Naishi naye ndio, Lakini...


Samahani

Samahani

Member
Joined
Oct 29, 2018
Messages
67
Points
125
Samahani

Samahani

Member
Joined Oct 29, 2018
67 125
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
 
Dionize N

Dionize N

Verified Member
Joined
Oct 22, 2012
Messages
1,461
Points
2,000
Dionize N

Dionize N

Verified Member
Joined Oct 22, 2012
1,461 2,000
Sasa mzee baba miaka mitatu yote mnaishi pamoja hujawahi kuwa nae hisia tu? Mlikua mnaishi vipi sasa.

Basi mwambie tu ukweli kuwa humhitaji ila utakua na dhambi sana kwa kumtumia muda wote huo.

Effect yake kisheria. Hadi hapo mlipofikia sheria inawatambua kama mmeoana...soma kigungu cha 160(1) cha sheria ya ndoa ila unavyomuacha lazima umpe chochote kitu.

Ushauri wa maana kutoka kwangu wa kidini zaidi We OA bana
 
Thad

Thad

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2017
Messages
11,583
Points
2,000
Thad

Thad

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2017
11,583 2,000
Sasa mzee baba miaka mitatu yote mnaishi pamoja hujawahi kuwa nae hisia tu? Mlikua mnaishi vipi sasa.

Basi mwambie tu ukweli kuwa humhitaji ila utakua na dhambi sana kwa kumtumia muda wote huo.

Effect yake kisheria. Hadi hapo mlipofikia sheria inawatambua kama mmeoana...soma kigungu cha 160(1) cha sheria ya ndoa ila unavyomuacha lazima umpe chochote kitu.

Ushauri wa maana kutoka kwangu wa kidini zaidi We OA bana
Weekend hii na mimi nahamia kwako
 
colin_morgan

colin_morgan

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
1,813
Points
2,000
colin_morgan

colin_morgan

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
1,813 2,000
Daah , nikiona hizi nyuzi napata kiwewe ,

Aaargh nimechepuka na manzi flan bila kinga leo ananiambia ni mjamzito na ki ukwel ni genye tu zilinipeleka huko kwakua mke wngu hakuwepo ila naanza km kuhisi balaa linakuja hivi...
 
L

LadyRed

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2016
Messages
5,131
Points
2,000
L

LadyRed

JF-Expert Member
Joined Mar 19, 2016
5,131 2,000
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Kweli kabisa
 
1stMay

1stMay

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
577
Points
1,000
1stMay

1stMay

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2018
577 1,000
Ha ha ha,,wapi huko na lini?
yaani alipotea vuup... Huwa najiuliza hadi leo ni nini kilitokea. Afu hatukuwa hata wapenzi labda nimdange, nakumbuka text ya mwisho alinambia anaenda angalia mpira angenitafuta simuni akirudi, dah hakurudi. Nilimpigia simu, text ila waapi. Niliumia sana kumkosa, niliumia yaani vile kuwa na stress. Kibaya sikuwa namjua kivile ndo tulikuwa tunaanza juana. Sijui alikufa mpirani, labda siku moja atanitafuta.
 
Leonardchama7

Leonardchama7

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
1,300
Points
2,000
Leonardchama7

Leonardchama7

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2018
1,300 2,000
yaani alipotea vuup... Huwa najiuliza hadi leo ni nini kilitokea. Afu hatukuwa hata wapenzi labda nimdange, nakumbuka text ya mwisho alinambia anaenda angalia mpira angenitafuta simuni akirudi, dah hakurudi. Nilimpigia simu, text ila waapi. Niliumia sana kumkosa, niliumia yaani vile kuwa na stress. Kibaya sikuwa namjua kivile ndo tulikuwa tunaanza juana. Sijui alikufa mpirani, labda siku moja atanitafuta.
Pole sana,vipi bado unamtegemea kuwa siku moja atakutafuta?
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
5,904
Points
2,000
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
5,904 2,000
Cha kufanya
Mjengee nyumba ya vyumba vitatu tu huyo uliyezaa naye. Fully furnished.
Mwanzishie biashara ya kufanya huku ukiendelea kusupply chakula throughout.
Mwambie tu ulikuwa umeoa hivyo huna budi kufikia hayo maamuzi.!!

Oa huyo mke wako ambaye una malengo naye.(sijui Ni malengo gani huwa tunayo zaidi ya mbunye)
Muendelee kuishi na maisha yasonge mbele.

Uendelee kuhakikisha huyo mwenye mtoto hakosi mahitaji muhimu.
Ujiandae pia kupigwa pigo takatifu na huyo uliye na malengo naye.!!
Kuna uwezekano ukaishia kulea watoto wa wanaume wenzio wakati wa kwako umemtupa anateseka huko na mama yake.


In summary Ni kuwa wewe utakuwa mume wa wanawake wawili!!
Hata ukikataa, tayari umeshazaa na mtu. Ni mkeo tayari huyo. Hivyo utakuwa umeoa na kuacha.!!
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
24,658
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
24,658 2,000
Akili umepewa na kuzitumia umeshindwa baki na mama mtoto wako...

Huyo mwingine achana nae aende kwingine...


Cc: mahondaw
 
The real Daniel

The real Daniel

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2017
Messages
209
Points
250
Age
25
The real Daniel

The real Daniel

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2017
209 250
Naomba niwaulize mnaosema ampangishie nyumba au amjengee na kumfungulia biashara kisha aoe kipenzi chake na kumuacha huyu mama mtoto wake ; hivi huyo mwanamke anayeishi nae mnahisi anahitaji hela + nyumba au anahitaji penzi la jamaa?
Na je mnavyohisi jamaa akimpatia vitu hivyo, ataridhika kwamba jamaa aoe mke mwingine na wakati ashakaa nae for 3 years?
 
Selwa

Selwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Messages
441
Points
500
Selwa

Selwa

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2010
441 500
Wewe niamini mimi kakaangu, mwanamke ukishamfanyia ubaya temana nae tena usirudi nyuma, utakuwa umefungua mlango kwake wa kukufanyia lolote tena bila aibu maana wewe ndo ulianza kukosea tena atakufanyia vitimbi utahisi ni shetani, hawezi kukusamehe wakati bado unaishi na huyo binti eti anapenda mtoto wangu, ivi una akili timamu wewe? unajisikia?. usithubutu kuoa huyo mchumba wako.kubali kosa na haya ndio matunda ya makosa yako, oa huyo binit unae ishi nae anza familia. Na huyo binti umempotezea muda sana ukianza kumwacha sasa hizi na mtoto wewe kubali madhaifu anza maisha ya kifamilia. Sielewagi mtu unaishi na mtu miaka mitatu afu unasema hujawahi mpenda unaishi nae sababu ya mazingira magumu kwao, mazingira gani? ulishindwa kumpangia nyumba? acha kutafuta sababu kumrudia mpenzi wako wa zamani ukidhani kuna mapenzi hapo. Hamna na ukirudiana nae niamini mimi hadi sumu anakuwekea yani umezaa nje na unaishi na mwanamke mwingine afu unategemea anakuelewa???????????????????????????????????????????
 
Selwa

Selwa

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Messages
441
Points
500
Selwa

Selwa

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2010
441 500
huyu jamaa naona hajielewi.umekaaje na mtu miaka 3 huna malengo nae? me hata miezi 2 namsepesha
Hili ndio kosa ulilofanya just imagine mtu mnalala na kuamka kwa number of years then ghafla anakwambia hana malengo na wewe does it make sense?
 

Forum statistics

Threads 1,295,671
Members 498,336
Posts 31,219,247
Top