CoderM
Senior Member
- Jun 15, 2015
- 102
- 272
Baada ya mvua za msimu huu kuwa za kusita na kupoteza mbegu kwa kupanda zaidi ya Mara mbili na kuungua na jua, huku nyanya nazo zikiwa zinachechemea, nimeamua kuanza ufugaji wa kuku chotara Aina ya sasso wakati tunaendelea kusubiri neema ya mvua Kama itatuwezesha kuvuna.
Mpango ni kufikisha kuku 1000 na zaidi mpaka mwisho wa mwaka huu 2022.
Kwa Sasa nimeanza na kuku 25 (mitetea 20 na majogoo 5) ambao nimewanunua December 26 wakiwa na miezi miwili.
Malengo makuu ni kusubiri kuku wafike umri wa kutaga kuanzia march 2022 (wakiwa wamefikisha miezi 5) ili nitotoleshe mayai.
Kuku wakianza kutaga nategemea kupata wastani wa mayai 10 kwa siku (kwa uchache) sawa na mayai 100 Kila baada ya siku 10. Hii inamaana Kila baada ya siku 10 nitapeleka mayai 100 kutotolesha.
Baada ya siku 120 ambayo ni wastani wa miezi 4 kuanzia mwezi March sawa na mwezi July 22 nitakuwa nimetotolesha mayai 1200 ambayo kwa wastani nitapata vifaranga 1000 na kidogo (hayo mayai 200) naasume baadhi yatakuwa hayajatotoleshwa au vifaranga watakaoshindwa kuvuka nursery stage.
Kwahiyo mpaka inafika December 2022(insha_Allah) nitakuwa na kuku 1000 ambao ukiachana na parent 25 nilionza nao kutakua na wakubwa wenye miezi 6,5,4(watakua wameanza kutaga) size ya Kati na wadogo kabisa batch ya mwisho miezi miwili.
Baada ya kufikisha idadi hiyo nitaanza kuuza mayai au kutotolesha vifaranga kwa ajili kuuza au kwa ajili kufuga wa nyama.
KUHUSU GHARAMA
Kuku nimenunu 8000 Kila mmoja sawa na 200,000 kwa kuku wote.
Banda lilikuwepo linalowatosha kuku hao 25.
Kwa kuku watarajiwa Banda lao natarajia kuanza kuhangaika nalo baada ya kuku kuanza kutaga. Ambalo nitalijenga kwa awamu nne (Kila awamu nitakamilisha sehemu ya kuku 300) makisio ya gharama za ufundi kwa Banda la kisasala kuku 1000 na zaidi ambalo nimeandaa eneo la (20x10)m nimepata ni shilling 3.5M kwa materia ya eneo nililokuwepo.
KUHUSU CHAKULA
Kutokana nimewanunua wakiwa wakubwa nimetengeneza mchanganyiko wangu wa chakula ili kupunguza gharama. Ambapo gharama za debe moja(baada ya kuchanganya) ni chini ya 3000 na kuku wote 25 wanakula debe 1 na nusu kwa mwezi. Na nimeanza mchakato wa kutengeneza funza na hydroponic folders na baadae nitaandaa bwawa la azola.
Baada ya kufikisha kuku 1000 makadirio ya chakula kwa siku ni kilo 130 ambazo ni sawa kwa mchanganyo wangu wa chakula + hydroponic ni 500 kwa kilo. Sawa na sh 65,000 kwa siku
KUHUSU MATARAJIO YA FAIDA
kwa mwaka huu wote wa 2022 silengi kupata faida, nahitaji mradi ujisogeze na uwe stable. Kwa maana mpaka inafika December 2022 mradi uwe umerudisha gharama zangu japo kwa uchache na uwe inaweza kujiendesha kwa kuuza mayai au kuku.
Baadaya ya mwaka huu nategemea kupata faida Kama ifuatavyo.
1. Kwa kuwa natarajia kwenye kuku 1000 kuwe na mitetea isiyopungua 800 hivyo nategemea kukusanya mayai yasiopungua 510 kwa siku(kwa makadirio ya chini. Sawa na tray 17 kwa siku .
Tray 1ni sawa na tsh10,000 kwa mayai ya chotara (Bei za nilipo) sawa na tsh 170,000 kwa siku
NB: Mradi huu nitausimamia mwenyewe kwa asilimia 100 hivyo hakuta kuwa na gharama za ziada za mfanyakazi.
Hivyo ndivyo nitavyoiishi 2022.
Nakaribisha maoni.