Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 6,765
- 13,824
Wasalaam,
Kwanza nianze kwa kuwapongeza chama cha demokrasia na maendelea (CHADEMA) kwa uthubutu wao wa kuanzisha na kuratibu maandamano haya ya amani kama njia ya kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala na hata jamii ya kimataifa.
Kwa upekee sana nipende kuisifu serikali tawala na vyombo vya usalama hasa vya mkoa wa dar es salaam kwa ukomavu huu wa kuruhusu maandamano haya (japo najua ni kwa shingo upande na maelekezo maalum)
Lipo jambo moja lilikuwa likipigiwa chepuo wakati wa kunadi maandamano haya kuwa yatakuwa ya kitaifa pasi na kujali chama, dini na kadharika na viongozi wa chadema waliwakaribisha watanzania wote kushiriki na kufikisha ujumbe wa changamoto ya ugumu wa maisha na udharimu wa chama na serikali iliyokuwa madarakani.
Hiyo ndio picha niliyoiweka kichwani na kuamka nayo leo nikitegemea kuiona kwenye maandamano haya, lakini hali imekuwa tofauti licha ya maandamano hayo kufana kwa wingi wa watu na shamla shamla za hapa na pale ni kama yamekuwa maandamano ya chama kimoja tu.
Nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu huku nikijiuliza maswali yafuatayo.
Wako wapi magwiji wa siasa kutoka vyama vingine vya upinzani wanaolilia uvunjifu wa kanuni za uchaguzi kila kukicha?
wako wapi wafanyabiashara wakubwa na maarufu wanaokumbana na changamoto ya kodi zisizo na msingi kila kukicha?
Wako wapi viongozi wa dini maarufu wanaohubiri haki za raia kila kukicha na kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa raia?
Wako wapi wasanii wanaoimba nyimbo za kulalamikia maisha mabovu kwa watanzania kila kukicha?
Je, wako wapi waandishi wa habari nguli wanaongoza kupinga mikataba mbalimbali ya kidharimu kwa nchi yetu?
Ina maana hawa wote hawajaona umuhimu wa haya maandamano, kuunga mkono na kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala, je kinachoonekana leo kinaleta picha ya utaifa?
Ninachokiona mimi, uoga, unafiki, uzandiki wa watu maarufu kutoka kila nyanja nchini ambao kila kukicha kazi kupiga midomo kwenye keyboard leo wameamua kuonyesha unafiki wao na kufanya maandamano haya yaonekane ni ajenda ya kisiasa ya chama kimoja na si jambo la kitaifa kama ilivyokusudiwa.
Wasalaam.