Naishi naye ndio, Lakini...

Naishi naye ndio, Lakini...

Inategemeana na mazingira ama kuna kitu umelenga,ni ngumu mchumba wako utambue kuwa ana mwanamke mwingine tena anaishi naye na mtoto juu alafu eti umsamehe huku bado wanagegedana!!!hakuna kitu kama hicho,,lazima atakuwa ana target yake
Tukiachana, na huo ushauri...jina lako limenikumbusha mtu muhimu sana ambaye tulipotezana ghafla.
 
WAZEE wako wanasemaje
Nadhani ingawa wako katika kimya fulani hivi, lakini wao wanaangalia zaidi kile ambacho ntakiamua. Ingawa nakiri wazi, uwezo wa kutoa maamuzi katika hili unasaidia sana ushauri kutoka kwa wengi
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
waoe wote wawili mkuu
 
Kaa chini na wanawake wote wawili uwaeleze ukweli. Ukiwashirikisha wao utapata jibu la nini cha kufanya.

By the way muwe mnawaambiaga wanawake mapema kama ni take away/one night stand kuepusha madhara kama hayo. Starehe ya siku moja inaharibu mustakabali mzima wa maisha yako
 
Kama unampenda mtoto wako , oa mama yake.
Huyo mchumba wako unadhani amekusamehe ..ila anakuandalia kisasi. She will avenge ..haiwezekani akusamehe na bado unaendelea kuishi na huyo bibie.
Huyo atakuwa robot tu sio mwanamke kamili
 
Nawaonea huruma sana hao wana wake..haswaa huyo uliye mzalisha

Na jaribu kuvivaa viatu vyake ili niweze kuona kama nitaweza kuya pokea maumivu ya kuachwa " tena akiwa na mtoto ambaye amekuzalia" ...

Nacho baini nikwamba viatu vyake havinitoshi maana maumivu atakayo ya vuna sio ya mchezo mchezo ...

Samahani naomba nikuambie tu ukweli " wewe sio mwanaume sahihi wa hao wa-dada
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Achana na Mchumba wako Endeleza Maisha na huyu aliyekuzalia acha kuwa na Tamaaa
 
M naamin pia unaweza kujifunza kumpenda mtu as long as anatabia zinazoridhisha waswas wangu n kwa hyo unayedai n mchumba wako ukishamuoa ndo utamtambua vzur ogopa mtu anayebembelezea ndoa subir aipate sasa we s unaona et anampenda hyo dogo we subir ndoa ipatkane utajuta
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Mkuu nashindwa kukupata unaposema una malengo MAKUBWA na mchumba wako..... Lakini pia kama sikosei, sheria zetu zinamtambua mwanamke uliyeishi naye kwa muda huo kama mkeo halali, achilia mbali dini na pengine labda na kabila lako....! Lakini kwangu mimi nadhani yafaa sana kuishi na mwanamke ambaye unahisi amekupenda kuliko yule ambaye pengine unaona wewe umempenda...! Si ajabu tayari umeshaoa katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo ukimleta mwingine ni mjakazi tu...! Unautukuza sana msamaha wa mchumba wako, lakini sielewi ni wapi utaziweka na hizo laana unazotaka kujitengenezea...!

Mimi nakushauri kama hutaweza kuwaoa wote, basi fikiria namna ya kutulia hapohapo....!
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Sina cha kuongezea hapa.
 
Ila ngoja niongeze japo kidogo. Huyo unaemuita mchumba wako sio wako na moyo wake hauko kwako labda kama ana tatizo au ulemavu mwingine ambao anaona mwanaume mwingine hawezi kuukubali kama ulivyoukubali wewe ndo ataruhusu eti mchumba wake azae huko nje na mbaya zaidi wanaishi nae miaka mitatu ndani ya nyumba pika pakua na mnapeana unyumba?!!!! Kitu cha ajabu hiki jamani huyo mwanamke ana mwanaume mwingine sie wanawake tukipata mahusiano mapya tunaweza kukupa condom kabisa ukienda sfrn kujifanya tuna care au kukwambia jilinde tuu huko usiniletee maradhi kwa sbb tunajua kuna mwingine nampenda na anaprovide kila kitu. Ila mwanamke akikupenda hawezi ruhusu hilo sisi wanawake ni kazi kudivide love ukimpata new unasahau kabisaa wa zamani japo kama hajakuoa unakua unampa airtime kidogo kidogo huyu mwingine ili usikose pote ndoa hapo anakua ana target atakae oa wa kwanza obviously anajua huyu mpya ndo atakae muoa ndo maana kakuacha na huyo ulienae like seriously!!! Soo nachokwambiaa muoe huyo ulienae kaka angu maana utajuta badae ni bora huyo mama mtt anakupenda usije lazimisha unapopenda wewe ukalia kama spunch bob square pants machozi kama mvua sa elnino
 
Mnaomshauri kuwa amuoe mama mtoto wake mko sahihi na kwa wakati mmoja pia hamko sahihi kumbukeni huyu amesema pamoja na yote hana hisia naye sasa mwanaume kuishi na mwanamke asie na hisia nae kitakachofuata ni nini..?
.
Ila bado namshauri ajifunze kumpenda aliye zaa nae pengine ndie Mungu amempangia.
 
Mimi ninakushauri uliye naye ndiye mkeo. Ukimuacha utakuja kujuta. Ulikwisha fanya makosa. Just accept na kuendelea mbele.
Pia ukimwacha na huku ana mtoto na wewe, ukilinganisha pia na muda ambao umeishi naye, kisheria ni mke wako na anaweza kukupeleka mahakamani kwa kumpotezea muda wake.
 
Nimeshuhudia vifo vingi vikitokana na incidence kama hii, hasa kwa yule mwanamke unaempenda. Mwakajana mwishoni kuna jamaa alimpa mimba binti na wakati huo huo anamtu wake wanaependana. Sasa wazazi wakajua lazima amuoe, lakn jamaa akakataa na kuwaambia ana mtu wake mwingine na atailea tu mimba. Haikupita mwezi yule kipenzi chake tukamzikq kwa masikitiko makubwa. Na nimeona visa vingi sana kama hivyo vikileta matatizo kama vile
1. Ugumba
2. Vifo vya watoto
3. Mikosi ( baada ya kufanya kama unachotaka kufanya wengi wamenikuta hawawezi kudumi kwenye ndoa) .
Lakin mtoa mada unatakiwa uelewe kosa ulilofanya ni
Kuishi na mtu aliyekuzalia mtoto kwa zaidi ya miaka miwili huku mkishiriki tendo kama kawa, na jamii inashudia. Pia wazazi wa huyo binti wanajua binti yao kashaolewa na hata yeye mwenyewe anajua kashaolewa. Hivyo ukisema umuondoe utajiletea matatizo makubwa sana kwenye maisha yako, mkeo mtarajiwa pamoja na huyu mtoto uliye naye sasa hiv.
Chakukushauri ukifanye ni kumuoa huyo mwanamke unayeishi nae na kumueleza huyo kipenzi chako akubaliane na hali halisi, na uachane nae jumla. Na saiv unasema hauna hisia na huyu uliyenae, hii ni kwa sababu unamuwazia mtu mwingine. Lakin kama ukiachana na huyo kipenzi chako basi utampenda na utakuwa na hisia naye vizuri tu.
ONYO KWA VIJANA: unapoanzisha mahusiano ya temporarily, hakikisha unaisoma vizur akili ya unaye anzisha nae mahusiano na ukiona yeye yuko serious sana, achana naye mapema kabisa ili usimletee madhara yeye au mwanamke wako ambaye unamipango ne ya permanent. Kiukweli inaumiza sana
 
Pia ujue kwamba asilimia kubwa ya waliooa, hawajaoa wanawake wa ndoto zao au ambao walikuwa na makengo ya mda mrefu. Kwa hiyo usifikiri kwamba kumuacha huyo kipenzi chako utakua wakwanza
 
Back
Top Bottom