Naishi naye ndio, Lakini...

Samahani

Member
Oct 29, 2018
68
125
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
 
jaywacnza

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
890
1,000
Unaishi nae miaka miatu, unafanya nae mapenzi marakwa mara sio haki. Usingekubali kuishi nae nngekushaur uachane nae, ila umeishi nae miaka mitatu na unamlala daily af unasema huna hisia nae....tena mnatumia hadi njia za uzaz wa mpango ahahaa noma sana......

We cha msingi usifate ushauri wa mtu yoyote, ishi kama unavyoishi muda utaamua wenyewe, we ishi tu mambo yatajiset yenyewe badae
 
xaracter

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,027
2,000
Ukitaka kufanya kosa utakalolijutia maisha yako yote achana na huyo mwanamke aliyekuzalia mtoto oa huyo mchumba wako.
 
mabutu1838

Member
Feb 20, 2019
71
125
Naomba nikuulize "samahani", na ninaomba jibu la kweli kabisa pasipo kificho; JE UNAMPENDA HUYO ULIYEZAA NAE? JE UNAISHI NAYE KWA SABABU YA HURUMA? JE HUYO MCHUMBA DEMU WAKO WA NJE ANAFANYA SHUGHULI GANI? JE TANGU UANZISHE UHUSIANO NA HUYO ULIYENAYE NDANI, UMESHAWAHI KUMTAFUNA HUYO DEMU UNAYEDAI UTAMUOA? JE HUYO ALIYE NDAN NI KABILA GANI NA JE ALIYE NJE NI KABILA GANI? Kama utashindwa kunijibu hapa njoo inbox. Ahsante
 
max 20

Member
Jan 18, 2019
10
45
Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia.

Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile.

Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu.

Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami.

Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo.

Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro.

Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini.

Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu.

Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.

Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana.

Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo.

Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
Jitahidi kuwa muungwana bro,ninachokiona hapo huyu uliyezaa naye ndo mke maana mmeishi walau kwa miaka mitatu.Huyo ambaye unasema una malengo naye nakwambia utarudi tena hapa kuomba ushauri.Anajifanya kukusamehe na kumpenda mwanao kwa sabb tu hujamweka ndani,siku ukimweka ndani utajuta,ipo siku hautaamini macho na masikio yako.Lkn pia naona unataka kufupisha tu maisha yako,huyo uliyezaa naye mnaishi mtaa mmoja au eneo moja ni maumivu gan atayapata ukimwambia et una mchumba mwingine wa kuoa na yeye yupo tu kupoteza muda.Jitafakali bro,unaweza kufurahi leo lkn ukalia soon.
 
Bulaya001

JF-Expert Member
Dec 21, 2018
5,042
2,000
Malengo yazidi umuhimu wa mwanao, hivi unajua wanawake wanavyowatesa watoto wa kutowazaa japo saizi anajifanya kondoo? achana na malengo pambania huyo ulienae sasa..
 
Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,311
2,000
Nadhani umejibiwa vyema...fuata sana ushauri wa page ya kwanza. Kila la kheri.
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,335
2,000
Usiishi na mwanamke usiyempenda eti kisa umezaa naye, Mwandalie Mazingira mazuri mama na mwanao halafu muoe haraka mwanamke wa ndoto zako ili uishi kwa furaha, Usitishwe na maneno hakuna revenge wala kisasi
Amewezaje kuishi na mwanamke asiyempenda kwa miaka mitatu?
 
muluvigwa

JF-Expert Member
Jul 15, 2012
252
225
Kuna wakati Mungu anakuletea kitu ambacho wew hukuwahi kufikiri yn unaweza ukachukia jambo lkn hill jambo likawa na heri na wew pia unaweza ukapenda jambo lkn hilo jambo likawa na Shari na wew ...oa mama mtoto wako mchumba atampata mwenzake Hugo mchumba anakulia timing uingie ktk 18 zake akulipizie
 
Top Bottom