Nahitaji msaada wenu wa haraka

Wewe unaona na huyo mwanaume mnaendana?
KiElimu, Family Status na Financial Freedom?

Isije kuwa alikuja kwako kwa papuchi tu.
 
Nilijitahidi kufanya kwa upande wangu, kumpigia, kumtext, kumtembelea kwake na vizawadi.

Hiyo nguvu nyingi kunipata sijaelewa.. lakini imefikia hatua akinipigia ana shida na hapo atanichatisha na kunipigaia lakini ikiisha tu shida yake basi anarudi tena mbali.

Najitahidi kumpigia na kumtext lakini ndio inakuwa ya upande mmoja zaidi.

Nashukuru kwa ushauri wako
Hapa ndiyo penye tatizo. Kama unaamini ndani ya moyo wako kwamba umejitahidi kumuonyesha penzi na badala
yake jamaa bado anakutenda hivyo, ni vyema ukaacha kuuchosha moyo wako. Acha kumbembeleza, mpe nafasi
"anayodhani" anaihitaji. Jilinde asikutumie, yaani acha kuendekeza shida zake. Asipojiongeza itabidi wewe ujiongeze usonge mbele na maisha.
 
Ndugu wanajamii, nawasalimu.

Mimi ndugu yenu nina shida na ninahitaji msaada wenu ili niweze kukabili hii hali inayonisumbua.

Tatizo langu ni kukata tamaa mapema, siwezi kupigania kitu nakipenda na kukihitaji na mpaka sasa naona nitapoteza mwelekeo.

Niko kwenye mahusiano na huyu mwanaume mwaka mmoja sasa, lakini huyu mwenzangu alianza kunikalia kimya ghafla, hajibu ujumbe kwa wakati au anaweza asijibu kabisa na akipiga simu anajambo anataka nimsaidie, nikajua pengine ubize wa kazi lakini hali ikaendelea kama mwezi, nilipomuuliza akanijibu kuwa hakujua kama kwa kufanya hivyo " ananikera."

Nikatafakari na kumuuliza kama kuna chochote nimekosea akasema hakuna, sasa nimeamua kujiongeza tu kuwa hapa hamna kitu na bahati mbaya sana akiwa na shida ndio ananitafuta.

Mtaniwia radhi kwa uandishi lakini Ushauri na msaada wenu unahitajika kwa haraka, natanguliza shukrani.

Kabla ya kukushauri ni bora ujibu haya maswali:

1. Una miaka mingapi?
2. Huyu ni mchumba? Au mnakulana tu?
3. Una msupport financial?
4. Wewe Una Kazi?
5. Yeye Ana Kazi?

Ukijibu hayo maswali kwa ukweli ninaweza kukushauri vizuri sana, Kama hutaki kuyajibu then ushauri wangu;

“Achana na huyo mtu, Ganga moyo wako, achana na kufukuzia mahusiano, yatakuja yenyewe”
 
Huna tatizo...wew ni aina ya watu (introvert) ambao hawana ile hali ya kujikomba komba/kujipendekeza...

Cha kufanya jipende wew mwenyewe kwanza hao wanaoignore upendo wako watakuja kukupenda badae wao wenyewe..

Nina hali kama ya kwako,huwa inanitokea sana na wote walio dharau upendo wngu uko nyuma weng wao wanajuta...wanatamani waupate sasa baada ya wao kuumizwa Ila nami nakuwa busy na mambo yangu.

Vipi lakin fursa bado ipo?
Naona unavutia kwako
 
Ndugu wanajamii, nawasalimu.

Mimi ndugu yenu nina shida na ninahitaji msaada wenu ili niweze kukabili hii hali inayonisumbua.

Tatizo langu ni kukata tamaa mapema, siwezi kupigania kitu nakipenda na kukihitaji na mpaka sasa naona nitapoteza mwelekeo.

Niko kwenye mahusiano na huyu mwanaume mwaka mmoja sasa, lakini huyu mwenzangu alianza kunikalia kimya ghafla, hajibu ujumbe kwa wakati au anaweza asijibu kabisa na akipiga simu anajambo anataka nimsaidie, nikajua pengine ubize wa kazi lakini hali ikaendelea kama mwezi, nilipomuuliza akanijibu kuwa hakujua kama kwa kufanya hivyo " ananikera."

Nikatafakari na kumuuliza kama kuna chochote nimekosea akasema hakuna, sasa nimeamua kujiongeza tu kuwa hapa hamna kitu na bahati mbaya sana akiwa na shida ndio ananitafuta.

Mtaniwia radhi kwa uandishi lakini Ushauri na msaada wenu unahitajika kwa haraka, natanguliza shukrani.
Apo tumesikiliza upande wako tu bado kwa huyo mwamba nae hawezi kosa neno...Kama kawaida wanawake hua mnalalamika Sana kuhisi hatuwafanyii mazuri Yani kosa moja litafunika mazuri yote.

Yawezekana unayafanya kikamilifu hayo uliyosema Apo ila utakua na mapungufu/tabia zako ambazo zinafanya uone mwamba kabadilika na inawezekana kabisa ashakwambia hataki 1,2,3 lakin umekua sikio la kufa.

Mawasiliano Ndio nguzo ya mahusiano ila binafsi nakereka na sim za kila mda ambazo si za lazima na kutuma msg kila wakati ukitegemea nitakujibu hell no. ..! Hua mnalalamika kua mbona kipind tunawafukuzia au mwanzo wa mahusiano hua tunakua tuko active Sana..? Na Yale mazoea ya jinsi mlivokua mnawasiliana yakipungua kdgo mna Anza kuona Kama tumebadilika .Jibu Ni ndio hua tunakua active ili tuwanase vizuri hata Research inatumiaga mda na gharama akili pia...Na tukishazoeana Yale mapenzi ya Moto yanaishaga kinachobaki Ni bond ya nyakati zenu tu.
 
Kwa iyo akiwa na shida ya kunyandua tu ndio anakutafuta aisee pole sanaa cha muhimu kaa nae ongea nae kwa undani akueleze tatizo nini na kama ana mtu mwingine akueleze ukweli tu hata kama itakuuma ila ukweli utakuwa ushajua
Nashukuru
 
Kabla ya kukushauri ni bora ujibu haya maswali:

1. Una miaka mingapi?
2. Huyu ni mchumba? Au mnakulana tu?
3. Una msupport financial?
4. Wewe Una Kazi?
5. Yeye Ana Kazi?

Ukijibu hayo maswali kwa ukweli ninaweza kukushauri vizuri sana, Kama hutaki kuyajibu then ushauri wangu;

“Achana na huyo mtu, Ganga moyo wako, achana na kufukuzia mahusiano, yatakuja yenyewe”
1. Umri late 20's
2. Sio mchumba
3. Hapana, simsupport wala hanisupport
4 & 5. Wote tuna kazi

Nashukuru nitazingatia.
 
Hapa ndiyo penye tatizo. Kama unaamini ndani ya moyo wako kwamba umejitahidi kumuonyesha penzi na badala
yake jamaa bado anakutenda hivyo, ni vyema ukaacha kuuchosha moyo wako. Acha kumbembeleza, mpe nafasi
"anayodhani" anaihitaji. Jilinde asikutumie, yaani acha kuendekeza shida zake. Asipojiongeza itabidi wewe ujiongeze usonge mbele na maisha.
Asante kwa ushauri
 
Wewe unaona na huyo mwanaume mnaendana?
KiElimu, Family Status na Financial Freedom?

Isije kuwa alikuja kwako kwa papuchi tu.
Kanizidi elimu, family status hatujazidiana sana(kwa mujibu wa maelezo yake maana sijawahi kuonana nao), financially sina hakika sana hakuwa ananiambia vingi kuhusu uchumi wake.
 
Apo tumesikiliza upande wako tu bado kwa huyo mwamba nae hawezi kosa neno...Kama kawaida wanawake hua mnalalamika Sana kuhisi hatuwafanyii mazuri Yani kosa moja litafunika mazuri yote.
Nashukuru lakini tulikuwa tunawasiliana sana asubuhi kabla ya kazi na jioni baada ya kazi.. hapa katikati labda kuwepo na kitu cha lazima na hii ni kutokana na nature ya majukumu yetu.

Walau yangepungua kidogo ila ni yamepungua sana na hata ikitokea tuko mazingira ya pamoja hatuonani tena kama mwanzo bila sababu yoyote.

Hajawahi kuniambia kuwa kitu hiki nikiache hakipendi, labda kama kuna kitu na hakuwa ameniambia japo nilimuuliza na hakusema kama nimemkosea kwa chochote.
 
Back
Top Bottom