Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Unaponunua mbao za fisherbodi

pia jitahidi uchague fisherbodi Pana (width) Kama utazipiga kabla ya kupangisha bati.
(Standard ni nchi 12, zimefeli Sana ni nchi 10)

Nb: zikiwa fupi Sana (chini ya nchi 10), Huwa zinatabia ya kufunikwa na bati, hazionekani, hasa Kwa wenye mapaa yenye slope kubwa sana.

Inaweza kukusabishia ukalazimika kuunganisha fisherbodi mbili mbili
Ili kufosi fisherbodi zako zionekane zipendezeshe nyumba.
 
Ili kuifanya nyumba Yako iwe na mwonekano mzuri wa slope.

YAANI isiwe na slope kubwa sana au isiwe na slope ndogo Sana.

Chukua eneo lote la nyumba Yako, ligawanye Katika skwea (mistatiri na miraba) mbalimbali mikubwa Kadri iwezekanavyo.

Chukua skwea kubwa (mraba mkubwa) kuliko yote.

Huo ndo utaamua kingPOST Yako (paa kuu) liwe na urefu kiasi gani.

Chukua upana WA huo mraba wako, ugawanye Mara 2, urefu utakapotikana ndio utakua urefu WA king post Yako.

Mfano:
Nyumba yenye paa kuu lenye urefu WA MITA 16 na upana wa MITA 8

kingPOST yake inapaswa kua MITA 4 kwenda juu.

Zingatia: kingPOST ikiwa mbaya, itaathiri mwonekano wote wa mapaa yanayofuata, maana mapaa yote madogo lazima yatakua yanamegwa kutoka kwenye kingpost kuu
 
Ushauri wa ziada:
Kama huna Ela ya mawazo,

Ni vema ukaanza kupiga kenchi na rati kabla ya kupiga bati.

Hii itakusaidia kuweza kununua zile bati za kupima kwa urefu WA MITA kiwandani.

Hizi bati zinazotoka juu Hadi chini, uwa zinaepusha kukata kata mabati ovyo saiti.
 
Ukishamaliza kupaua,
Zile mbao zinazobaki, usizigawe au kuziuza.

Huwa zinasaidia Sana wakati WA blandaring, (utaongezea nyingine kidogo TU)

Au mwongeze ela fundi ili akupgie kabisa blandaring ya nje (Ile ya kuzuia popo wasiingie kwenye paa.

Au
Zihifadhi vizuri ili zisiibiwe juu ya Dari la nyumba Yako.

Ukifika wakati wa blandaringi, unakwea unazitoa na kuzitumia Tena.
 
Mkuu weka na bei aiseh
Kwa bati ya geji 30, futi 10

NABAKI uwa wanacheza kuanzia elfu 60 Hadi 65 Kwa bati pc 1

ALAF wanacheza kuanzia elfu 40 Hadi elfu 50 Kwa bati pc 1

Dragon, sunshare, kinglion wanacheza elfu 25-30 Kwa pc

Kiboko ,batibomba na nyingine za kichina ni kuanzia elfu 20 Kwa pc
 
Unapokwenda kununua mbao,
Jitahidi uende na tepu Yako. Bei yake haizidi elfu 5

Wauzaji WA mbao wengi Sio waaminifu.

Wanakua na tepu zao zilizochakachuliwa.

Utauziwa mbao fupi Kwa Bei sawa na na Bei ya mbao Ndefu.

Ikumbukwe,
Ukinunua mbao fupi chini ya urefu WA futi 12, utakua nje ya tathimini ya idadi ya mbao zinazohitajika nilizokutajia kule mwanzoni.
 
Jitahidi kuchagua mti mzuri wa mbao unapokwenda kuchagua mbao za kupaulia nyumba Yako.

Sokoni zipo aina 3 common za mbao:-

1. Ukichagua mti WA MLINGOTI,
Jitahidi ununue ambazo hazijakauka Sana na saiti zisikae Sana bila kupauliwa, Huwa zinatabia ya kupinda zikipigwa jua.

Pia hazifai Kwa nyumba yenye Kuta dhaifu, inasababisha nyufa sababu ya paa kua zito Sana..

Uzuri wake: Zinahimili Sana mchwa Hata kama umenunua ambazo hazijatibiwa.

2. Ukichagua mti WA Cyprus,
Jitahidi upate ambazo zimetibiwa, hizi zinaliwa na mchwa Balaa.
Ikishindikana, zipakae oil chafu, inasaidia zidumu MDA mrefu.

Uzuri wa hizi
-hazipindi hovyo Hata zikipigwa na jua
-paa linakua jepesi, Hata kama Kuta ni dhaifu. (Zinafaa kwenye maghorofa,nyumba zenye misingi dhaifu, nyumba zilizojengwa kwenye udongo mfinyanzi)

3. Ukichagua mti wa msufi,
Jitahidi upate za msufi pori uliokomaa vzur, mbao changa inamung'unyika kama biskuti na Ni rahisi Sana kupekechwa na mchwa kuliko ata Cyprus.
Changamoto yake ni, hautaki maji, kitobo kimoja TU cha msumari unaovuja kinaweza sababisha mbao yote ikakatika katikati.
Hakikisha nyumba Yako haivuji Hata kitobo kimoja baada ya kupauliwa.

4. Ukipata mbao ya mnazi uliokomaa, vizuri utaenjoy, ni miaka buku, hamna mchwa wala kupinda.

5. Jitahidi usije kuuziwa mbao ya mwembe, hasa kama haujatibiwa.Utajuta.

Mti Bora sana Kwa kupaua Kama huna ela ya mawazo ni MVULE😊👍
 
Unapokwenda kununua mbao,
Jitahidi uende na tepu Yako. Bei yake haizidi elfu 5

Wauzaji WA mbao wengi Sio waaminifu.

Wanakua na tepu zao zilizochakachuliwa.

Utauziwa mbao fupi Kwa Bei sawa na na Bei ya mbao Ndefu.

Ikumbukwe,
Ukinunua mbao fupi chini ya urefu WA futi 12, utakua nje ya tathimini ya idadi ya mbao zinazohitajika nilizokutajia kule mwanzoni.
Mkuu DeepPond nina swali sijui kama litaeleweka.
Mfano una ramani ya nyumba yako nzima, ukaamua kujenga kwanza nusu yaani upande wa mbele (sebule, chumba na dining) kama nilivyokata na mstari wa blue hapo kwenye picha.
Je inawezekana kuezeka hiyo nusu kwa lengo lako lile lile la muonekano wa paa ili uje umalizie badae utakapokuwa umekamilisha jengo? Au ni lazima uezeke slope kwanza ili jengo likishakamilika ufumue uezeke upya?

Au kwa maneno mengine chukulia hiyo nyumba ingejengwa nusu kama mstari wa blue unavyoonesha, je ingeweza kupauliwa hivyo hivyo nusu upande huo wa mbele na kuja kumalizia badae upande wa nyuma pindi jengo likikamilika?

Sababu ni kwamba nina nyumba nimejenga hivyo lakini sitaki kuezeka slope ili badae nije nifumue pia muonekano mbaya wa slope.
 
Attachments

  • IMG_20250407_011959.jpg
    IMG_20250407_011959.jpg
    162.3 KB · Views: 37
Kujenga slope ni hasara, PATA fundi mzuri, Funika kutokana na ramani Yako Ila kiwe kinusu, gepu linalobaki unaweza kuamua kupandisha ukuta kabisa kuziba (linaitwa gebo) , au ukafunika na bati reject kuzuia mvua ya upepo n maji kuingia ndani.

Ila hakikisha unaacha matoleo ya mbao na tofali za Kuta ili kukurahisishia siku umeamua kuendeleza ujenzi.
Mkuu DeepPond nina swali sijui kama litaeleweka.
Mfano una ramani ya nyumba yako nzima, ukaamua kujenga kwanza nusu yaani upande wa mbele (sebule, chumba na dining) kama nilivyokata na mstari wa blue hapo kwenye picha.
Je inawezekana kuezeka hiyo nusu kwa lengo lako lile lile la muonekano wa paa ili uje umalizie badae utakapokuwa umekamilisha jengo? Au ni lazima uezeke slope kwanza ili jengo likishakamilika ufumue uezeke upya?

Au kwa maneno mengine chukulia hiyo nyumba ingejengwa nusu kama mstari wa blue unavyoonesha, je ingeweza kupauliwa hivyo hivyo nusu upande huo wa mbele na kuja kumalizia badae upande wa nyuma pindi jengo likikamilika?

Sababu ni kwamba nina nyumba nimejenga hivyo lakini sitaki kuezeka slope ili badae nije nifumue pia muonekano mbaya wa slope.
 
Ushauri wa ziada:

Kama una pesa, nunua mwenyewe dawa ya kutibu mbao au oilchafu ichanganye na brake fluid kidg (dot4)

kisha mwite kijana,mpe pesa kidogo azitibu mwenyewe mbao zako ukiwepo.

Skuhz Wajanja wengi sana apa mjini,

Mbao zinazoitwa treated zinapakwa Sana juicecola badala ya dawa
 
Kujenga slope ni hasara, PATA fundi mzuri, Funika kutokana na ramani Yako Ila kiwe kinusu, gepu linalobaki unaweza kuamua kupandisha ukuta kabisa kuziba (linaitwa gebo) , au ukafunika na bati reject kuzuia mvua ya upepo n maji kuingia ndani.

Ila hakikisha unaacha matoleo ya mbao na tofali za Kuta ili kukurahisishia siku umeamua kuendeleza ujenzi.
Mkuu

[/QUO

Mkuu asante sana. Nilifikiri haiwezekani , hapo naona mipango yangu itaenda vizuri sasa.
 
Fundi nipo hapa wa kupauw ikikupendeza nitafute kwa mawasiliano zaidi
Fundi soma coment #30 useme kama hiyo kazi unaiweza. Elezea utaifanyaje ili nishawishike kukutafuta. Ukitupia kama picha mbili za kazi zako pia sio mbaya.
 
Kampuni ya NABAKI africa Iko POA Sana (NABAKI wanamfunika hadi ALAF)

, pia DRAGON wanajitahidi. (Dragon ni mzuri Sana kuliko kiboko)

Kiboko Yuko levo Moja na kina sunshare, kinglion na sunshine.
Mkuu nimependa uchambuzi wako, naomba unifahamishe hizi bati za kuagiza china moja kwa moja zipo vizuri au ni sawa na hizi za kichina zinazouzwa bongo
 
Kampuni ya NABAKI africa Iko POA Sana (NABAKI wanamfunika hadi ALAF)

, pia DRAGON wanajitahidi. (Dragon ni mzuri Sana kuliko kiboko)

Kiboko Yuko levo Moja na kina sunshare, kinglion na sunshine.
mkuu vipi kati kiboko na dragon ipi yenye bei kubwa?
 
Bati za kuagiza china ni Kama kubeti, ukipata supllier mwaminifu, ni nzuri, Ila ukipata kanjanja, imekula kwako
Mkuu nimependa uchambuzi wako, naomba unifahamishe hizi bati za kuagiza china moja kwa moja zipo vizuri au ni sawa na hizi za kichina zinazouzwa bongo
 
Back
Top Bottom