Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Zinauzwa kuanzia 12,000-15,000,
Skuhz Zinauzwa sehem chache SANA,

Mara nyingi zinatumika kupaua wide roofs kama kumbi,makanisa na misikiti.
(Wengine wanaozihitaji uziagiza Kama special order)

Kwa nyumba za kuishi uwa hazitumiki( paa linakua zito mno,inaweza sababusha nyufa)

LABDA uzitumie TU kupigia mahesabu ya kupata 2×4 na 2×2 kama nilivofanya pale juu
Ahsante.
Fundi ameniambia nahitaj Bati 70 na mbao 70 samahani naomba unisaidie hapo mbao za 2× 4 zitakua ngapi?
 
Jitahidi kuchagua mti mzuri wa mbao unapokwenda kuchagua mbao za kupaulia nyumba Yako.

Sokoni zipo aina 3 common za mbao:-

1. Ukichagua mti WA MLINGOTI,
Jitahidi ununue ambazo hazijakauka Sana na saiti zisikae Sana bila kupauliwa, Huwa zinatabia ya kupinda zikipigwa jua.

Pia hazifai Kwa nyumba yenye Kuta dhaifu, inasababisha nyufa sababu ya paa kua zito Sana..

Uzuri wake: Zinahimili Sana mchwa Hata kama umenunua ambazo hazijatibiwa.

2. Ukichagua mti WA Cyprus,
Jitahidi upate ambazo zimetibiwa, hizi zinaliwa na mchwa Balaa.
Ikishindikana, zipakae oil chafu, inasaidia zidumu MDA mrefu.

Uzuri wa hizi
-hazipindi hovyo Hata zikipigwa na jua
-paa linakua jepesi, Hata kama Kuta ni dhaifu. (Zinafaa kwenye maghorofa,nyumba zenye misingi dhaifu, nyumba zilizojengwa kwenye udongo mfinyanzi)

3. Ukichagua mti wa msufi,
Jitahidi upate za msufi pori uliokomaa vzur, mbao changa inamung'unyika kama biskuti na Ni rahisi Sana kupekechwa na mchwa kuliko ata Cyprus.
Changamoto yake ni, hautaki maji, kitobo kimoja TU cha msumari unaovuja kinaweza sababisha mbao yote ikakatika katikati.
Hakikisha nyumba Yako haivuji Hata kitobo kimoja baada ya kupauliwa.

4. Ukipata mbao ya mnazi uliokomaa, vizuri utaenjoy, ni miaka buku, hamna mchwa wala kupinda.

5. Jitahidi usije kuuziwa mbao ya mwembe, hasa kama haujatibiwa.Utajuta.

Mti Bora sana Kwa kupaua Kama huna ela ya mawazo ni MVULE[emoji4][emoji106]
Mbao yq mkaratusi vipi?
 
Hapana,
Unatafuta eneo la Kila square ya nyumba yako, afu unajumlisha skwea zote kwa pamoja.

Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1

[emoji117]Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi

[emoji117]Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi

[emoji117]Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi

[emoji117]Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi

[emoji117]Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi

[emoji117]Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi

Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi

Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.

Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144

YAANI, 809÷144= 5.62

Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.

Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.
Lakini bati hazilingani upana? Zip zeny 75,81, 91 had 110cmt hapo vip msaada?
 
Unaponunua mbao za fisherbodi

pia jitahidi uchague fisherbodi Pana (width) Kama utazipiga kabla ya kupangisha bati.
(Standard ni nchi 12, zimefeli Sana ni nchi 10)

Nb: zikiwa fupi Sana (chini ya nchi 10), Huwa zinatabia ya kufunikwa na bati, hazionekani, hasa Kwa wenye mapaa yenye slope kubwa sana.

Inaweza kukusabishia ukalazimika kuunganisha fisherbodi mbili mbili
Ili kufosi fisherbodi zako zionekane zipendezeshe nyumba.
Mwambaaa hongeraa Sana hii mada imenikuta mahili husika kwa wakati sahihi yaani umenisaidia mnoooo boss wangu, ubalikiwe Sana mkuuu
 
Mkuu DeepPond Nyumba yenye mzunguko wa mita 60, yaani hii ni jumla ya kuta zote. Itahitaji bati ngapi na mbao ngapi kwa ujumla?
 
Back
Top Bottom