Nafsi imesahaulika. (a rant).

Utagundua hakuna miujiza, celebrity huzaliwa akiwa celebrity and thus hata kwenye Bible kuzaliwa kwa messiah tayari kulikuwa kumeshapangwa na hata nyota zika align
Unataka kusema hata mashoga walishajulikana watakuwa mashoga toka viunoni mwa baba zao?

Kumbe Mungu amempangia kila mmoja ataishi vipi hapa duniani? Sasa kwanini watu wanatafuta miujiza?
 
(not debating just leaving this here. Sijatumwa kupoteza muda na wasio amini)


1) Kosa la kwanza: Kufikiri wewe ni MUNGU. Hii ni shida yako personally wewe mleta uzi.


2) Kosa la pili: Kutaka kuwa sawa na MUNGU. The Devil's original sin. Mmefanana sana na baba yenu.

Kisa Masihi alipangwa kuja unafikiri na wewe umepangwa.

Hujapangwa na mtu bwana na kila unachofanya unafanya kwa maamuzi yako ya hiari na utawajibika na maamuzi yako.

Umepewa zawadi ya uhai, very rare opportunity when you think of how massive the universe is. Kama hutaki kuishi milele basi mtamalizana na aliyekupa pumzi siku ya mwisho.


3) Kosa la tatu: Kumkataa MUNGU/ YESU/Kweli. Consequently unakataa reality. Unakaa kubuni false reality yako kichwani kwako in other words: Delusional.

Yani unabunibuni tu unatujazia mabandiko tu ya ubunifu wa ki schizophrenic.

Wenzio tunamsikiliza YESU kwasababu ameonysha ana nguvu za kiungu. The creator himself.

Tunamsikiliza jamaa aliyekufa akarudi. Kwakuwa tunajua tutakufa, tunamsikiliza aliyeenda huko akarudi.

Tunamsikiliza aliyekuwepo kabla hajakuja na uthibitisho tunao maana alijiandika kabisa kabla hajaja kuwa atakuja. Inshort Tunamsikiliza jamaa aliye nje ya muda.

Tunamsikiliza jamaa aliyeuishi Upendo hata akafa kwaajili ya wasiostahili, sio kutuhubiria upendo nye nye halafu baadae tunakufumania una operate kwa frequency ya kapepo kachafu.


Sasa nyie mna nini tuwasikilize watu wenyewe mna personality disorders? ? ?


4) MUNGU wetu sio idea iliyobuka kichwani mwa Delusional God-wannabes,

MUNGU wetu sio story za vijiweni za Gilgamesh,

MUNGU wetu ni  KWELI.

MUNGU wetu ni FACT katika kila sekta.

Kaacha chata kila sekta. Ni wewe kuwa kiazi by choice.


5) Litmust test yangu ni YESU: kama hukubali YESU aliishi karne ya kwanza, alifanya miujiza,aliuawa, akafufuka siku ya tatu,

hatuwezi kukubaliana na chochote kile maana Litmus yangu inanionyesha uko na shida ya kutafuta na ku interprete data.

Utanipotezea muda na kuninyonya energy bure (typical demonic move) ndomana tumeagizwa kwa anayemkataa YESU, amsha.

Mfano mmoja wa shida ya ku interpret ni masimulizi ya gharika. Karibu kila jamii duniani ina story ya mafuriko kutokea na watu wote kufa na wachache kuokolewa na wanyama kwenye boti.

Nimesimulia baadhi hapa:

Mtu ana conclude kuwa hii inamaanisha simulizi la garika la Noa kwenye Biblia ni hadithi tu! !

Ndiposa sisi tunashindwa ku tolerate aina hii ya ukiazi tunaamsha na kwenda kijiji kingine.

Mtu aina hii hachelewi ku conclude kuwa masimulizi ya matetemeko ya ardhi katika jamii tofauti inathibitisha matetemeko ni hadithi. Energy ya ku deal na hii kichwa ndio hatuna!


6) Kosa la nne: Kufikiri unajua na hujui! ! ! ! Eti watu wanabishia dini na hawajui.

Wewe ndo hujui!

Ancient teachings ndo nini! ! Hizo teachings/knowledge zimetoka kwa nani! Na kwanini unawasikiliza?

Yani mtu akija miaka 100 ijayo akasoma mabandiko yako hapa akubali mambo unayoandika kwasababu ipi yani

Who are you? ? ?


7) Kosa la mwisho kwa leo ni kuwapa Hollywood nguvu wasiyonayo. Hollywood sio manabii. Wala hawana nguvu yoyote.

Hollywood ni kama wale jamaa wanaolipisha watu hela kuwawekea WhatsApp na Facebook kwenye simu.

Wanawalipisha watu kuwafundisha jinsi ya kufanya Facebook ads.

Wanalipisha watu kuwaprintia police report.

Inshort Hollywood is the Devil and his people taking advantage of your Ignorance.

Hollywood hawajatabiri chochote kila wanachotuonyesha kilishatolewa unabii kwenye Biblia: from robots to AI to rockets/ ma ballistic missiles to a world government to aliens.

Hata hizo agenda za magonjwa, depopulation, vita zilishaandikwa kwenye Biblia.

Hollywood hawana jipya kwa watoto wa Mungu.

(Pia jitahidini kutomuhusisha Mungu wetu na ujinga mnaofanya kwa hiari yenu. Mungu Hajapanga, Kawaona. Wajibikeni)


Hapa niache andiko linalotoa unabii juu ya robots/ AI, world government, worlwide digital ID, SpaceX's Falcon 9 / missiles. All in one. Mengine tafuta.

"Naye akafanya ishara kuu na za ajabu, hata kusababisha moto kushuka toka mbinguni kuja duniani watu wakiona waziwazi.

Kwa sababu ya zile ishara alizokuwa amepewa uwezo wa kuzifanya kwa niaba ya yule mnyama wa kwanza, akawadanganya watu walioishi duniani. Akawaamuru wasimamishe sanamu kwa heshima ya yule mnyama aliyekuwa amejeruhiwa kwa upanga lakini akaishi.

Akapewa uwezo wa kuipa pumzi ile sanamu ya yule mnyama wa kwanza, ili iweze kusema na kuwasababisha wale wote waliokataa kuiabudu hiyo sanamu kuuawa.

Pia alimlazimisha kila mmoja, mdogo na mkubwa, tajiri na maskini, mtu huru na mtumwa, atiwe chapa kwenye mkono wake wa kuume au kwenye paji la uso wake,


ili mtu yeyote asiweze kununua wala kuuza isipokuwa amekuwa na hiyo chapa, ambayo ni jina la huyo mnyama au tarakimu za jina lake.

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na ufahamu na ahesabu tarakimu za huyo mnyama, kwa maana ni tarakimu za kibinadamu. Tarakimu zake ni mia sita sitini na sita (666).

Ufunuo.13.12-18.NENO2025
 
Kwa sababu zote mode of operation ni moja.. Mwili hauwezi ku move bila mind.

Na mind inahitaji movement ili I make sense(even thought is movement)
Sijakuelewa kabsa unaposema habari za movement..
Mimi najua akili iko kwenye nafsi, na ndio maana akili aishikiki
 
Unataka kusema hata mashoga walishajulikana watakuwa mashoga toka viunoni mwa baba zao?
Hii ninakataa maana kuwa hivyo ni maamuzi binafsi kama unavyo amua kuvaa nguo gani leo, ila what I meant ni ile light ya ndani ambayo ina shine through celebrity.. Mfano labda jinsi sauti ya mtu inakuwa na ukubwa wa kumfanya awe msanii(mwanamuziki), labda muonekano wa mtu unafanya aje kuwa model, uwezo wa ku immaginate unafanya mtu awe mchoraji mzuri kama wa kina Piccasso, the list goes on
Kumbe Mungu amempangia kila mmoja ataishi vipi hapa duniani? Sasa kwanini watu wanatafuta miujiza?
Ndio, ila kwa kufuata vipawa nilivyo jaribu kuelezea hapo juu👆, miujiza ni ile kudhani imetokea bila sababu. Watu wanatafuta miujiza ni watumwa wa kutaka wasicho nacho
 
Sijakuelewa kabsa unaposema habari za movement..
Mimi najua akili iko kwenye nafsi, na ndio maana akili aishikiki
Hapana mkuu akili na mawazo ni kitu kimoja na ni matokeo ya movement ya celi na neva za ubongo
 
not debating just leaving this here. Sijatumwa kupoteza muda na wasio amini)
No one si debating wewe mbona huwa unakuja na gia za kujistukia?

Kwanza mpaka hapo wewe ndo huna akili

Baada ya kuleta validity ya kile kilicho mezani umeanza kukosa without knowing the truth of what you're defending

Kama imani yako unayo dhani ni kweli inakufunza kuwa mnyenyekevu mbona unakuwa mshamba kuleta mapovu na ya kijinga bila kuwa na real tangible information..

Huyo yesu ni nani? Na je Unajuaje yeye ndo Mungu halisi?

Before Christianity miaka ya nyuma huko mbona yesu na Mungu wake wa adamu haonekani?

Kumbe bado hujakuwa kifikra bwana. Ulipaswa usije na hiyo negative energy..

Ungejua na madai valid katoa thesis zenye mpangilio sio kusingizia ujinga wa mental illness wakati simu unayoitumia na chemical za dawa unazo kunywa zimetokana na kistudy hizi laws ambazo nimejaribu kuelezea kwa ufupi

Wewe ndo huna fluidity ya kujifunza zaidi unaishia kumhasi huyo Mungu kwa matusi yasiyo na kichwa wala miguu..
Who are you? ? ?
Ngoja ni kujibu kwa kukuumiza zaidi I maana hunapa kutokea

I AM A GOD 😎
In short we jamaa ni huna utambuzi wala akili timamu..

Unaita schizophrenia waliotengeneza simu unayoitumia leo kutype haya maandishi? Walitumia God's language na kui replicate mpaka Waka gundua radio waves na mpaka leo unawashwa wifi kwenye simu yako

Unawaita wajinga?

You are so dumb, na wewe umetengeneza nini na huyo yesu wako, Mwana wa adamu mwenye uwezo na utambuzi wa kila jambo?

Stop being dramatic na kuleta mihemko, kama unaona bandiko hukiwezi usilete trauma na existential pain kwetu.
 
Kwa hakika tumefika Kwa sababu ya mapokezi ya Imani za kigeni na kuacha asili yetu. Huo ndo ulikuwa mwanzo wa Utumwa ambao mpaka sasa tumetekwa.
Walihakikisha wanateka nyanja kuu ambazo ni Spirit and Soul baada ya hapo mind and body zikafuata na ndo hicho kinaendelea hapa.
Imani za kigeni zilikuja Kwa lengo la kutuweka gizani na kutufanya kuwa watumwa.
Waafrika walio wengi, wamepumbazika baada ya kutojua uelekeo wao. Wanafuata na kuamini kila kitu cha kigeni pasipo kuhoji.
Tupo ndani ya Giza nene.
Ili kuondokana na Giza Hilo inatupasa sasa kuruhusu NURU sahihi kutoka kwenye chanzo chetu, Kisha hekima, busara na maamuzi yaliyo sahihi yataanza kujitokeza.
Bila kuruhusu NURU sahihi, basi tunaenda kuwa mazezeta.
 
Kuna Movie Moja inaitwa Atlas kaigiza JLo.Ile Movie inajaribu kufungua kwa kiasi nini kitatokea sikuzijazo kwenye hizi mambo za AI...

Kuna wakati AI zitataka kumiliki mwili na kuwa na utambulisho rasmi(Kutambulika) na hapo ndo balaa litaanza.
 
Kuna Movie Moja inaitwa Atlas kaigiza JLo.Ile Movie inajaribu kufungua kwa kiasi nini kitatokea sikuzijazo kwenye hizi mambo za AI...

Kuna wakati AI zitataka kumiliki mwili na kuwa na utambulisho rasmi(Kutambulika) na hapo ndo balaa litaanza.
Mimi naona tayari hizi chat bots Zimesha anza kazi hiyo bila hata sisi kulitambua mmana Kadri tuvyo itumia ndo zina feed information
 
Walihakikisha wanateka nyanja kuu ambazo ni Spirit and Soul baada ya hapo mind and body zikafuata na ndo hicho kinaendelea hapa.
Hakika na soul ndio light inyo shine through the body and mind. Nafsi ikishakufa tu, ndo unaona haya matokeo.. Ila tatizo lilopo unatumia mind hiyo hiyo iliyo kufa kutafuta uzima wa nje(material)
Imani za kigeni zilikuja Kwa lengo la kutuweka gizani na kutufanya kuwa watumwa.
Waafrika walio wengi, wamepumbazika baada ya kutojua uelekeo wao. Wanafuata na kuamini kila kitu cha kigeni pasipo kuhoji.
That's the plan
Tupo ndani ya Giza nene.
Ili kuondokana na Giza Hilo inatupasa sasa kuruhusu NURU sahihi kutoka kwenye chanzo chetu, Kisha hekima, busara na maamuzi yaliyo sahihi yataanza kujitokeza.
Bila kuruhusu NURU sahihi, basi tunaenda kuwa mazezeta.
Nuru⚡
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…