Hans Raphael 23
New Member
- Aug 5, 2023
- 1
- 0
nimejifunza mengi sanaaa napenda kusema asante na tuendelee kupeana mrejeshoo hakuna kufanikiwa kwa muda mfupi katika haki wote tujifunze hiloo
Congratulations mkuuMalengo bado ni makubwa sana, mpaka mwisho wa mwaka ujao natarajia kuzalisha kuku wasiopungua 1000 kila baada ya miezi mitatu. Yaani niwe nnaweza kuuza kuku 1000 kila baada ya miezi mitatu, kwa tafsiri nyingine ni kuwa na uwezo wa kuuza kuku 300 kila mwezi.
Ili mipango iende sawa nimejenga cages za kulelea vifaranga ili kila mwezi niwe na uhakika wa kuweka vifaranga 300.View attachment 2785232
Baada ya mwaka 2023 kuisha narudi tena na mrejesho mwingine.
December 2023 nilipata changamoto na kuamua kuuza kuku wote, nilitakiwa nisafiri na bahati mbaya sikuwa na mtu wa kunisaidia kuangalia kuku wangu ambao walikua takriban 100 na kidogo
Kwa sasa nimerudi tena na nna endelea mpaka kieleweke.
Tarehe 30 January nimeingiza vifaranga 100 aina ya sasso, ambavyo kwa sasa vinaelekea kumaliza wiki ya tatu, na tarehe 13 feb nimeingiza vifaranga 100 aina ya sasso vinakaribia kumaliza wiki ya kwanza.
Kwasasa malengo yamebadilika baada ya kuona kukaa na kuku muda mrefu ni gharama na haina tija. Ili upate faida kwenye kuku hawa wa chotara hakikisha unauza kuku wako ndani ya miezi mitatu tu. Ukizidisha unakua hauna uhakika wa kuipata faida kutokana na wanunuzi wengi wa kuku wanapenda kuku bei ya chini, sasa anavyokua zaidi ndio unavyopunguza idadi ya wanunuzi.
Ila unaweza ukachagua kwenye kila batch unayouza ukabakiza kuku 10 kwa ajili ya kuuzia wale wateja wasio na mawazo ya pesa, yaani wanaweza kununua kuku hata kwa 25,000 bila maneno mengi.
Malengo ya mwaka huu ni kuuza kuku sio chini ya 1000 au zaidi.
funza nliwahi jifunza kitambo huku kwa kina KubotaUko vizuri. Nataka nijifunze hapo kwenye hydroponic folder na namna ya kutengenezs funza.