A
Anonymous
Guest
Mradi wa EACOP ulianza mwaka 2021 na sasa mwaka 2026 unakaribia kufikia mwisho. Hata hivyo, kuna wasiwasi mkubwa kuhusu utekelezaji wa mpango wa uhamishaji wa ujuzi na urithishaji wa nafasi (succession plan), hususan kwa wafanyakazi wa Kitanzania.
Kwa zaidi ya miaka minne, Watanzania wamefanya kazi na kupata uzoefu mkubwa katika maeneo mbalimbali kama HSE, Mazingira, HR, Uhandisi na taaluma nyingine muhimu. Pamoja na uzoefu huo, wengi wao wanaondolewa baada ya mikataba yao kuisha, huku baadhi ya wataalamu wa kigeni wakiendelea kubaki katika nafasi ambazo zinaweza kufanywa kwa ufanisi na Watanzania.
Suala hili linaibua maswali kuhusu utekelezaji wa sera za Local Content na uhamishaji wa ujuzi ambazo zilipaswa kuwa miongoni mwa faida kuu za mradi huu kwa taifa. Watanzania wamechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya mradi huu na wanastahili kupewa nafasi ya kuendeleza taaluma zao na kutumia uzoefu walioupata.
Tunaiomba Serikali, , , na kufuatilia kwa karibu suala hili ili kuhakikisha kuwa fursa za ajira, maendeleo ya taaluma na uhamishaji wa ujuzi vinawanufaisha Watanzania kama ilivyokusudiwa.
Local Content isibaki kwenye ripoti pekee; ionekane katika ajira, uongozi na fursa zinazotolewa kwa Watanzania ndani ya miradi mikubwa ya kimkakati. 🇹🇿