Katika kupima futi hapo kwenye kupima nyumba unahesabu Kwa mizunguko mzima kma najua Kwa upana na urefu maana yake najumlisha futi za urefu na upana?
Hapana,
Unatafuta eneo la Kila square ya nyumba yako, afu unajumlisha skwea zote kwa pamoja.
Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1
👉Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi
👉Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi
👉Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi
👉Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi
👉Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi
👉Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi
Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi
Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.
Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144
YAANI, 809÷144= 5.62
Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.
Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.