Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

MREJESHO BAADA YA MIEZI MITATU.

Leo tarehe 1 April ni miezi mitatu imepita tangu nimeanza mradi huu. Na huu ni mrejesho kwa vijana wenzangu ili watakapoanza wajue muongozo sahihi.

Nilifanikiwa kununua kuku wengine wakafika jumla 60. Lakini wakapungua
Mpaka Sasa wamebaki 50. Mpaka Sasa nimezika kuku watano wawili kwa ajili ya ugonjwa na watatu walikua wadhaifu wameuliwa na majogoo wakati wanawapanda Mara kwa Mara.

Kuachana na vifo mradi unaenda vizuri, japo mafua na kuharisha ilikua ndio changamoto kubwa lakini kwa Sasa nimeweza kuidhibiti.

Kuku wamekua wakubwa, Ila changamoto hawana uwiano sawa wa ukuaji, hii ni kutokana na wakati nna wanunua walikua hawana ukubwa sawa japo walikua Wana umri sawa.

Mpaka Sasa hawajaanza kutaga japo wanatetea Sana. Nimeambiwa changamoto inaweza ikawa lishe ya awali(yaani wakati wakiwa vifaranga au lishe ya Sasa). Yaani wanasema kuku anaetakiwa kutaga baadae analishwa tofauti na kuku anaetakiwa nyama kipindi Cha kifaranga(bado nafanya utafiti nitaleta mrejesho)

Lakini pia wanasema kuku ukimlisha chakula chenye mashudu mengi, mwili unatengeza mafuta Sana na kuharibu mfumo wa mayai(bado nafanya utafiti nitaleta mrejesho)

Nimefanikiwa kuuza kuku mmoja kwa sh 18,000 na nimepanga kupunguza majogoo kwa sh 20,000 pasaka hii. Na Kama utafiti juu ya chakula kipindi Cha kifaranga kinaweza kuwa sababu ya kushindwa kutaga vizuri au kutaga kabisa basi nitawauza wote nianze upya

Nimefanikiwa pia kutengeneza mashine ya kutotolesha mayai (incubator) ambayo Jana tarehe 31 March imefanikiwa kutotolesha mayai 42 Kati ya 53 ya kanga na mayai 60 Kati ya 60 ya kuku.
Mashine hii Ina uwezo wa kutotolesha mayai tray 6 sawa na mayai 180 mpaka 200.

Mpango ni kutengeneza nyingine ya mayai 720 mapema mwezi huu baada ya kupata matokeo mazuri ya mashine ya awali.

Nitaendelea kutoa mrejesho kwa maendeleo zaidi. Asante
Hongera Mkuu kwa kupiga hatua, hawa Kuku namna unavyowapa chakula kinachangia katika kuwafanya wawe wanataga kwa sana Mayai au wa Nyama...

Kipindi tunanunua Mzee aliyetuuzia alituonyesha kuku ambao aliwalisha vizuri kwa ajili ya nyama wanavyokua, na wale aliowalisha kwaajili ya mayai wanavyokua. Pia akatupa na formula ya chakula kuanzia wakiwa wadogo mpaka wanakua kwaajili ya kutaga mayai sema sasa karatasi nililoandikia hzo formula sikumbuki niliweka wapi ila ukipata wataalamu wanaweza kukusaidia.
 
Hongera chief.....ila nikwambie kitu, hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku.

Sasso sio a layering breed....ni kuku kwaajili ya nyama. Uwezo wao wa utagaji ni mdogo sana, na ni chini ya asilimia 30 kwa siku.

Tafuta breed nzuri kwaajili ya mayai. Nakuhakikishia hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku. Nitafute kwa mwongozo zaidi.
Fanya tafiti kijana. Usilazimishe matokeo ulioyapata kwako iwe ndio final say.

Kwa Sasa nimeanza kutotolesha wa Malawi. So nitakuwa na breed mbili na nitaleta mrejesho
 
Nimefuga hawa kuku na wife ndio msimamizi mkuu ila tumekosa wateja.
Idadi 150 wapo kahama wana miezi 5. Tufahamishane kwa anaejua wateja maana nimeweka tangazo humu na kuzunguka kahama lakini hola
Unawauza Bei gani na wamefikisha uzito kiasi gani? Pasaka inakuja endelea kufanya matangazo huenda Mambo yakawa mazuri.
 
Hongera chief.....ila nikwambie kitu, hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku.

Sasso sio a layering breed....ni kuku kwaajili ya nyama. Uwezo wao wa utagaji ni mdogo sana, na ni chini ya asilimia 30 kwa siku.

Tafuta breed nzuri kwaajili ya mayai. Nakuhakikishia hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku. Nitafute kwa mwongozo zaidi.
Upo sahihi Mkuu lkn kuku wa sasso ni chotara ivyo anaweza kufungwa kwa ajili ya nyama au mayai so chakula ndio kinacho fanya awe wa mayai au wa nyama na sio Breed kama unavyo zani ww

Ipo ivi endapo utampa 18-20 % ya protein kwenye chakula pindi akiwa na umli wa 1-8 week then ukampatia 16-18% ya protein pindi akiwa na umli wa 9-16 then kwanzia week ya 17 na kuendelea ukimpa 18-20 ya protein basi utagaji utakuwa juu lkn endapo protein ikawa juu Zaid ya apo wazi kutaga

Pia kuku aina ya sasso anavyo kuwa na umli wa 16 na kuendelea inabid apate mwanga kwa masaa 16 pia Giza kwa masaa 8 kwasababu atafanya utakagaji utakuwa mkubwa maana pituitary grand ya kuku inakwa active endapo ikipokea mwanga kwa masaa 16 ivyo kufanya kazalisha homorne ya utengenezaji wa mayai kwa kiasi kikubwa
 
Hongera sana mkuu. Ni mawazo mazuri sana. Kwa kusimamia mwenyewe hakika utafanikisha malengo yako na Mungu wetu wa mbinguni akutangulie. Ulishawahi kufuga before? Mimi pia hadi sasa nafanya kama unachofanya, nimeanza mwaka jana September na maendeleo siyo haba. Mimi ninafuga almost ndege (Wafugwao) wote wanaopatikana mazingira ya Tz.

Sasa nina haya machache nadhani yanaweza kukufaa;
1. Kwa idadi ya hao matetea unaweza kukomaa ukatotolesha kwa kutumia kuku wenyewe (sina hakika kama sasso wanaatamia). Kwa maoni yangu ni bora kuliko mashine. Ndicho nachofanya. Nilishawauzia watu mashin sana kabla sijaamua kuanza kufiga. Mashine zina changamoto sana ya efficiency. Unaweza peleka mayai 100 ukaambiwa yametotolewa 15. Unaweza zimia au ukahisi umeibiwa. Kuku ukimwekea mayai 13 atakupa walau vifaranga 10. Kuna maelezo mengi sana hapa ya kuelezea. Tuishie hapa kwa sasa.

2. Vifaranga wakitotolewa hakikisha wanakaa juu na poop inadondoka chini. Yaani jenga kitu kama chanja hivi ili huduma zao zote wapate wakiwa juu. Ukifuga hii staili ya siku zote vifaranga wakakaa chini/kwenye maranda utaumia sana. Utachukia ufugaji. Ukifanya hii staili nakuhakikishia hatakufa kofaranga yeyote kwa ugonjwa.

3. Hakikisha unajipanga kwa chanjo zote za muhimu za kuku. Japo kwa hiyo staili ya ukaaji hapo juu (2) niliyosema hata ukiamua usichanje watakua vizuri tu. But no need to risk kwa project kubwa. Wapige chanjo zote muhimu.

4. Hakikisha maji na chakula wanapata ipasavyo na kwa wakati. Bila kusahau usafi wa vyombo. Usicheze na usafi kabisa.

5. Jipe muda wa kukaa na kuku bandani na kiwaangalia, wasome tabia zao. Hii itakusaidia kujua kama kuku anaumwa au la. Kuna muda ugonjwa unaweza ingia usifahamu ukachelewa kuwapa dawa halafu ukakuumiza.

6. Vifaranga hakikisha wanakula super starter (pellet) kwa wiki 2 za mwanzo. Pia katika wiki hizi mbili za mwanzo ukiweza wanyweshe maji yenye multvitamin, OTC 20, Trimazine, Amplorium.

7. Hakikisha hizo dawa hapo juu plus fluban muda wote uko nazo ndani.

8. USAFI wa banda ni muhimu muda wote kama kuku wenyewe walivyo muhimu!

Anyway, yapo mengi ya kuelezea. Muhimu FOCUS.

Kila la heri mkuu!

Dongbei.

*
Natunza hii kwa matumizi ya baadae.
 
""Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua""

Hii 👆👆👆 ni nini?
Mpunga au?

Ila pia kuku ratio huwa ni matetea 10 - 12 kwa jogoo mmoja.

#YNWA
 
Namba mbili naomba unifunze vizuri mkuu
 
Ilikua nyanya mkuu Ila nashukuru nilifanikiwa kuvuna na Sasa naweka Tena mbegu chini kwa ajili ya msimu wa April mpaka kiangazi.
""Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua""

Hii 👆👆👆 ni nini?
Mpunga au?

Ila pia kuku ratio huwa ni matetea 10 - 12 kwa jogoo mmoja.

#YNWA
 
Nimefuga hawa kuku na wife ndio msimamizi mkuu ila tumekosa wateja.
Idadi 150 wapo kahama wana miezi 5. Tufahamishane kwa anaejua wateja maana nimeweka tangazo humu na kuzunguka kahama lakini hola
Hao unaweza kuwauza kwa kiwanda Cha alpha choice wananunua kuku kwa ajili ya kuwaprocess kuwapeleka nchi za uarabuni ni pm nikuunganishe na fomeni wa kiwanda UWE unauza kwao wananunua kuanzia kuku 50 na kuendelea

sent from HUAWEI
 
Shukrani mkuu
 
Hongera chief.....ila nikwambie kitu, hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku.

Sasso sio a layering breed....ni kuku kwaajili ya nyama. Uwezo wao wa utagaji ni mdogo sana, na ni chini ya asilimia 30 kwa siku.

Tafuta breed nzuri kwaajili ya mayai. Nakuhakikishia hutapata mayai zaidi ya matano kwa siku. Nitafute kwa mwongozo zaidi.
Mimi nniliwafuga saso na walitaga kila siku. Niliwapa chakula kidogo Cha kuchanganya na makombo
 
Back
Top Bottom