Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Itategemea unanunua bati ya aina gani mkuu, ukinunua zile zinazorange 30,000 kushuka had 20,000 haifiki ata 3milion

Ukinunua ALAF, Tena zile zile za vigae vigae au chenga chenga , jiandae kisaikolojia
ALAF ndo wanafanya watu wakate tamaa kujenga. bati la kigae wanauza 84, 000 (meter 3) YAAANI meter moja kwa 28,000.. sasa nyumba inakula bati meters 300 🤣... seka lile bati likikaa apo juu ni unyama sana
 
Itategemea unanunua bati ya aina gani mkuu, ukinunua zile zinazorange 30,000 kushuka had 20,000 haifiki ata 3milion

Ukinunua ALAF, Tena zile zile za vigae vigae au chenga chenga , jiandae kisaikolojia
Hivi Lile bati la ALAF ilo kigae chenga kwa nini hawana ya mgongo mpana .. kama haya makampun mengine yalivo nachenga chenga za muundo wa mgongo mpaka
 
Ili kupata tathmini nzuri ya kilo za misumari (nchi 4 au nchi 5) ya kugongea mbao zote za kwenye paa lako.

Chukua idadi ya bati zote zinazohitajika kwenye nyumba Yako, gawanya Kwa 2, JIBU UTAKALOPATA ndio utakua kilo za misumari inayohitajika kugongea paa lako lote la nyumba.

Mfano:
-nyumba ya bati 100, inahitaji kilo 50 za misumari ya kugongea mbao.
Je nyumba ya bando nane inahitaji misumari kiasi na mbao kiasi gani?
 
Boss deeppond nataka kujua uzoefu wako kwenye bati za chenga chenga kama zinapauka maan sijawahi ona sehemu imepauka ata kama kwnye campuni izi ndogo
 
Boss deeppond nataka kujua uzoefu wako kwenye bati za chenga chenga kama zinapauka maan sijawahi ona sehemu imepauka ata kama kwnye campuni izi ndogo
Hizo sjawai kuziuza Wala kutumia, ebu ntawauliza wazoefu afu ntakupa mrejesho
 
Jitahidi kuchagua mti mzuri wa mbao unapokwenda kuchagua mbao za kupaulia nyumba Yako.

Sokoni zipo aina 3 common za mbao:-

1. Ukichagua mti WA MLINGOTI,
Jitahidi ununue ambazo hazijakauka Sana na saiti zisikae Sana bila kupauliwa, Huwa zinatabia ya kupinda zikipigwa jua.

Pia hazifai Kwa nyumba yenye Kuta dhaifu, inasababisha nyufa sababu ya paa kua zito Sana..

Uzuri wake: Zinahimili Sana mchwa Hata kama umenunua ambazo hazijatibiwa.

2. Ukichagua mti WA Cyprus,
Jitahidi upate ambazo zimetibiwa, hizi zinaliwa na mchwa Balaa.
Ikishindikana, zipakae oil chafu, inasaidia zidumu MDA mrefu.

Uzuri wa hizi
-hazipindi hovyo Hata zikipigwa na jua
-paa linakua jepesi, Hata kama Kuta ni dhaifu. (Zinafaa kwenye maghorofa,nyumba zenye misingi dhaifu, nyumba zilizojengwa kwenye udongo mfinyanzi)

3. Ukichagua mti wa msufi,
Jitahidi upate za msufi pori uliokomaa vzur, mbao changa inamung'unyika kama biskuti na Ni rahisi Sana kupekechwa na mchwa kuliko ata Cyprus.
Changamoto yake ni, hautaki maji, kitobo kimoja TU cha msumari unaovuja kinaweza sababisha mbao yote ikakatika katikati.
Hakikisha nyumba Yako haivuji Hata kitobo kimoja baada ya kupauliwa.

4. Ukipata mbao ya mnazi uliokomaa, vizuri utaenjoy, ni miaka buku, hamna mchwa wala kupinda.

5. Jitahidi usije kuuziwa mbao ya mwembe, hasa kama haujatibiwa.Utajuta.

Mti Bora sana Kwa kupaua Kama huna ela ya mawazo ni MVULE😊👍
👍
 
Mkuu DeepPond nina swali muhimu sana naomba jibu.
Ukiachilia mbali habari za kupauka kwa rangi, tuje kwenye uimara.
Hivi bati Geji 30 ya kampuni A inaweza kuwa na utofauti katika uimara na Geji 30 ya kampuni B ? Au tuseme Geji 30 ya Alaf ina utofauti katika uimara na Geji 30 ya Kiboko? Au kwa kuwa zote ni Geji 30 uimara unfanana?
Nasisitiza tena tusigusie habari za rangi kupauka.
 
Hapana,
Unatafuta eneo la Kila square ya nyumba yako, afu unajumlisha skwea zote kwa pamoja.

Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1

👉Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi

👉Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi

👉Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi

👉Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi

👉Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi

👉Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi

Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi

Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.

Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144

YAANI, 809÷144= 5.62

Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.

Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.
Asante
 
Ili kuifanya nyumba Yako iwe na mwonekano mzuri wa slope.

YAANI isiwe na slope kubwa sana au isiwe na slope ndogo Sana.

Chukua eneo lote la nyumba Yako, ligawanye Katika skwea (mistatiri na miraba) mbalimbali mikubwa Kadri iwezekanavyo.

Chukua skwea kubwa (mraba mkubwa) kuliko yote.

Huo ndo utaamua kingPOST Yako (paa kuu) liwe na urefu kiasi gani.

Chukua upana WA huo mraba wako, ugawanye Mara 2, urefu utakapotikana ndio utakua urefu WA king post Yako.

Mfano:
Nyumba yenye paa kuu lenye urefu WA MITA 16 na upana wa MITA 8

kingPOST yake inapaswa kua MITA 4 kwenda juu.

Zingatia: kingPOST ikiwa mbaya, itaathiri mwonekano wote wa mapaa yanayofuata, maana mapaa yote madogo lazima yatakua yanamegwa kutoka kwenye kingpost kuu
Mkuu ,nyumba ikiwa na vipimo vya 15m kwa 14.6m hapo kingpost itapaswa iwe ngapi kwa slope standard.Sijaelewa vizuri ile ya kugawanya vyumba.
 
Back
Top Bottom