Nafasi za kazi mbalimbali - 2026 Mega thread

Nafasi za kazi mbalimbali - 2026 Mega thread

Seran ukipata michongo ya Dodoma ya kazi za Sales, Marketing, Public Realations and Promotions please let me know au share hapa. Nina mtu wangu yupo Dar na ningependa anijoin huku Dom na tiketi yake ni kama akipata mchongo huku.
 
Ila waajiri sometimes jau sana.

1. Unakutana na tangazo la kazi, unafanyiwa process zote za kazi na unapata hiyo kazi, unaambiwa tunakupa wiki moja ya kukuangalia Ufanyaji kazi wako practically.

Unasema poa.

Ghafla unaanza kufanya kazi tofauti na mlizokubaliana afu boss anakuambia mbona sioni maendeleo yako, sikuelewi unafanya nini hapa 😂

Sasa utaonaje maendeleo ya kazi wakati unanipa majukumu ambayo ni mapya kwangu na sio kama yale tuliyokubaliana?



2. Kuna hii kazi ya social media officer / content creator

Unaweza kuajiriwa leo, afu baada ya wiki boss anakuuliza mbona sioni matokeo chanya?
Yaani kama ni kampuni inayotaka wateja, basi anataka wateja wajae ndani ya wiki hiyo hiyo uliopata kazi
Wiki hiyo hiyo anataka views wawe milioni, comments zifike laki, reactions zifike laki 😂

Unamshauri, ili hii content ifanyike vizuri inahitajika hiki na hiki, na yeye anaanza kusema ah mbona wengine wanafanya hvy hvy bila hivyo vifaa 😂

Boss mwngn anaamini kifaa fulani ndio bora kuliko kingine.
Atakuambia camera ya Sony inatoa picha/Video kali, WTF basi chukua hiyo camera nawe utoe picha/Video kali.

Boss mwngine anasema Komputa za MAC zinafanya kazi vzr 😂
90% ya kazi za social media officer / content creator huwezi kuziepuka kompyuta za windows

Sehemu zingine hazina wifi afu hapo hapo anataka content ziende kwa wakati 😂

Unajua kabisa h kampuni yangu inahitajika iwe na vifaa, afu hapo hapo unategemea huyo unayemuajiri awe na vifaa vyake binafsi 😂


Ah kudadeki mambo ni mengi
 
ajira kiwanda cha sigara
Hili tangazo kama sio matapeli basi TCC wamekosa umakini. Cha kwanza kwenye preamble wameandika four hundred and ninety four positions kisha kwenye mabano wakaweka (20). Pili nafasi zilizotangazwa ni 30 na sio 494 kama tangazo lilivyoelekeza. Tatu nafasi zote mbili zinataka watu wenye Diploma ila mwishoni mwa tangazo kwenye general instructions inasema wa attach certificates na transcripts za Postgraduate, Degree/Advance Diploma na Diploma. Nne email iliyotolewa ina kikonyo cha gmail badala ya .co.tz
 
Back
Top Bottom