Naishi naye ndio, Lakini...

Naishi naye ndio, Lakini...

Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Pole mkuu. I feel your situation japo kuna sehemu umeamua kupindisha ukweli.
Naomba comment yangu iende kwa akina dada.. Acheni tabia ya kubeba ujauzito pasipo makubaliano. Kufanya ngono haimaanishi kuzaa.. Via vya uzazi vya binadamu vilipewa kazi nyingine ya kuuburudisha mwili.. Inachukiza sana watu mmekubaliana mnauburudisha mwili halafu baada ya week 3 mtu anakwambia nina mimba yako lkn SITOI. Utafikiri alikutegeshea. Baadaye huko mje muwasimulie watoto eti babako alikukataa.. Love and Affection kwa mtoto huanza kabla ya Mimba. Makubaliano wakati wa maandalizi ya kubeba ujauzito yanabeba maana halisi ya upendo wa baba na mama kwa mtoto. Mimba za kulazimishana bhana.
I once was in a similar situation.. inabore kinyama.
 
Kuna mmoja musoma nae alikuwa player sana, siku moja akaingia chaka km kawaida akapiga hlf akakimbia. Kilichomkuta asb alijikuta anakuwa na kasauti ka kike hlf jamaa alikuwa bonge la bwana. Kahangaika na ile sauti km miaka miwili, siku alivyopona alifunga na ndoa na akaacha hiyo tabia.
Ha ha haaaaa
Mbavu zangu jaman
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Umemaliza yote niliyotaka kusema...
Mkuu huyu uliyenae kitanda kimoja na kwichikwichi deile ndio mkeo huyu hata sheria ya selikari inamtambua maana mmeishi kwa miaka mitatu na mtoto juu, anyway....huyo mchumba wako yy bado anakusubiliaga tu mpamge malengo mpaka leo?? Nakushauri anza kumpenda mkeo na hiyo mipango kabambe panga na mkeo na mtafanikiwa, kikubwa kwa sasa fanya mipango ya kubariki ndoa yako na uifanye iwe rasmi...
 
Ila wanaume mna roho ngumu sana,mna maamuzi chenga sana yaani,na ubinafsi umejaa ona una jali tu furaha yako ya huyo uliyemzalisha wala hujali.
 
Ila wanaume mna roho ngumu sana,mna maamuzi chenga sana yaani,na ubinafsi umejaa ona una jali tu furaha yako ya huyo uliyemzalisha wala hujali.
Ukisema wanaume tu ndo tuna roho ngumu unakua mbinafsi pia haya mambo sasa hivi si ya upande mmoja japo linapotokea anayeonekana anaonewa ni mwanamke.

Kiukweli jamaa yuko wazi hampendi huyo mama ilitokea tu mimba bahati mbaya sasa katika hali kama hiyo ukioana na mtu ambaye hayuko moyoni mwako utamtesa bure ni bora kuishi bila ndoa kuliko kuishi kwenye ndoa yenye matatizo.
 
Una undugu na uyo mchumba anayependwa au ndo wewe???
Unataka kunambia kuwa ushauri wako Ndio wa mwisho, tusimshauri, au huyo dada amekosea kumsamehe jamaa hivo hafai kuwa mke
 
Jamaa ataumia tu kwa maamuzi yoyote atakayeyachukua maana kawapotezea muda wote 2
Mimi pia ni muumini wa hicho ulicho-comment.

Tatizo huyu mtoa mada kakaa na mtoto wa watu miaka minne (jumlisha na kulea mimba) wakipika na kupakua. Ingekuwa ni kipindi kifupi kidogo ingeleta mantiki.
 
Fikiri mara 2 mkuu, Kuna uwezekano mkubwa wa kumuumiza huyo dada, kama hujawahi ona au kusikia sawa, halafu kwa nini mnamuhukumu huyo future wife wake amekosea wapi? Kusamehe au nini, na kwa nini mnamtabiria mabaya? Kwani huyo anayeishi naye hawezi badilika akiamua? Nafikiri uamuzi ni wa kwake maana kayakoroga mwenyewe
Sasa mkuu angejua kama huyo mwingne ni wa muhimu asingemwagia ndanii...!! Kwanza huyo mwingine anamchoraa tuu...Kuna siku ataujua ukweli kuhusu huyo anaedai ana future naee hakika atarudi hapa kushuhudiaa... Hakuna mwanamke utamsaliti na kumpa mimba mwanamke mwingine alafu akakusamehe kizembe hivyooo Trust me Hayupooo tena mpo mbaliii aisee huko ukute ashaanza maisha yake na jamaa anamlaaa na wana future yaooo Wanawake usicheze nao mkuuu
 
Huyo huyo jenga nae hayo malengo makubwa mkuu

Wahenga waliposema mpende akupendae hawakukosea kabisa

La sivyo utakuja kujuta
 
Back
Top Bottom