HAUJATOFAUTIANA SANA NAMIMI MKUU,SOMA YANGU KISHA MWISHO CONCLUDE KAMA MIMI
Nilikuaga sina mpenzi kabisa Tangu niamue kuanza maisha,nilijua kujiiingiza ktk mahusiano ntapotea haraka so nikaamua kuwa busy na maisha yangu na mihangaiko..lakini katika pitapita za hapa na pale siku moja nikakutana na rafiki yangu school mate tuliosomaga nae shule zamani kidogo,Alikua ni mdada(jina lake ni RODA) tulipokuaga shule nilikua natoka na Pacha ake maana wako mapacha so tulikua tunaitanaga SHEMEJII...
basi siku hiyo aliponiona namimi kumuona tu akaniita Shemejiiiii namimi kumuangalia sura kama inakuja basi akanambia mimi Flani baada ya kuntambulisha nilimkumbatia kwa furaha sana...siku hiyo tukakaa mahali tukapiga story nikamuuliza huku unafanya nini akanambia nipo Chuo,na mimi nkamwambia nipo tu nahangaika na maisha Basi tulipiga story baadae tukaachiana namba tukaachana kila mtu akaendelea na ratiba zake.
Maisha yangu yaliendelea kama kawaida,sinaga mpenzi mimi wala sikua na time na huo muda maana hata kazi nlizokua nafanya hamna mdada nitaemtongoza akanikubali zaidi ya kunidharau so nikawaga zangu nimepata rafiki hata wa kuchati HATA kwenye simu..RODA akawa rafiki angu tukawa tunawasiliana na kwa mara ya kwanza nikapata rafiki wa kwenda hata mtembelea,alikuaga anakaa Hostel.
Nikawa naenda mara kadhaaa,tukazoeana sana na Roda majina yetu ni yale yale yakuitana Shemeji shemejii,na tulikua tukimaanisha na tuliheshimiana ipasavyo...kama kawaida hamna kazi unayofanya ukakosa majanga,siku moja nikiwa kazini kuna mtu alinitibua,nilikasirika nikainua Chupa piga Kichwani Mtu akalala chaliiiii...watu wakaja nikabebwa Juu Juu hadi polisi niliyempiga kakimbizwa Hospitali.
Kumbuka tangu mwanzo sinaga rafiki nashukuru Mungu nilikutanaga na RODA,basi baada ya lile janga nikapelekwa kituoni nikiwa njiani nikampigia RODA nikampa taarifa,basi nikapelekwa ndani nikatulia..kesi ikaenda nikiwa pale pale lock up mapolisi thamana hawataki kunipa maana wanadai hali ya mgonjwa bado mbaya so nisubiri...mahakamani hawataki nipeleka basi kituoni pakageuka GETO nikawa naletewa chakula na Roda asubuhi mchana jioni.
Baadae lile sooo RODA alilimaliza kwa gharama zaidi ya 500,000 nikatoka,maisha yakaendelea nikamshukuru roda maisha yakaendelea...kazi kama kawaida Roda akawa msaada mkubwa sana maisha ni mwangu,ki ufupi alifanya MENGI ambayo siwezi maliza yasimulia hapa.
Siku moja nikiwa zangu nyumbani nikawa nawaza na kujiuliza hivi kwanini RODA ananisaidia hivi namimi sio mpenzi wake?? yani urafiki tu ananisaidia hivi? anakuja home ananisaidia kufanya usafi,kufua,nk nikipata majanga ana clear yani ni mwanamke asiekubali kuona baya linatokea kwangu ingali yeye yupo na anashuhudia.
Nikasema Huyu anafaa kabisa kuwa mpenzi wangu,acha nifanye mpango nimwambie ukweli kuwa namuhitaji awe mpenzi wangu kabisa,RODA ni mwanamke aliyeokoka namfahamu tangu Secondary mwana UKWATA mwenzangu,walikuaga ni hatari kwa maombi sasa nilivyokumbuka hilo nikaona yes Huyu huyu ananifaaaa.
Siku ikafika nikamwita roda nikamweleza haja na nia yangu ya kuwa nae..ki ukweli Alinitolea nnje,sikutaka muudhi wala mkera nikakubaliana nae ila nikatulia siku nyingine tena tena..sikuchoka msumbua na kumuomba kwa Machozi tena,basi siku moja akaniita akanambia SAM njooo,siku hiyo nilitoroka kazini nikaenda kufika Akanambia NIMEKUKUBALIA lile swala lako lakini soma hiki cheti kwanza.
Akanipa cheti ambacho nakumbuka tulipewaga zamani tukiwa FORM TWO kinachohusu SEX engagements..NI kiapo walikula wakaekewa maombi kabisa kwamba THEY WILL NOT ENGAGE THEMSELVES INTO ANY SEXUAL INTERCOURSE UNTILL MARRIAGE...basi niliona nikamuuliza unamaanisha nini?? akanambia SAM nakua na wewe ila SEX NO mpk tutakapo oana,namimi ki ukweli kutoka moyoni sikumuhitaji roda kwa ajili ya SEX nilimpenda kwa anavyojitoa ktk maisha yangu so SEX haikua ishu kbsa kwangu so NIKAMKUBALIA na nikamuahidi.
Tukawa rasmi wapenzi ambao hatu sex..akawa kila weekend akiwa hana vipind anatoka hostel anakuja kwangu analala hadi j3 ila NO SEX mzeee ni kulala kama dada na kaka ila ni wapenzi though romance zilikuepo...basi maisha yakaendelea na nikawa mwaminifu kweli,tutaenda kuoga wote tutafanya kila kitu ila siwezi hata mtamani,ikafika kipindi hata sikua na hamu hata na hyo romance.
Maisha yakasonga ila namimi nikawa na mchepuko wangu nnje(ambae ndio mama watoto wangu wa sasa),ukawa unanipoza kila ukitaka kuja kwangu naupiga calender maana sikua nataka apafahamu asije akaja siku mimi niko na roda..so maisha yakaendelea na kwakua nae alinipenda alikua haoni shida lipia Hotel tulale then kesho yake nirudi home bhasi maisha yakaenda hivyo.
Baadae Roda alimaliza chuo akawa anatafuta kazi so akaja kuishi HOME kbsaaa..huku namimi nikiendelea kukipiga na mama watoto..siku moja mimi nikajitoa ufahamu Nikasema hapa lazima niseme ukweli Nikamwambia mama watoto watoto wangu bwana eeeh mimi naishi na mtu..kuna moja mbili tatu na nne HATUSEX so namimi nimeshindwa kukaa muda wote huo ndio kuja kukupata wewe.
Ki ukweli wife hakuniamini hata kidogo eti nalala na mwanamke halafu si do nae,basi akanambia nimthibitishie nikafanya kila alichotaka na hatimae akaja akaamini,ishu ikaja WIFE anataka niachane na RODA nimwambie asepe kwao ili tuishi na yeye,hapo kwangu pakawa pagumu vibaya mno sasa namuachaje RODA kwa yote alonifanyia namuachaje yani namfukuzaje?
Bwna wakati nikiwa nawaza hayo kumbe roda Alishanishtukia siku mingiiiiii Kua nina mchepuko akawa anauchunaga tuu anasubiria kuona mwisho wake....kabla hata mimi kumuanza siku moja roda akanambia wakat natoka kwenda kazini SAM msalimie MAGE (ndio wife sasa) daaah moyo ulipasuka PAAAH
Nikasepa kazini ila hiyo siku nzima nilihisi kama roda ananitokea yani nilikua natamani kufa,kila kitu sikioni vizuri,masaa yanaenda nikifkiria kurudi HOME ndio nahisi kama naenda kuchomwa kisu na roda leo nikiwa usingizini,bwana niliwehuka.
Ndugu yangu nilichofanya nilimrudia mchepuko (wife) nikamwambia bwana Mimi kumwambia RODA tuachane nimeshindwa,wewe si unataka kukaa na mimi na unanipenda,basi yale yote alionitendea roda tumlipe kwa kumuachia vitu vyote ndani ya ile nyumba..sisis twende tukapange..THANK GOD nikaeleweka...nikarudi home kwa mara yya mwisho nikawa namuangalia RODA uchungu unanijia sema ndo ntafanyaje sasa.
Nikaandika barua then siku naondoka nikaificha kabatini,nikasepa zangu sikuchukua hata kitu kimoja..nikamtext roda aende kabatini sehemu flani kuna ujumbe wake Akaenda akauona...ila HAKUKUBALI,alinambia SAM wewe ni wangu NITAKUPATA TU.
Maisha na mchepuko (wife) yakaendelea... Story ya Roda ni refu kidogo.
Ila point yangu MKUU fanya kama nilivyofanya mimi ila kwakua una mtoto sikushauri uandike barua we fanya kama Unasafiri then kaanze maisha upya mahali na huyo mchumba ako,najua unaweza tishwa kua huyo mchumba ako anakuandalia revenge ila HAPANA kuna wanawake wakisema I LOVE YOU they mean it brother....nenda kwa mchumba ako ila huku ulikozaaa usichukue hata nguo zako mwachie ili ajue bado upo nae yani hata boxa usichukue...GO START YOUR NEW LIFE if you realy care about your baby mama and kid.
Usithubutu kumwambia acha kichwa yake imwambie kua umechwa ila usimwambie,atakapokuja GUndua Utamwambia ukweli..ila jitahidi uende ishi mahali ambapo hatajua hata uko wapi but HUDUMIA MWANAO,wapigie simu..AHADI kibao Wajali kama mwanamke hana kazi msaidie hadi uhakikishe anasimama wima kiasi cha kumuhudumia mwanao bila tatizo...Muda wote huo yuko mbali na wewe Atatongozwa TU na atapata mtu moyo utaomuelewa we muache Hiyo ndio pona yako.
Akija gundua badae una mke haitouma kivileeeeee maana tyr alishazoea maisha ya bila wewe,usimpigie simu ovyo...Hudumia vizuri ila jitoe kwenye akili yake kwa akili as a REAL man UNAE mjali yeye na mwanao.
Umepata kitu MKUU najua.