Naomba ushauri juu ya kufuga kuku Hawa!

Sambinyakwe kitololo

JF-Expert Member
Nov 15, 2022
2,420
2,880
Habari za mids hii

Siku Kama nne hivi zilizopita nimenunua vifaranga 7 aina ya saso , sijawahi kufuga kuku ndo nimeamua jaribu , baada ya kuwachukua nilinunua starter 1Kg ndo wanaila ila hapa

Sasa naomba kuuliza utaratibu ukoje kuhusu chanjo Ni ipi na Kila baada ya muda gani , je wakiwa wanaumwa i.e kuharisha kusinzia niwape Nini

Kuhusu lengo la kuwafuga Bado sijajua kuwa nitaacha watage au nitawatafuna kabla hawajataga

Ushauri wenu tafadhali kwa Sasa naona Wana afya njema wanaruka ruka huko nje kwa makisio Wana week bila shaka nilisahau uliza niliponunua
 
Kuku 7 mbona itakuwa ghalama kuwahumia? Bora wangekuwa hata 50,mfano Chanjo ukinunua unachanja kuku 7 tu inayobaki haifai kuitunza unaitupa huoni ni ghalama?
Kweli

Kwa hio Bora ninunue wakubwa tusio

Maana nilitaka wapishanisha wakiwa naweek mbili nanunua wengine hivo chanjo Ni ile ile
 
Habari za mids hii

Siku Kama nne hivi zilizopita nimenunua vifaranga 7 aina ya saso , sijawahi kufuga kuku ndo nimeamua jaribu , baada ya kuwachukua nilinunua starter 1Kg ndo wanaila ila hapa

Sasa naomba kuuliza utaratibu ukoje kuhusu chanjo Ni ipi na Kila baada ya muda gani , je wakiwa wanaumwa i.e kuharisha kusinzia niwape Nini

Kuhusu lengo la kuwafuga Bado sijajua kuwa nitaacha watage au nitawatafuna kabla hawajataga

Ushauri wenu tafadhali kwa Sasa naona Wana afya njema wanaruka ruka huko nje kwa makisio Wana week bila shaka nilisahau uliza niliponunua
Ni ngumu kumudu gharama ya chanjo Kwa idadi hiyo ya kuku wachache sana utakula hasara.
 
Habari za mids hii

Siku Kama nne hivi zilizopita nimenunua vifaranga 7 aina ya saso , sijawahi kufuga kuku ndo nimeamua jaribu , baada ya kuwachukua nilinunua starter 1Kg ndo wanaila ila hapa

Sasa naomba kuuliza utaratibu ukoje kuhusu chanjo Ni ipi na Kila baada ya muda gani , je wakiwa wanaumwa i.e kuharisha kusinzia niwape Nini

Kuhusu lengo la kuwafuga Bado sijajua kuwa nitaacha watage au nitawatafuna kabla hawajataga

Ushauri wenu tafadhali kwa Sasa naona Wana afya njema wanaruka ruka huko nje kwa makisio Wana week bila shaka nilisahau uliza niliponunua
Gharama sana kwa kuku hao in terms of chanjo. Maana kwa kawaida ziko 3. Newcastle, gumboro na ndui. Chanjo hizo zinapishana siku saba sana na jumla si chini ya 20. Dawa ukishagungua haitumiki tena.
 
Dawa ikishafunguliwa haifai Tena?

Na chanjo Ni siku ngapi au moja? Au siku kadhaa

Nikishawapiga wote narudia Tena lini au ndo mazima mpaka wanachinjwa

Pia nilinunua Israel Wana mafua je niwape dawa gani
 
Chanjo siyo bei sana mkuu usiogope ndui ndiyo inauzwa kwenye 10k nayo nunua ile ya kuchoma na sindano usijekununua tatu moja utalia, newcastle inauzwa 2900-3500, gumboro nayo ni humuhumo,

Baada ya siku saba wape newcastle baada ya siku 14 gumboro utarudia tena newcastle tena gumboro halafu ndui ila hakikisha mazingira yawe safi ili wasipate mafua na uwape na dawa ya minyoo

Hongera kwa kuanza ufugaji mkuu
 
Minyoo asisahau na mafua.
 
Mkuu kwanza pole kwa kutapeliwa, hao vifaranga uliouziwa sio sasso vinaitwa vijogoo, ni madume wa layers, bei zake kwa sasa ni 500 kwa mmoja pia ukuaji wao ni wa taratibu sana kuliko hata wa kienyeji.
 
Wakiwa na umri gani je Kama wamepewa huko maana Nina wengine wakubwa nahisi Wana mwezi hivi according to wauzaji

Gharama sana kwa kuku hao in terms of chanjo. Maana kwa kawaida ziko 3. Newcastle, gumboro na ndui. Chanjo hizo zinapishana siku saba sana na jumla si chini ya 20. Dawa ukishagungua haitumiki tena.
 
Chanjo siyo bei sana mkuu usiogope ndui ndiyo inauzwa kwenye 10k nayo nunua ile ya kuchoma na sindano usijekununua tatu moja utalia, newcastle inauzwa 2900-3500, gumboro nayo ni humuhumo,

Baada ya siku saba wape newcastle baada ya siku 14 gumboro utarudia tena newcastle tena gumboro halafu ndui ila hakikisha mazingira yawe safi ili wasipate mafua na uwape na dawa ya minyoo

Hongera kwa kuanza ufugaji mkuu
 
Attachments

  • IMG_20231030_123823.jpg
    IMG_20231030_123823.jpg
    422.7 KB · Views: 5
Nimenunua na size hio sijawapa chanjo bado yoyote nahisi Hadi wamefika umri huo tayari Wana chanjo

Nimewapa dawa mbili tu hizi hapa chini
IMG-20231030-WA0016.jpeg

Kuna ambao Wana mafua tuseme Ni wote tu hizo dawa naona Kama Kuna saa zinasaidia Kuna saa mafua yanazidi Hadi mmoja hali anazubaa tu

Last night nikaweka tetracyline wakanywa naona wamechangamka ila mafua hayajaisha naomba ushauri juu ya dawa ya mafua

Pia nasikia ukiwapa chanjo Kama hivo wanakufa
 
Back
Top Bottom