Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 11,132
- 20,254
Kuna Baba Mmoja jirani yangu hapa juzi, katoka kwao Mbulu kwenye kilimo basi katika maongezi yanayohusu kilimo huko alikotoka Kuna jambo kidogo lilinishangaza sana na kufanya siku yangu yote kuharibika.
Ni hivi huyu bwana mara ya mwisho kutoka hapa kwenda huko kwao kwenye kilimo Kwa maelezo yake alikuwa na nauli ya kwenda TU na ilikuwa msimu wa kulima Sasa nikamuuliza, je vibarua hao wanaolima aliwalipa nini wakati alikuwa Hana pesa nyingine?
Alichonijibu ni hiki; kule kwao Yan sehemu kubwa ya maisha ya huko au utamaduni unaotumika kuwalipa vibarua ni kuwanunulia Gongo kwenye galoni ya Lita 5 au kitoto ndoo Cha Gongo kulingana na ukubwa wa shamba na wingi wa vibarua,
Huko shambani ambapo watafanya kazi kuanzia Asubuhi Hadi jioni Kwa ujira wa kunywa Gongo TU tena wakiwa huko huko shambani .
Hakuna malipo mengine wala chakula watakachopewa huko shambani au baada ya kumaliza kazi aidha ya kulima ,kupalilia au kuvuna. Na Maisha yanaendelea kama kawaida.
Je waungwana Kwa aina hii ya malipo je ni ubinadamu? Hata kama mtu atasema si wamekubali wenyewe je kiubinadamu ni sawa? Hata kama mtu ni maskini ndo umtese kiasi hicho jamani 🥲?