Naibu Spika Tulia anahangaika na mambo yasiyo na tija anaacha mambo ya Msingi

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,360
11,507
Huwa namfuatilia mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia huyu pamoja na Ubunge ni Naibu Spika ni msomi mzuri wa Sheria. Lakini kiukweli akili ya kisiasa hana kabisa toka anajindaa kuwa Mbunge mpaka anakuwa Mbunge hakuna mambo ya maendeleo ya maana anayoyafanya. unamwona anaangaika na petty issues za kusaidia vijitimu vya mpira, ngoma, utamaduni na mambo madogo madogo yasiyo na tija kwa Mkoa wa Mbeya.

Inahuzunisha sana kuwa anakosa kushughulikia suala la Msingi la kujengwa Tawi la Chuo Kikuu Mbeya kwa kufanikisha na viongozi na wakazi wa Jiji kutoa Uwanja wa Kutosha kwa ajili hiyo ila unamwona anacheza cheza tu kwenye matamasha na sherehe mbalimbali. yaani mambo madogo anayafanya makubwa na mambo makubwa anayafanya madogo.

Ni aibu sana kwa mtu msomi kama yeye na exposure aliyo nayo kushindwa kujua mahitaji ya msingi kwa Mkoa wa Mbeya ni nini. Kila mara utamwona akicheza cheza kwenye matamasha na sehemu mbali mbali na kutoa vimichango mbuzi vya jersey, vifaa vya michezo n.k akisahau mambo muhimu ya msingi kwa ajili ya maendeleo akama shule, hospitali, zahanati, vyuo, barabara au miundo mbinu, mipango mji n.k anazunguka zunguka tu kula bata haonekani akifanya jambo la msingi JIJINI MBEYA. yaani huyu Mbunge ni Gunzi Kabisa.
 
Chuo kikuu cha DSM kampasi ya Mbeya viongozi wasione ni jambo la kawaida na Mh. JK. kuwaambia waandae eneo la kutosha ameonesha mapenzi ya dhati kwa mkoa wa mbeya iki kijengwe chuo chenye hadhi inayoendana na UDSM, pia ni fursa nzuri ya jiji la Mbeya kuchangamka zaidi na kuleta mzunguko mzuri wa pesa ukiangalia Dodoma wanafunzi wa UDOM wakiwa likizo jiji lina shake kiuchumi mzunguko wa biashara unapungua na pana poa sana, sasa wana Mbeya na viongozi wa Mbeya changamkeni na hiyo fursa sababu watu wengi watapata ajira wakati wa ujenzi wa chuo hicho, wajasiliamali watanufaika kwa kufanya biashara na faida nyinginezo.
 
Tulia alibebwa kinguvu sana, ndio maana anasahau kuisaidia mbeya. Elimu kubwa mchango wake mdogo sana.
 
Huwa namfuatilia mbunge wa Mbeya Mjini Dr. Tulia huyu pamoja na Ubunge ni Naibu Spika ni msomi mzuri wa Sheria. Lakini kiukweli akili ya kisiasa hana kabisa toka anajindaa kuwa Mbunge mpaka anakuwa Mbunge hakuna mambo ya maendeleo ya maana anayoyafanya. unamwona anaangaika na petty iunge ni Gunzi Kabisa.
Umesema kweli mkuu ni mnafiki hakuna anachofanya
 
Sasa kwa TAARIFA yako, sisi Watanzania tunapenda Kiongozi anayedhamini Timu za Mpira, anayeshiriki misiba na anayeshiriki nasi shughuli za Ngoma na michezo kiujumla.

Huyo tutampa Kura mpaka aseme basi.

Wakati huo tukisubiri kujengewa Mabarabara na Mahospitali kwa misaada ya Watu wa Merikani.

Viongozi wetu wacha tucheze nao Ngoma, ndiyo shughuli wanaimudu vizuri.
 
Toka Majuzi nafuatilia nyuzi zako naona umetumwa na Sugu kumananga kipenzi chetu cha Mbeya
Pole sana shemeji.... wewe either ni sugu alikukataa au unampenda sana Sugu. Mimi naongea jambo ambalo kama Tulia atalifanyia kazi ni karata yake kubwa sana. yaani hapa nilikuwa nampa siri za ushindi. kama hili wew eunaliona ni dogo unamkumbuka sugu utakuwa na tatizo sana kama alikukataa achana naye ana maisha yake mengine.
 
Sasa kwa TAARIFA yako, sisi Watanzania tunapenda Kiongozi anayedhamini Timu za Mpira, anayeshiriki misiba na anayeshiriki nasi shughuli za Ngoma na michezo kiujumla.

Huyo tutampa Kura mpaka aseme basi.

Wakati huo tukisubiri kujengewa Mabarabara na Mahospitali kwa misaada ya Watu wa Merikani.

Viongozi wetu wacha tucheze nao Ngoma, ndiyo shughuli wanaimudu vizuri.
Hapa umenena vyema.
 
Back
Top Bottom