Nahitaji msaada wenu wa haraka

IqraNI

Senior Member
May 16, 2020
140
136
Ndugu wanajamii, nawasalimu.

Mimi ndugu yenu nina shida na ninahitaji msaada wenu ili niweze kukabili hii hali inayonisumbua.

Tatizo langu ni kukata tamaa mapema, siwezi kupigania kitu nakipenda na kukihitaji na mpaka sasa naona nitapoteza mwelekeo.

Niko kwenye mahusiano na huyu mwanaume mwaka mmoja sasa, lakini huyu mwenzangu alianza kunikalia kimya ghafla, hajibu ujumbe kwa wakati au anaweza asijibu kabisa na akipiga simu anajambo anataka nimsaidie, nikajua pengine ubize wa kazi lakini hali ikaendelea kama mwezi, nilipomuuliza akanijibu kuwa hakujua kama kwa kufanya hivyo " ananikera."

Nikatafakari na kumuuliza kama kuna chochote nimekosea akasema hakuna, sasa nimeamua kujiongeza tu kuwa hapa hamna kitu na bahati mbaya sana akiwa na shida ndio ananitafuta.

Mtaniwia radhi kwa uandishi lakini Ushauri na msaada wenu unahitajika kwa haraka, natanguliza shukrani.
 
Huna tatizo...wew ni aina ya watu (introvert) ambao hawana ile hali ya kujikomba komba/kujipendekeza...

Cha kufanya jipende wew mwenyewe kwanza hao wanaoignore upendo wako watakuja kukupenda badae wao wenyewe..

Nina hali kama ya kwako,huwa inanitokea sana na wote walio dharau upendo wngu uko nyuma weng wao wanajuta...wanatamani waupate sasa baada ya wao kuumizwa Ila nami nakuwa busy na mambo yangu.

Vipi lakin fursa bado ipo?
 
Asante kwa ushauri
 
Kigezo Cha kwanza kwenye mapenzi ni mawasiliano. Ukishagundua kuwa mwenza wako hatilii maanani suala la kuwasiliana na wewe ,hiyo ni taa nyekundu (ishara mbaya) katika mapenzi yenu.

Kama hauna namna nyingine yeyote ya kufanya komaa naye.
 
Back
Top Bottom