Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

Unaweza kujiuliza,
Kwanini tunagawanya eneo (square) ya nyumba Kwa 144(kama tulipimia futi) na 16 (Kama tulipimia MITA), Kisha mwishoni tunazidisha Kwa 12?

Jibu ni kwamba,
👉Huwa tunagawanya Kwa 144 sqft au 16sqm kwaSababu tunajaribu kuigawanya nyumba nzima Katika vyumba Vidogo vdg vya futi 12×12 au MITA 4×4 .
🙏
 
Unaweza kujiuliza pia,
Kwanini Sasa huwa tunazidisha Kwa 12?

Jibu ni kwamba,
Standard bati moja Huwa Lina urefu WA futi 3×3.5

Kwahiyo li uweze kupaua chumba kimoja cha kulala chenye MITA 4×4 (futi 12×12) Kwa style ya paa linalomwaga Mara 4 Kwa slope ya bati yenye nyuzi 45°.

Utahitajika kuandaa bati 12.

Hivyo ili upate hesabu nzur lazima uzidishe hesabu ya Kila chumba Kwa bati 12 kupata bati zote za nyumba Yako.🙏
 
Mkuu nahitaji kupaua nyumba yangu kwa kampuni ya Dragron vipi kwa uzoefu wako ni bati isiyopauka?

Maana mtu wao wa mauzo amenishawishi sana, naogopa kuingia chaka.
MKUU, kumradhi nitoe uzoefu wang kdg apa, nmeingilia comment ya mtu🙏

Dragon nmeiskia Sana ila nmeitumia mwaka huu tu, YAANI Mara Moja.

Tena niliinunua bati 43 Kwa mtu Kwa Bei chee Sana mwaka jana mwezi Kama huu (nilimlalia Sana Bei),

Ni alipaulia kwake zikabaki, akaleta dukan kwangu tufanye exchange nimpatie material za finishing.

Nilivozishika TU kuzikagua,aisee ule ugumu wake ulinishawishi, nikatafta kujua ni kampuni gani hii, ndo nikakuta imeandikwa DRAGON, nikakubali ni bati imara kias chake.

Nilizipeleka saiti Moja Kwa Moja kuzitest, na mwaka huu nmezipaulia vyumba viwili self vya kupangisha na vimesha kamilika mwezi march mwaka huu. Wapangaji washahamia.

Kuhusu kupauka Kwa rangi,sijajua.

Ila nnachojua, Kila bati uwa inapauka rangi,Ila ALAF ndo zinachelewa zaidi.

Hebu Ngoja nizichunguze zaidi angalau Kwa miaka 2, naweza kupata majibu

Ila humu naamini wapo waliokwishazitumia kitambo, wanaweza kuleta majibu zaidi🙏
 
Attachments

  • download-2.jpeg
    download-2.jpeg
    12.9 KB · Views: 45
Hapana,
Unatafuta eneo la Kila square ya nyumba yako, afu unajumlisha skwea zote kwa pamoja.

Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1

👉Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi

👉Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi

👉Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi

👉Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi

👉Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi

👉Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi

Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi

Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.

Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144

YAANI, 809÷144= 5.62

Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.

Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.
😄😄Ngoja Nikinywa chai nitarudi aisee
 
MKUU, kumradhi nitoe uzoefu wang kdg apa, nmeingilia comment ya mtu🙏

Dragon nmeiskia Sana ila nmeitumia mwaka huu tu, YAANI Mara Moja.

Tena niliinunua bati 43 Kwa mtu Kwa Bei chee Sana mwaka jana mwezi Kama huu (nilimlalia Sana Bei),

Ni alipaulia kwake zikabaki, akaleta dukan kwangu tufanye exchange nimpatie material za finishing.

Nilivozishika TU kuzikagua,aisee ule ugumu wake ulinishawishi, nikatafta kujua ni kampuni gani hii, ndo nikakuta imeandikwa DRAGON, nikakubali ni bati imara kias chake.

Nilizipeleka saiti Moja Kwa Moja kuzitest, na mwaka huu nmezipaulia vyumba viwili self vya kupangisha na vimesha kamilika mwezi march mwaka huu. Wapangaji washahamia.

Kuhusu kupauka Kwa rangi,sijajua.

Ila nnachojua, Kila bati uwa inapauka rangi,Ila ALAF ndo zinachelewa zaidi.

Hebu Ngoja nizichunguze zaidi angalau Kwa miaka 2, naweza kupata majibu

Ila humu naamini wapo waliokwishazitumia kitambo, wanaweza kuleta majibu zaidi🙏
sawa mkuu
 
Mkuu Kuna Hawa jamaa wanaitwa Lodhia nafikiri kwa Dsm wako vikindu ni wahinidi ingawa Sina uhakika sana nao wanafyatua Bati zao.Nilijaribu kuwacheki wakaniambia nimcheki Kamaka ndio ajenti Mkuu.Je una uzoefu nao?
 
Ili kupata tahmini nzuri ya mbao zinazohitajika kupaua,

Idadi ya bati ndo Huwa idadi ya mbao kuu (2×8) inayohitajika kupaua nyumba husika.

Mfano:
Nyumba ya bati 100, utapaswa kuandaa mbao za (2×8) pc 100.

Hizo 2× 8
Ndo kila ubao utachanwa kutoa rati 4 za(2×2) au kenchi 2 za (2× 4)
Hivi hizi mbao za 2×8 zinauzwa kuanzia shilingi ngap?
Nimeulizia sehem kadhaa sion wa kiuza .
 
Hivi hizi mbao za 2×8 zinauzwa kuanzia shilingi ngap?
Nimeulizia sehem kadhaa sion wa kiuza .
Zinauzwa kuanzia 12,000-15,000,
Skuhz Zinauzwa sehem chache SANA,

Mara nyingi zinatumika kupaua wide roofs kama kumbi,makanisa na misikiti.
(Wengine wanaozihitaji uziagiza Kama special order)

Kwa nyumba za kuishi uwa hazitumiki( paa linakua zito mno,inaweza sababusha nyufa)

LABDA uzitumie TU kupigia mahesabu ya kupata 2×4 na 2×2 kama nilivofanya pale juu
 
Lodhia ni wazur kwenye Nondo,
Mkuu Kuna Hawa jamaa wanaitwa Lodhia nafikiri kwa Dsm wako vikindu ni wahinidi ingawa Sina uhakika sana nao wanafyatua Bati zao.Nilijaribu kuwacheki wakaniambia nimcheki Kamaka ndio ajenti Mkuu.Je una uzoefu nao?
kwenye bati ndo naskia leo
 
Back
Top Bottom