Naingia kwenye kufuga kuku chotara (Saso)

Nimefuga hawa kuku na wife ndio msimamizi mkuu ila tumekosa wateja.
Idadi 150 wapo kahama wana miezi 5. Tufahamishane kwa anaejua wateja maana nimeweka tangazo humu na kuzunguka kahama lakini hola
Hola kivipi, kwamba wanunuzi hawawataki?
 
Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua, huku nyanya nazo zikiwa zinachechemea, nimeamua kuanza ufugaji wa kuku chotara Aina ya sasso wakati tunaendelea kusubiri neema ya mvua Kama itatuwezesha kuvuna.

Mpango ni kufikisha kuku 1000 na zaidi mpaka mwisho wa mwaka huu 2022.

Kwa Sasa nimeanza na kuku 25 (mitetea 20 na majogoo 5) ambao nimewanunua December 26 wakiwa na miezi miwili.

Malengo makuu ni kusubiri kuku wafike umri wa kutaga kuanzia march 2022 (wakiwa wamefikisha miezi 5) ili nitotoleshe mayai.

Kuku wakianza kutaga nategemea kupata wastani wa mayai 10 kwa siku (kwa uchache) sawa na mayai 100 Kila baada ya siku 10. Hii inamaana Kila baada ya siku 10 nitapeleka mayai 100 kutotolesha.

Baada ya siku 120 ambayo ni wastani wa miezi 4 kuanzia mwezi March sawa na mwezi July 22 nitakuwa nimetotolesha mayai 1200 ambayo kwa wastani nitapata vifaranga 1000 na kidogo (hayo mayai 200) naasume baadhi yatakuwa hayajatotoleshwa au vifaranga watakaoshindwa kuvuka nursery stage.

Kwahiyo mpaka inafika December 2022(insha_Allah) nitakuwa na kuku 1000 ambao ukiachana na parent 25 nilionza nao kutakua na wakubwa wenye miezi 6,5,4(watakua wameanza kutaga) size ya Kati na wadogo kabisa batch ya mwisho miezi miwili.

Baada ya kufikisha idadi hiyo nitaanza kuuza mayai au kutotolesha vifaranga kwa ajili kuuza au kwa ajili kufuga wa nyama.

KUHUSU GHARAMA
Kuku nimenunu 8000 Kila mmoja sawa na 200,000 kwa kuku wote.

Banda lilikuwepo linalowatosha kuku hao 25.

Kwa kuku watarajiwa Banda lao natarajia kuanza kuhangaika nalo baada ya kuku kuanza kutaga. Ambalo nitalijenga kwa awamu nne ( Kila awamu nitakamilisha sehemu ya kuku 300) makisio ya gharama za ufundi kwa Banda la kisasala kuku 1000 na zaidi ambalo nimeandaa eneo la (20x10)m nimepata ni shilling 3.5M kwa materia ya eneo nililokuwepo.

KUHUSU CHAKULA
Kutokana nimewanunua wakiwa wakubwa nimetengeneza mchanganyiko wangu wa chakula ili kupunguza gharama.
Ambapo gharama za debe moja(baada ya kuchanganya) ni chini ya 3000 na kuku wote 25 wanakula debe 1 na nusu kwa mwezi. Na nimeanza mchakato wa kutengeneza funza na hydroponic folders na baadae nitaandaa bwawa la azola.

Baada ya kufikisha kuku 1000 makadirio ya chakula kwa siku ni kilo 130 ambazo ni sawa kwa mchanganyo wangu wa chakula + hydroponic ni 500 kwa kilo.
Sawa na sh 65,000 kwa siku

KUHUSU MATARAJIO YA FAIDA
kwa mwaka huu wote wa 2022 silengi kupata faida, nahitaji mradi ujisogeze na uwe stable. Kwa maana mpaka inafika December 2022 mradi uwe umerudisha gharama zangu japo kwa uchache na uwe inaweza kujiendesha kwa kuuza mayai au kuku.

Baadaya ya mwaka huu nategemea kupata faida Kama ifuatavyo.

1. Kwa kuwa natarajia kwenye kuku 1000 kuwe na mitetea isiyopungua 800 hivyo nategemea kukusanya mayai yasiopungua 510 kwa siku(kwa makadirio ya chini. Sawa na tray 17 kwa siku .

Tray 1ni sawa na tsh10,000 kwa mayai ya chotara (Bei za nilipo) sawa na tsh 170,000 kwa siku

NB: Mradi huu nitausimamia mwenyewe kwa asilimia 100 hivyo hakuta kuwa na gharama za ziada za mfanyakazi.

Hivyo ndivyo nitavyoiishi 2022.
Nakaribisha maoni.
Hongera sana ndugu yangu, samahani ningependa kupata mawasiliano yako hasa namba ya simu nizungumze na wewe. Nina tanguliza shukrani za awali!
 
Mrejesho namba 2.

Jana tarehe 24April Nimefanikiwa kuuza kuku wote walioko bandani niliowanunua december 26.
Majogoo makubwa nimeuza kwa shiling 20,000 na kuku wadogo kabisa (ambao walikua wawili tu) nimeuza kwa shilingi 10,000.
Wengi nimeuza kati ya 17,000 na 13,000.

Kuhusu faida: Faida haijapatikana yenye tija ila gharama zangu zimerudi na kifaida kidogo sana.

Uamuzi wa kuuza kuku wote ni baada ya kugundua kuku nilinunua kwa mfugaji ambao aliwaandaa kwa ajili ya nyama na sio mayai. Hivyo malengo yangu yasingeweza kutimia kwa kutaka kupata mayai mengi kwa ajili ya kutotolesha na mengine kuuza.

(ANGALIZO) Kabla ya kununua kuku alienza kufugwa na mfugaji mwingine hakikisha unajua aliwafuga kwa ajili ya nyama au mayai.
Kuku anaefugwa kwa ajili ya kutaga anatakiwa aandaliwe kwa lishe kuanzia akiwa kifaranga wa wiki mbili.

Kutokana na changamoto hiyo nimeamua kuanza tena na vifaranga wa siku moja ili niweze kuwaandaa kwa ajili ya kutaga na waweze kuendeleza malengo ya 2022.

Magonjwa ya kuku wa chotara yanayosumbua sana ni Mafua na Kuhara. Magonjwa haya ni rahisi sana kuyathibiti kuliko kuyatibu. Gharama za dawa za kuku ni ghali sana, na unaweza ukatumia hata dozi zaidi ya mbili na wasipone. Hivyo kwa wewe unaesoma mrejesho huu jitahidi sana kuondoa mazingira ya magonjwa karibu na kuku wako ili kuepuka gharama za ziada za dawa.

Nyongeza: Soko la kuku lipo sana, nilianza kuuza kuku pasaka kwa kuwaambia watu wachache, ila hivi sasa ninatafutwa na watu wengi sana wanatafuta kuku. Hivyo masoko sio tatizo. Na huwezi kuliona soko lilipo mpaka uwe na bidhaa.

Nitaendelea kuleta mrejesho baada ya kuingiza vifaranga bandani.
Kazi iendelee
 
Mimi nataka kutengeneza incubator yangu ndogo kama ya mayai 300 hivi nakua nanunua mayai nakutotolesha ili kuokota mayai isiwe kipaumbele changu kazi yangu inakua ni kuuza tu mtu akatafute hasahasa nimewalenga Sasso
 
Mkuu CoderM, wewe ni mzoefu naomba kuuliza. Nataka kufuga kuku chotara nichukue kloira kuku mia kwa ajili ya mayai tu, ila wakifikisha miezi mitatu nitayapunguza majogoo nitabakaisha wachache pmj na tetea. Lengo atleast kila siku niwe natoa tray moja ya mayai. Kwa uzoefu wako na gharama za chakula na dawa, je itanilipa hata kidogo tu?
 
Nimechukua vifaranga 200 vya Sasso kwa ajili ya mayai maana uku nilipo mayai ya kuku wa kisasa watu awapendelei ivyo nimeona ni bora ni fugue kuku aina ya Sasso kuliko wa kienyeji then nije kufungua duka la kuuza Mayai tuu

Nitakuwa nawapa mrejesho kila baada ya siku Saba kuhusu ulaji wao na ukuaji wao lkn sijatumia chakula Cha sliver land so nimetengeneza Cha kwangu Mimi mwenyewe
 
Nimesha-subscribe.
 
Mrejesho 1

Tarehe 26/04/2022 nilichukua box mbili za vifaranga vya sasso kutoka makota Iringa kila box lilikuwa na vifaranga 102 ivyo ikafanya idadi na kuwa 204

Maandalizi ni kama yafuatayo

1 Chakula (Nilitengeneza mm mwenyewe kama ifuatavyo)

starter inabid iwe na 20-18 % ya Digestible Crude Protein ( DCP) ili kufanya kifaranga kiote manyoya haraka ili kujikinga na baridi, Chakula hichi watakula kwa miezi miwili then nitabadilisha mfumo wa kuchanganya

Mahindi yalio balazwa 65 Kg
Mashudu yalio balazwa 22 kg
Uduvi ule mdogo wa langi ya red-silver 8 kg
Diphosphate calcium (DCP) 1 kg
Chokaa ya kuku 2.50 kg
Mifupa 1 kg
Chumvi ya jikon 500 g

Nilitengeneza 100 kg Kwa awamu ya kwanza lengo la kufanya ivyo ili chakula kisikae muda mlefu kikawa na Sumukuvu maana huwa inasababisha kuku kufa

Ili kupata Mahindi na mashudu yalio balazwa inabidi uende mashineni wanapo saga unga wa ugali then unamwambia yule operator atoe ile chekeche kwenye machine ya kusagia then akipitisha ayo Mahindi zinatokea chenga chenga ambazo kifaranga kitaweza kula vizuri

2 Jiko
Nilinunuwa Yale majiko special kwa ajili ya vifaranga yapo kama chungu ivi lkn kina matundu pembeni na mfuniko juu
Ivyo kama moto ukiwaka tayali nafunika juu na ule mfuniko ivyo joto linaweza kudumu kwa muda wa masaa 5-6 endapo ukifunika lkn ukiacha wazi 2-3 masaa tayali joto linapotea

3 Sehemu vifaranga vinapo shinda
Nilinunuwa magazeti kilo 3 na board moja, mbao ya 2 by 4 na mapumba ya mpunga ( rice husk )

Mapumba ya mpunga nilitandika chini ili kuzuia unyevu usipande juu na kunyonya maji endapo yakimwagika

Magazeti kwa ajili ya kutandika chini maana inabid utandike matabaka 3 ya magazeti then kila siku lile tabaka la juu unalitoa then unaweka lingine

Board kwa ajili ya kutengeneza round ili vifaranga wasife maana wanatabia ya kujikusanya kwenye Kona kwa pamoja ivyo ukutumia board sio lahisi kupata Kona

Mbao 2 by 4 izi ni kwa ajili ya kuunganisha board moja na nyingine ivyo nilizichana kidogo katikati ili kukutanisha board mbili na kutengeneza round

Eneo nililo tumia kwa hatua za mwanzo ni 1.5 m kwa 1.5 ili vifaranga wapate joto na muda mwingi watumie kula na kupumzika kuliko kutembea lkn baada ya week ya pili nitaongeza ukubwa wa eneo

4 Vyombo vya kulia
Nilinunuwa dinker 4 na feeder 6 Kwa awamu ya kwanza lkn kwa upande wa feeder natumia kile kisahani tuu

5 Mpangilio wa kimiminika ( Maji)

Ile siku nilio waleta ( hii siku sio siku ya kwanza maana siku inakuwa na masaa 24 ivyo inakuwa Zero day) niliwapa maji yenye mchanganyiko wa Glucose na Vitamin kwa masaa mawili kabla sija wapa chakula lengo la kufanya ivyo ni kuwapatia nguvu kutokana na uchovu wa safari na kufungua mfumo wa kumengenya chakula

Siku ya kwanza hadi ya Tano
Niliwapa maji yenye mchanganyiko wa Antibiotic lengo la kufanya ivyo nikukausha vitovu ili wasipate tatizo choo kuganda ( Constipation )

Siku ya sita ambayo ni Leo
Niliwapa maji ambayo ayana mchanganyiko wa kitu chochote kile

Siku ya Saba ambayo ni kesho
Nitawapa chakula then baada ya masaa manne nitawapa maji yenye mchanganyiko wa dawa ya kideli (Newcestle) kwa masaa mawili tuu then baada ya hapo nitawapa maji ya kawaida

Mafanikio

✓Hadi sasa akijafa ata kifaranga kimoja

✓Akuna kifaranga kilicho pata ulemavu

✓Asilimia 75 ya vifaranga mabawa Yao tayali yamefunikwa na manyoya ivyo inaonyesha chakula ni kizuri kwa hatua za mwanzo za ukuaji

✓Vifaranga vinakula sana mida ya asubuhi kuliko mchana ivyo inaonyesha afya Yao ni nzuri na mfumo wa umengenyaji umekaa vizuri

✓Akuna kifaranga aliye pata tatizo la choo kigumu

Changamoto

✓Kila baada ya masaa manne inabidi niwepo bandani ivyo inakuwa vigumu kufanya ivyo maana nakuwa nipo kwenye majukumu memgine kwaiyo inabid kila baada ya masaa sita ndio niwepo bandani

✓Kuamka usiku inakuwa ni tatizo maana sijazoea ivyo Kuna bahadhi ya siku huwa napitiliza hadi asubuhi

✓Vifaranga vinapendelea sana uduvi kuliko Mahindi na mashudu ivyo inabid nisubilie kwanza then ndio wanaanza kula Mahindi na mashudu

Mwisho

Mrejesho 2 nitauleta tena jumatatu ijayo Yani siku ya 13
View attachment 2208838View attachment 2208839View attachment 2208840
 
I’m touched,
Endelea kutupa update kila upatapo nafasi ili kutupa elimu hii adhimu.

Binafsi niko mbioni kuanza project kama yako, unanipa motisha sana.

Ubarikiwe mno.
 
Pamoja Mkuu tuombeane uzima ayo mengine yatakuja tuu
 
Unafugia wap
 
Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua, huku nyanya nazo zikiwa zinachechemea, nimeamua kuanza ufugaji wa kuku chotara Aina ya sasso wakati tunaendelea kusubiri neema ya mvua Kama itatuwezesha kuvuna.

Mpango ni kufikisha kuku 1000 na zaidi mpaka mwisho wa mwaka huu 2022.

Kwa Sasa nimeanza na kuku 25 (mitetea 20 na majogoo 5) ambao nimewanunua December 26 wakiwa na miezi miwili.

Malengo makuu ni kusubiri kuku wafike umri wa kutaga kuanzia march 2022 (wakiwa wamefikisha miezi 5) ili nitotoleshe mayai.

Kuku wakianza kutaga nategemea kupata wastani wa mayai 10 kwa siku (kwa uchache) sawa na mayai 100 Kila baada ya siku 10. Hii inamaana Kila baada ya siku 10 nitapeleka mayai 100 kutotolesha.

Baada ya siku 120 ambayo ni wastani wa miezi 4 kuanzia mwezi March sawa na mwezi July 22 nitakuwa nimetotolesha mayai 1200 ambayo kwa wastani nitapata vifaranga 1000 na kidogo (hayo mayai 200) naasume baadhi yatakuwa hayajatotoleshwa au vifaranga watakaoshindwa kuvuka nursery stage.

Kwahiyo mpaka inafika December 2022(insha_Allah) nitakuwa na kuku 1000 ambao ukiachana na parent 25 nilionza nao kutakua na wakubwa wenye miezi 6,5,4(watakua wameanza kutaga) size ya Kati na wadogo kabisa batch ya mwisho miezi miwili.

Baada ya kufikisha idadi hiyo nitaanza kuuza mayai au kutotolesha vifaranga kwa ajili kuuza au kwa ajili kufuga wa nyama.

KUHUSU GHARAMA
Kuku nimenunu 8000 Kila mmoja sawa na 200,000 kwa kuku wote.

Banda lilikuwepo linalowatosha kuku hao 25.

Kwa kuku watarajiwa Banda lao natarajia kuanza kuhangaika nalo baada ya kuku kuanza kutaga. Ambalo nitalijenga kwa awamu nne (Kila awamu nitakamilisha sehemu ya kuku 300) makisio ya gharama za ufundi kwa Banda la kisasala kuku 1000 na zaidi ambalo nimeandaa eneo la (20x10)m nimepata ni shilling 3.5M kwa materia ya eneo nililokuwepo.

KUHUSU CHAKULA
Kutokana nimewanunua wakiwa wakubwa nimetengeneza mchanganyiko wangu wa chakula ili kupunguza gharama. Ambapo gharama za debe moja(baada ya kuchanganya) ni chini ya 3000 na kuku wote 25 wanakula debe 1 na nusu kwa mwezi. Na nimeanza mchakato wa kutengeneza funza na hydroponic folders na baadae nitaandaa bwawa la azola.

Baada ya kufikisha kuku 1000 makadirio ya chakula kwa siku ni kilo 130 ambazo ni sawa kwa mchanganyo wangu wa chakula + hydroponic ni 500 kwa kilo. Sawa na sh 65,000 kwa siku

KUHUSU MATARAJIO YA FAIDA
kwa mwaka huu wote wa 2022 silengi kupata faida, nahitaji mradi ujisogeze na uwe stable. Kwa maana mpaka inafika December 2022 mradi uwe umerudisha gharama zangu japo kwa uchache na uwe inaweza kujiendesha kwa kuuza mayai au kuku.

Baadaya ya mwaka huu nategemea kupata faida Kama ifuatavyo.

1. Kwa kuwa natarajia kwenye kuku 1000 kuwe na mitetea isiyopungua 800 hivyo nategemea kukusanya mayai yasiopungua 510 kwa siku(kwa makadirio ya chini. Sawa na tray 17 kwa siku .

Tray 1ni sawa na tsh10,000 kwa mayai ya chotara (Bei za nilipo) sawa na tsh 170,000 kwa siku

NB: Mradi huu nitausimamia mwenyewe kwa asilimia 100 hivyo hakuta kuwa na gharama za ziada za mfanyakazi.

Hivyo ndivyo nitavyoiishi 2022.

Nakaribisha maoni.
Hongera Sana mkuu
 
Huko singida si wamejaa sana kuchi
Kwanini umeamua kufuga saso

Nipe tofaut ya gharama kufuga kuchi na saso according to mpango kazi wako
Ni kweli kuchi wapo lkn ukuwaji wake sio mzuri kama wa sasso pia kwa sasa kuku aina ya Sasso wanapendwa sana sokoni kutokana na uzito wake

Kuhusu gharama sijajua kwa upande wa kuchi Mkuu lkn kwa Sasso nitakupa kila nitakavyo kuwa naleta mrejesho

Malengo ya kufuga Sasso ni kwa ajili ya Mayai maana wanataga wakiwa na week 20 ivyo nitafungua duka la kuuza Mayai tuu pia nataka niwe nauza majogo kila baada ya miezi mitatu maana utagaji wa kuku autegemei jogoo ivyo nitakuwa nauza majogo na kubakia na matetea
 
Wadau nmetotolesha vifaranga kutoka kwenye mayai haya ya kisasa....nawalisha chakula vizuri....na sa iv wana wiki kama 8 hivi....je hawa kuku wana uwezo wa kuja kutaga mayai kwa ajili ya biashara???
 
Back
Top Bottom