Naishi naye ndio, Lakini...

Naishi naye ndio, Lakini...

na uhakika akiwambia wote watakubali ila kila mtu atasema Mwache fulani uwe namimi..zoezi litabaki pale pale kuwa gumu.
Ni gumu . Lakin ndo ukweli mzuri kuwa hauwezi kuacha bora wakubali wote wapeane ratiba kwa week. Mbona wanaooa wake wawili au watatu wanaweza
 
Wakati fulani ukweli ni dawa hata kwa magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu
 
Haiingii akilini eti mwanamke huna hisia nae halafu unalala na kuamka nae 4 good years na mtoto juu tena unagegeda kila siku
Ndugu, hebu pitia Uzi huu, huenda ukajiongezea kitu fulani muhimu sana kwenye Hilo...

Samahani lakn,Hivi ulimuoa nani sasa Kati yule wa malengo au yule mwenye kiumbe chako...Kuna Jambo la kujifunza hapa
Mmmh.... Hili jambo halijawahi kuwa rahisi.. wote ni wazazi anyway, na wanafahamiana na imebidi tu maisha yaendelee kwa "mfumo usio rasmi" machoni pa wengi...
 
Dah...Ila Kuna mmoja anakufaidi kuliko mwingine..hasa unaeishi nae...anyway kazi iendelee
 
Ndio scenarios za maisha zinavyoamua wakati fulani kutulazimisha kuishi maisha yetu tofauti kidogo na mitazamo ya wengine na wakati fulani pia, tofauti na vile tunavyopanga... Maisha ni fumbo linalohitaji macho ya ziada kuling'amua
 
Hakika umenena vyema,haya Maisha haya hayatabiriki hata kidogo.
Ndio scenarios za maisha zinavyoamua wakati fulani kutulazimisha kuishi maisha yetu tofauti kidogo na mitazamo ya wengine na wakati fulani pia, tofauti na vile tunavyopanga... Maisha ni fumbo linalohitaji macho ya ziada kuling'amua
 
Owa huyo mwenye mtoto mara nyingi huwa hatuowi au kuolewa na wale wenye malengo nasi. Uliza wazazi wako na ndugu watakwambia unapanga panga weee MUNGU.
 
Na hapa wengi sana wameshaumia... Kung'ang'ania kuolewa au kuoa mtu ambaye umezaa nae ni hatari mno kwa afya ya ndoa...
 
Yule hujaishi nae humjui kuwa wapenzi na unaeishi nae ni tofauti. Songesha maisha ukienda kule utaona utofauti utamkumbuka huyo mama mtoto shauri yako.
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Huyu anongozwa ns hisia sio akili, huyo mwanamke anayempenda yeye yuko kwake kwa maslai fulani ila jamaa hajui mkuu akubali tu alifanya kosa na aweke mambo sawa aoe huyo baby mama walee yu watoto
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Mkuu kwenye maisha huwa tunakosea, na kosa kubwa sana kwa sisi wanaume ni kama ilivyotokea kwako. Ulitakiwa kutelekeza mama na mtoto ( uamzi huu siupendi na nibaya sana) kwa hapo ulipofikia ni point of no return ushakaa na mtoto wa watu more than 4yrs
1. Umempotezea sana muda
2. Utamwathiri kisaikolojia mwanao na mama yake pia endapo utaachana na mzazi mwenzako
3. Huyo dada anaweza kukudhuru kwa sababu umeshamharibia maisha yake wanaume wengi hatupendi kuoa mwanamke mwenye mtotot
Cha kufanya sasa
Endelea kyishi naye kama mkeo ila endapo utapenda basi waoe wote 2 huyu mkubwa yule mdogo ili mtunze mtoto wwnu pamoja
Hii kitu ilinipata exactly kama wewe, ndie mke wangu niko naye hadi sasa mwaka wa 13 sasa
 
Kosa la kifundi ni wewe kuruhusu kuzaa na mtu ambaye huna mpango nae, na mbali ya hapo kukaa nae kama mke. Chakushangaza zaidi mpaka leo uko nae na unaendelea kumla eti unajizuia kuzaa nae, wakati huo huo unasema una mwanamke eti mna mipango mikubwa.
Nakushauri kama umeweza kuishi nae huyu miaka yote hii na umejiridhisha anakupenda, huyu ndio mkeo, huyo mbaye inaonekana wewe unampenda , yeye hakupendi mpaka kukuruhusu uishi na mke mwingine akijua kabisa mnakutana kimwili, ana malengo tu fulani na wewe.
Oa huyu mzazi mwenzako akupendaye.
Wise advise!!
 
Ila wanaume bana, kweli mnadhani akili za wanawake ni hamnazo kiasi hicho. Tulia utunze familia yako vinginevo yowe la dunia linakuhusu
 
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Huyo unayeishi naye ni mke wako tayari anaitwa "Common Law Wife".

Ukutaka kumuacha bila utaratibu hata mahakamani anatambulika kama mke wako hivyo.
 
Back
Top Bottom