na Kama Huyajui Basi Yajue!

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
KUNA kisa cha bwana aliyemwomba sana Mungu amsaidie. Siku moja akaambiwa; sala zako zimeshasikilizwa, isipokuwa, Mungu atakusaidia kwa sharti moja; Kwamba kile atakachokupa wewe, basi, jirani yako atampa mara mbili yake. Bwana yule akahitaji muda wa kwenda kutafakari kabla hajampa Mungu jibu. Akarudi na jibu; " E Mola wangu, naomba unipe chongo, utoboe jicho langu moja. Bwana yule alikuwa tayari awe na chongo ili jirani yake awe kipofu kabisa!

Ni katika mazingira haya, utamkuta mtu anamfanyia hila na hiyana Mtanzania mwenzake anayejitahidi kutafuta maendeleo yake kwa njia za halali tu, lakini, Mtanzania huyu mwenye roho mbaya atajitahidi kumvuta mwenzake asiende mbele kimaendeleo.Ukimwuliza; " Kwanini uchukie maendeleo ya mwenzako anayejitafutia kipato chake kwa njia ya halali? Atakujibu; " Mi namchukia tu huyu, akifanikiwa atajidai!

Anachoficha kusema ni ukweli kuwa anamchukia binadamu mwenzake kwa sababu ya ubinafsi na roho yake mbaya tu, kwamba hataki mandeleo ya mwenzake, basi. Na anachoshindwa kuelewa huyu anayechukia maendeleo ya mwezake ni ukweli kuwa maendeleo ya mtu huyo binafsi yatakuja kwa namna moja au nyingine kumnufaisha hata yeye. Kwanini uchukie maendeleo ya binadamu mwenzako yenye kutokana na bidii yake?

From : Kwanzajamii
 
BOflo ndugu yangu, siamini kama huyu mwenye kuandika hapa ni wewe! hata kama umekopi sehemu basi una upeo mzuri tu wa kujua vitu vyenye mantiki

wataalamu wa mambo wanasema jina la mtu nalo linakuwa na baraka zake na linaweza kumfanya mtu akawa wa tofauti kabisa, mfano SAUL SIO PAUL, ABRAM SIO IBRAHIMU, Na nadhani BWABWA SIO BOFLO, nahisi ukilibadilisha na hilo BOFLO KUWA ******, UTAKUWA NI MWINGINE KABISA
 
Utamwambiaje ame copy na hali ameshawakilisha? hahaha
 
Back
Top Bottom