Naishi naye ndio, Lakini...


Samahani

Samahani

Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
67
Points
125
Samahani

Samahani

Member
Joined Oct 29, 2018
67 125
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
 
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
32,821
Points
2,000
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
32,821 2,000
Mchumba wako atakua wakwanza kuiona pepo. Yani umzalishe mtu (nitakuelewa) na bado uishi nae ndani chief??? Nisingekubali huo upuuzi labda kama na mimi nina mishe zangu na kwako kuna ninachofaidika nacho ila mapenziwise siwezi kubali huo upumbavu
 
Black Dove

Black Dove

Senior Member
Joined
Aug 24, 2016
Messages
129
Points
225
Age
26
Black Dove

Black Dove

Senior Member
Joined Aug 24, 2016
129 225
Muachie huyo mama na mtoto hiyo nyumba waishi, some part apangishe. Plus tuma mahitaji muhimu ya mtoto.
Then.... endelea na huyo ambaye uko na mpango nae!
 
Leonardchama7

Leonardchama7

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
1,275
Points
2,000
Leonardchama7

Leonardchama7

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2018
1,275 2,000
Mchumba wako atakua wakwanza kuiona pepo. Yani umzalishe mtu (nitakuelewa) na bado uishi nae ndani chief??? Nisingekubali huo upuuzi labda kama na mimi nina mishe zangu na kwako kuna ninachofaidika nacho ila mapenziwise siwezi kubali huo upumbavu
Mshauri wewe labda atakuelewa,,maana mm nimeshindwa hata kushangaa
 
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
4,855
Points
2,000
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
4,855 2,000
Mchumba wako atakua wakwanza kuiona pepo. Yani umzalishe mtu (nitakuelewa) na bado uishi nae ndani chief??? Nisingekubali huo upuuzi labda kama na mimi nina mishe zangu na kwako kuna ninachofaidika nacho ila mapenziwise siwezi kubali huo upumbavu
Hakika wanawake mmeumbwa tofauti, unajua mimi ukizalishwa tu wakati tupo kwenye mahusiano sikuelewi. Labda nkukute tayar una mtoto wako ila umezalishwa wakati upo nami?? Basi duh hapatoeleweka
 
jaywacnza

jaywacnza

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Messages
707
Points
500
jaywacnza

jaywacnza

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2012
707 500
Mnaomshauri kuwa amuoe mama mtoto wake mko sahihi na kwa wakati mmoja pia hamko sahihi kumbukeni huyu amesema pamoja na yote hana hisia naye sasa mwanaume kuishi na mwanamke asie na hisia nae kitakachofuata ni nini..?
.
Ila bado namshauri ajifunze kumpenda aliye zaa nae pengine ndie Mungu amempangia.
Nachoweza kumwambia huyu mtu, hisia nae anazo ila ana tamaa, anaonekana anapenda sana chini...anamlinganisha mke wake na wanawake wengine
 
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
32,821
Points
2,000
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
32,821 2,000
Hakika wanawake mmeumbwa tofauti, unajua mimi ukizalishwa tu wakati tupo kwenye mahusiano sikuelewi. Labda nkukute tayar una mtoto wako ila umezalishwa wakati upo nami?? Basi duh hapatoeleweka
Nitaelewa umbali ulichangia kupata tamaa ukanicheat yakatokea yaliyotokea. Sasa kuishi nae tena hapo siwezi kukuelewa kabisa.
 
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
4,855
Points
2,000
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
4,855 2,000
Nitaelewa umbali ulichangia kupata tamaa ukanicheat yakatokea yaliyotokea. Sasa kuishi nae tena hapo siwezi kukuelewa kabisa.
Sasa si ndio mbali huo huo unanifanya naishi nae, unadhani mimi kila siku ntananihii wali wakati wewe upo kagera huko??
 
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
32,821
Points
2,000
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
32,821 2,000
Mkuu hapa huna jinsi tena, huyo mtoto anahitaji malezi yenu wote...oa tu kwani hata zamani wazee wetu walikuwa wanaoana kimazoea. Hampendani ila baada ya muda mnaanza kuzoeana na kupendana, mazoea yana taabu na raha yake pia.
Hivi wanaume mnaweza kuishi na mwanamke usiempenda??
 
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Messages
32,821
Points
2,000
Mzigua90

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined Sep 23, 2014
32,821 2,000
Sasa si ndio mbali huo huo unanifanya naishi nae, unadhani mimi kila siku ntananihii wali wakati wewe upo kagera huko??
Kuishi nae na bado na mimi niwepo? Huyo dada lazima ana mambo yake huko alipo. Hamna mtu anaependa anaekubali kushare huba lake kirahisi hivyo
 

Forum statistics

Threads 1,294,198
Members 497,843
Posts 31,167,904
Top