Naishi naye ndio, Lakini...

Achana na fikra zako potofu za malengo makubwa na mchumba wako na kwamba huyo unayeishi naye huna hisia naye wakati ulimvua picchu huku umesimamisha na ukamgegeda. Muoe huyo mrembo bila kuchelewa. Malengo makubwa sasa yahamie kwa mama na binti yake.

Habari wana jamvi...

Natamani sana kupata msaada, uwe wa kimawazo, kisheria ama hata kiuzoefu tu katika hili ninalolipitia. Miaka mitatu iliyopita, nilikutana na mwanamke fulani ghafla tu, [ingawa badae niligundua kuwa tulikuwa tukiishi mtaa mmoja] na pasipo hata makubaliano yoyote ya kimaisha, tulikubaliana kulala pamoja siku ile. Nakiri wazi kuwa, nilikuwa nimepata kinywaji kidogo, hivyo sikuwa na uwezo wa kuamua ni nini kilikuwa sahihi kwa wakati ule. Siku iliyofuatia, niliondoka mapema na kuelekea kazini nikiamini kuwa naye angejiandaa upesi na kurudi nyumbani kwao. Wakati huu akawa amenieleza kuwa, palikuwa ni pale pale mtaani.

Ajabu ni kuwa, jioni ya siku hiyo nilimkuta akiwa bado nyumbani kwangu na alikuwa amenisaidia kufanya kazi nyingi ambazo sikuwa nimezifanya kwa muda mrefu. Nyumba ilikuwa na mwonekano wa tofauti kidogo. Hasira ikayeyuka na kwa mara nyingine akalala nami. Siku ya tatu akaridhia kurudi kwao, lakini mazoea ya kuja kwangu mara kwa mara hayakuisha.

Baada ya kipindi fulani, nilihisi kuwa alikuwa mjamzito na nilipomuuliza, alikiri na kuniambia wazi kuwa, alikuwa anaogopa sana kuniambia kuhusu hilo. Najua mtashangaa kidogo, lakini mwanamke huyu hatukuwa na mazoea ya kuongea mara kwa mara, hata tukiwa nyumbani. Kitabia, yeye ni mkimya kupitiliza nami ni muongeaji, hivyo hili halikuwa gumu kwetu.

Mimba ililelewa yeye akiwa kwao, lakini kutokana na ugumu wa mazingira ya pale kwao, tulikubaliana kuwa wakati wa kujifungua aende akajifungulie kwa dada yangu anayeishi Morogoro. Alijifungua mtoto wa kike ambaye hakuna shaka yoyote kuwa, ni wangu!! Tumefanana zaidi ya ninavyoweza kuelezea, na hili linathibitika zaidi kadiri alivyoendelea kukua.

Baada ya kula uzazi kwa miezi sita, alirudi nyumbani, na ile hofu yangu juu ya mazingira ya kwao [sina haja ya kuuelezea sana ugumu wake], nikapata wazo la kumwacha aishi pale nyumbani kwangu mpaka walau mtoto akue ndipo nijue nafanya nini. Sikuwahi kumwambia kuwa nna mchumba ambaye tuna malengo makubwa, lakini mchumba wangu yule nilimweleza kila kitu na amenisamehe na tunaendelea na mipango yetu, tena anajua wazi kuwa naishi na mwanamke huyu. Nadhani, huenda ananipa nafasi ya kufanya maamuzi magumu. Kiajabu, yeye pia anampenda sana mtoto na amekuwa akimtumia zawadi mara kwa mara.

Sasa ninaishi naye ndani kama SURIA, yani mtu ambaye sina ndoa naye.. Mtoto ana miaka mitatu sasa, na ninampenda sana mwanangu. Nieleweni nisemapo kuwa, sikuwahi kuwa na hisia na mwanamke huyu, ingawa yeye anaonekana wazi kuwa ananipenda sana. Jitihada zote zimefanyika ili kuhakikisha kuwa hatupati tena mtoto mwingine, lakini bado nashindwa kujua kuwa, nawezaje sasa kumweleza kuwa, inabidi aendelee na maisha yake na mimi pia nifanye hivyo. Namtazama mtoto wangu, namwonea yeye pia kama mama wa mtoto huruma, lakini nna malengo yangu makubwa SANA na mchumba wangu ambaye pamoja na makosa makubwa niliyotenda, ameamua kunisamehe na kuwa mtu wa karibu mno kwangu.

Tafadhali wajuzi wa mambo, naombeni sana msaada wa mawazo yenu...
 
Me makushauri mtie kwanza mimba huyo.mvhumba mwengine ile kwanza ujiwekee uwakika kama hyo mwengine ukishamtia mimba ndo anza kufanya nae mipango ya kukaa nae la sivyo nae atakufanyia kitu hutokuja kuamini kama yeye kakufanyia hivyo
Duh!!! Mpaka mwili umenisisimka...
 
Kikubwa tia mimba nahuyo mwengine me mwenyewe na mkasa kama wako kuna mtu nimezaa nae lakini linapokuja swala la upendo kwake alipo kabisa nimejitahidi mpaka basi yani ila ushauri wangu huyo unaempenda akikisha unatia mimba kwanza kujiwekea uwakika
Kuna jambo la kujifunza kwakweli...
 
Mkuu... Huyu ambaye ndiye yuko kwenye plan alivunjika sana moyo pindi alipoujua ukweli. Sikujua kuwa angeweza kunielewa. Lakini amekuwa nami katika kipindi chote. Yeye pia, baada ya kumweleza mazingira ambapo mtoto anaweza kukulia kama nikiachana na mama yake, amekuwa msikivu na mpango uliokuwa awali ukarudi upya.. Hakika sio rahohisi kulielezea hili...
Mkuu hakuna mwanamke anayeweza kukusamehe huku bado unaishi na huyo mwanamke,kuna kitu karenga juu yako na baada ya hapo unaweza kujuta maisha yako yote,fanya ufanyavyo kama ulie zaa nae hana shida usimuache,habari za hisia zitarejea tu ondoa shaka
 
Kama uliezaa naye hana shida zaidi ya kutokuwa na hisia naye, nakushauri usimuache na ogopa sana mwanamke mkimya,usifikiri hana mdomo mpe heshima yake,fanya yako na huyo mchumba wako japo naamini mwisho wake ni mbaya zaidi hasa utakapojichanganya ukamuacha mzazi mwenzio,na kama ni hisia kapige pombe zako lazima hisia zitasoma tu,kama zilivyosoma hapo mwanzo
 
Usiishi na mwanamke usiyempenda eti kisa umezaa naye, Mwandalie Mazingira mazuri mama na mwanao halafu muoe haraka mwanamke wa ndoto zako ili uishi kwa furaha, Usitishwe na maneno hakuna revenge wala kisasi
 
Kusamehe kunawezekana hasa kwa mtu unayempenda, mchumbako kakusamehe kweli, tena kumbuka amekuvumilia na kukusubiri kwa muda mrefu, fanya umuoe Mwanamke uliyemwahidi kumuoa, uliyezaa naye mwandalie Mazingira mazuri ya maisha
 
Mkuu umenichekesha sana unavyong'ang'ana kwamba una malengo makubwa wakati mimi sioni kama una lengo lolote kubwa 😀
Wewe bwana hapo ndio umeshaoa cha maana we endelea kujenga maisha na mkeo na mtoto wenu. Sio kila ndoa ina matarumbeta mkuu. Miaka minne yote mi nafikiri huyo ulie nae ndani ndio mkeo. Hizo nyingine ni ndoto tuu kama mimi navyoota kujenda ghorofa
Kuna jambo la kujifunza kwakweli...
 
Hayo malengo makubwa saaana na huyo unayemuita mchumba wako wa zamani ni yapi??
Kununua ndege?kununua treni ya mizigo?au kugombea urais yeye awe first lady??
Huyo uliyezaa nae hana nini?
Wewe jamaa ni fala tu kama mafala wengine,kuna jamaa kakuuliza humu,wazee wako wanasemaje kuhusu hilo??
Kumbuka upendo kwa mtoto ni kitu kizuri sana,na hivyo wewe unavyompenda mwanao na ndivyo mwanao anavyokupenda wewe pamoja na mama yake,kumuacha huyo mama yake ni kumuumiza kwa kiwango ambacho hakielezeki huyo mtoto japo hawezi kueleza ni jinsi gani anaumia.
Brother,kama uliyoisema siyo movie,endelea na maisha na huyo mwanamke uliyezaa nae,epuka kutengeneza matarajio feki na hewa
Hahahahahahahah jamani..... Nimecheka sana kwakweli hayo malengo amshirikishe baby mama wake wayafanye aache porojo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom