Naibu Msajili Mahakama ya Uhujumu aainisha masharti ya kusikiliza kesi ya Mbowe

Wafuasi wa Mbowe sio wa kuwachekea, wanavurugu sana, na hawakawii kuhatarisha amani ya nchi, ni watu ambao hawataki amani itamalaki ktk nchi hii.
 
16 September 2021
Dar es Salaam, Tanzania



Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi azungumzia utaratibu wa kuingia ndani ya Mahakama Kuu Maalum na kusikiliza kesi inayowakabilu Mbowe na wenzie 3.


  • Marufuku kurekodi kwa kutumia simu
  • Hakuna katazo kuingia ndani ya Mahakama
  • Ni haki kuingia na kusikiliza kesi
  • Wawakilishi wa wadau mbalimbali wanaweza kuingia ili kila wadau wapate haki ya kusikiliza. Wadau kama waandishi wa habari, wanafamilia, wawakilishi wa vyama n.k
  • Kurusha mwenendo mzima wa kesi live / mubashara umeleta ukakasi, Mahakama ingependa simu zizimwe
  • Nafasi ni finyu, kuna nafasi 48 tu kwa ajili ya watu kuingia ktk ukumbi wa Mahakama
  • N.k


Inatia moyo kuwa maelekezo haya ya Naibu Msajili yamesokomezwa kule alikookotwa yule profesa 😂😂😂!
 
..mahakama ingeruhusu kesi irushe LIVE.

..hiyo ingeondoa uwezekano wa wenye nia mbaya kuripoti ndivyo-sivyo.

..hata msongamano mahakamani ungekuwa mdogo, kesi ingefuatiliwa kwenye mtandao.

Yaani kwa pendekezo kama hili Mahakama, Jeshi la polisi na wote wanaona kama una kichaa hivi. Kwao hili haliwezekani.
 
17 September 2021

Mwenendo wa kesi baada ya tamko la Naibu Msajili Mahakama Kuu ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

 
Uthibitisho mwengine wa mahakama kutokuwa huru............"mahakama haifurahishiwi"
 
Raia wanahamu ya kufuatilia kesi hii yenye maslahi mapana kwa umma

17 September 2021

Kesi ya Mbowe || Wafuasi wa CHADEMA wapigania kuingia Mahakama Kuu


Mwenyekiti Mhe. Freeman Mbowe na wenzake wakiwasili Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa ambapo leo Septemba 17, 2021 shauri dogo ya kesi ya msingi Na. 16/2021 litaendelea kusikilizwa. Shauri hilo lipo katika hatua ya usikilizwajli wa Mashahidi upande wa Jamhuri.

Source: mwanzo tv
 
Hivi ruling ya mahakama kuu si ilishatpka kwamba utaratibu wa kurusha live na kurekodi hauna shida. Huyu mama hana taarifa? Mawakili wa serikali waliombwa kutoa kifungu cha sheria kinazuia hilo kufanyika wakashindwa hivyo ruling ikatoka watu waendelee. Huyu mama hajui mahakama inaongozwa kwa sheria na sio siasa? Ni hatari sana mahakama ikijiingiza kwenye hii trap ya wanasiasa.
16 September 2021
Dar es Salaam, Tanzania



Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi azungumzia utaratibu wa kuingia ndani ya Mahakama Kuu Maalum na kusikiliza kesi inayowakabilu Mbowe na wenzie 3.


  • Marufuku kurekodi kwa kutumia simu
  • Hakuna katazo kuingia ndani ya Mahakama
  • Ni haki kuingia na kusikiliza kesi
  • Wawakilishi wa wadau mbalimbali wanaweza kuingia ili kila wadau wapate haki ya kusikiliza. Wadau kama waandishi wa habari, wanafamilia, wawakilishi wa vyama n.k
  • Kurusha mwenendo mzima wa kesi live / mubashara umeleta ukakasi, Mahakama ingependa simu zizimwe
  • Nafasi ni finyu, kuna nafasi 48 tu kwa ajili ya watu kuingia ktk ukumbi wa Mahakama
  • N.k
 
Lema - Kesi yangu Mahakama ilikubadili kufunga spika



Kesi yangu watu walijaa sana, nikaomba nilete spika wananchi wasikilize wakiwa nje, hakimu akasema Lema usipate tabu Mahakama itafunga spika. Na kweli spika zilifungwa na mahakama hivyo watubwakaweza kufuatilia kesi vizuri.
 
18 September 2021

Maoni ya Wakili Emmanuel Augustino : Mwenendo Kesi ya Mbowe - Wiki 3 Bado kesi ya msingi namba 16 / 2021 Kusikilizwa, kufuatia Mapingamizi Yatawala ndani ya kesi ndogo ya kesi ya msingi namba 16 / 2021 ya Ugaidi

Kesi Iliyokuwa Imepangwa Kusikilizwa Mfululuzo, Imeshindikana Kusogea Baada Ya kutawaliwa Na Mapingamizi anasema wakili Emmanuel Augustino.

Wakili Emmanuel Augustino anachambua tija Ya mapingamizi hayo na mwenendo mzima wa kesi inayosikilizwa mbele ya Mh Jaji Mustapher M. Siyani .
Source: Channel1TV
 
Back
Top Bottom