Naibu Msajili Mahakama ya Uhujumu aainisha masharti ya kusikiliza kesi ya Mbowe

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
16 September 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi azungumzia utaratibu wa kuingia ndani ya Mahakama Kuu Maalum na kusikiliza kesi inayowakabilu Mbowe na wenzie 3.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Magdalena Ntandu, amefafanua sababu ya kuwepo kwa utaratibu mpya wa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

  • Marufuku kurekodi kwa kutumia simu
  • Hakuna katazo kuingia ndani ya Mahakama
  • Ni haki kuingia na kusikiliza kesi
  • Wawakilishi wa wadau mbalimbali wanaweza kuingia ili kila wadau wapate haki ya kusikiliza. Wadau kama waandishi wa habari, wanafamilia, wawakilishi wa vyama n.k
  • Kurusha mwenendo mzima wa kesi live / mubashara umeleta ukakasi, Mahakama ingependa simu zizimwe
  • Nafasi ni finyu, kuna nafasi 48 tu kwa ajili ya watu kuingia ktk ukumbi wa Mahakama
  • N.k
 
16 September 2021

Kesi namba 16 / 2021 ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi : Watuhumiwa Freeman Mbowe na wenzie 3

Hali ilivyokuwa mahakama kuu Leo 16 September 2021 jijini Dar es Salaam. Shauri la kesi namba 16 / 2021 ya Uhumuju Uchumi

Nchi za commonwealth zenye sheria na vifungu vya katiba zinazofanana na Tanzania kuhusu haki ya kuingia na kusikiliza pia kuripoti toka Mahakamani hawakatazi waandishi n.k kuripoti. Nini sasa Naibu wa Msajili wa Mahakama Kuu divisheni ya Rushwa na uhujumu anatafuta kuweka vikwazo vya kuripoti kesi hii yenye maslahi mapana kwa umma kuelewa kinachoendelea siku baada ya siku ?

17 January 2019
Nairobi, Kenya

Kesi ya Mwilu: Jaji Philomena Mwilu akabiliwa na kesi mahakamani

Nchi nyingine ya commonwealth na ya EAC yenye sheria na vifungu vya kikatiba kuripoti mwenendo wa kesi kwa manufaa mapana ya umma, wanaruhusu kesi kurekodiwa na kurushwa ktk media. Nini tatizo la Mahakama zetu kushiriki kubinya haki hiyo ya kikatiba kwa watanzania wasioweza kufika ktk viunga vya Mahakama Kuu?

18 December 2019

Kampala, Uganda
Male Mabirizi in bitter exchages with high court judge

16 September 2021

Kesi namba 16 / 2021 ya Uhujumu Uchumi na Ugaidi : Watuhumiwa Freeman Mbowe na wenzie 3

Hali ilivyokuwa mahakama kuu Leo 16 September 2021 jijini Dar es Salaam. Shauri la kesi namba 16 / 2021 ya Uhumuju Uchumi

..kwanini mshitakiwa mmoja amefungwa pingu huku wenzake wakiwa hawana?

Cc Petro E. Mselewa , Pascal Mayalla, Erythrocyte
 
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu anasema hawakufurahishwa namna mwenendo mzima wa kesi ulivyoripotiwa na kurushwa mitandaoni kupitia simu za watu waliokuwapo Mahakamani
... Ndio maana wanaambiwa warushe live ili kila interested citizen asikie directly from the horse's mouth nayo hawataki. Halafu eti nchi ya kidemokrasia, uwazi, na utawala wa sheria!
 
Anatumia sheria gani kuzuia kurekodiwa na kurushwa mubashara mwenendo mzima wa kesi kwenye sosho midia?

Je haoni kuwa kurekodiwa na kurushwa mubashara mwenendo wa kesi inasaidia kujibu changamoto ya ufinyu wa nafasi kwenye mahakana na kusaidia watu wengi zaidi kufuatilia mwenendo wa kesi?

:NB. Angekuwa na busara na akili kama msajili wa mahakama angeichukua iyo kama fursa ya kuboresha miundombinu kwa mahakama kuwa na mfumo wa kutoa habari na taarifa kuhusu mienendo ya kesi mbalimbali zilizoko mahakamani ili kutanua uhuru, haki na uwazi katika mahakama.
 
Haya ni mapya kutoka kwa watu wasiojulikana walio ngazi za juu. Kesi kurushwa LIVE kunaathiri kitu gani katika kesi husika?

Back
Top Bottom