Naishi naye ndio, Lakini...


Samahani

Samahani

Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
67
Points
125
Samahani

Samahani

Member
Joined Oct 29, 2018
67 125
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
 
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
1,169
Points
2,000
Age
46
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2016
1,169 2,000
Siyo atakuja kupiga, atakuwa anapiga tayari ndo maana hatilii maanani mchumbake kuishi na mke.
Huyo mchumba wako aliyekusamehe atakuja kukupiga pigo moja takatifu hadi utatamani umrudie huyo mwanamke uliyezaa naye na unayetaka kumuacha akahangaike na damu yako
 
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
1,169
Points
2,000
Age
46
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2016
1,169 2,000
Tatizo ni hisia.. Hisia zangu haziko kwake hata kidogo. Awali nilidhani kuwa, baada ya muda huenda ningeweza kujifunza kumpenda, lakini naona hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku
Usikubali kuongozwa na hisia. Hali halisi ndo kiongozi sahihi.
 
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Messages
760
Points
1,000
Age
21
Kamwene

Kamwene

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2016
760 1,000
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Mchuma janga hula na wa kwao washirikishe wazazi pengine wanaweza kuwa na msaada mkubwa zaidi ila hapa sina hakika sana anyway hope everything is ginna be okay.
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
28,338
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
28,338 2,000
Hahaa Hii Topic pia " diva ameicopy na kuirusha kwenye kipindi chake .... Anacho nikera ni kwamba

Sijui kwanini huwa hasemi kwamba huwa anazitoa hizo story Jamii forum
 
Peramiho yetu

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2018
Messages
286
Points
500
Peramiho yetu

Peramiho yetu

JF-Expert Member
Joined May 25, 2018
286 500
Mkuu nam nimeshangaa labda mtoa mada ndio kacopy huku kama siyo nasi watoe credit
Hahaa Hii Topic pia " diva ameicopy na kuirusha kwenye kipindi chake .... Anacho nikera ni kwamba

Sijui kwanini huwa hasemi kwamba huwa anazitoa hizo story Jamii forum
 
Diana Spencer

Diana Spencer

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2018
Messages
316
Points
500
Diana Spencer

Diana Spencer

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2018
316 500
Pole mkuu. I feel your situation japo kuna sehemu umeamua kupindisha ukweli.
Naomba comment yangu iende kwa akina dada.. Acheni tabia ya kubeba ujauzito pasipo makubaliano. Kufanya ngono haimaanishi kuzaa.. Via vya uzazi vya binadamu vilipewa kazi nyingine ya kuuburudisha mwili.. Inachukiza sana watu mmekubaliana mnauburudisha mwili halafu baada ya week 3 mtu anakwambia nina mimba yako lkn SITOI. Utafikiri alikutegeshea. Baadaye huko mje muwasimulie watoto eti babako alikukataa.. Love and Affection kwa mtoto huanza kabla ya Mimba. Makubaliano wakati wa maandalizi ya kubeba ujauzito yanabeba maana halisi ya upendo wa baba na mama kwa mtoto. Mimba za kulazimishana bhana.
I once was in a similar situation.. inabore kinyama.
Ilikuwaje kwako?
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
28,338
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
28,338 2,000
Mkuu nam nimeshangaa labda mtoa mada ndio kacopy huku kama siyo nasi watoe credit
Hapana yeye ndiye huwa anaiba humu story zetu mwehu yule " hii sio 1st kufanya anavyo fanya ....


Imagine hii post inamuda gani tangu iwe posted humu -- na yeye kipindi ndio kwanza kimaanza now ....

Pia kuna thread nyingine pia kaiongelea katika kipindi chake kabla hajaiongelea thread hii alianza na hiyo

Thread yenyewe inasema ---JE ULISHAWAHI KUMPENDA MPENZI WA RAFIKI YAKO

nadhani uongozi wa jf ulipaswa kuwashtaki hawa " ....... kwa sababu wanatumia content za hii platform bila kutoa credit .... Yaani wao wanapata sifa huko mitaani kumbe wana desa tu habari zetu
 
J

Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2013
Messages
6,961
Points
2,000
J

Jamaa_Mbishi

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2013
6,961 2,000
Mkuu hapa huna jinsi tena, huyo mtoto anahitaji malezi yenu wote...oa tu kwani hata zamani wazee wetu walikuwa wanaoana kimazoea. Hampendani ila baada ya muda mnaanza kuzoeana na kupendana, mazoea yana taabu na raha yake pia.
 
Noel Ngiama Makanda

Noel Ngiama Makanda

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2018
Messages
523
Points
1,000
Noel Ngiama Makanda

Noel Ngiama Makanda

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2018
523 1,000
Sasa hizi ndio huwa zinaitwa story about love and not a love story .
Ukimwacha huyo mwanamke utakuwa umefanya ushezny wa kiwango cha lami, umemzalisha na kumpotezea miaka si chini ya minne!!!
Na vipi bado unamgegeda huyo dada ambaye humpendi?
 
dark angel

dark angel

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Messages
2,130
Points
2,000
dark angel

dark angel

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2015
2,130 2,000
Kama unampenda mtoto wako , oa mama yake.
Huyo mchumba wako unadhani amekusamehe ..ila anakuandalia kisasi. She will avenge ..haiwezekani akusamehe na bado unaendelea kuishi na huyo bibie.
Yani una mpenzi single mwisho wa siku anageuka single dad kabla hajakuoa.
No thank you.
 

Forum statistics

Threads 1,294,192
Members 497,843
Posts 31,167,683
Top