Nafasi na mchango wa watu maarufu katika maandamano ya leo tarehe 24 Januari

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalaam,

Kwanza nianze kwa kuwapongeza chama cha demokrasia na maendelea (CHADEMA) kwa uthubutu wao wa kuanzisha na kuratibu maandamano haya ya amani kama njia ya kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala na hata jamii ya kimataifa.

Kwa upekee sana nipende kuisifu serikali tawala na vyombo vya usalama hasa vya mkoa wa dar es salaam kwa ukomavu huu wa kuruhusu maandamano haya (japo najua ni kwa shingo upande na maelekezo maalum)

Lipo jambo moja lilikuwa likipigiwa chepuo wakati wa kunadi maandamano haya kuwa yatakuwa ya kitaifa pasi na kujali chama, dini na kadharika na viongozi wa chadema waliwakaribisha watanzania wote kushiriki na kufikisha ujumbe wa changamoto ya ugumu wa maisha na udharimu wa chama na serikali iliyokuwa madarakani.

Hiyo ndio picha niliyoiweka kichwani na kuamka nayo leo nikitegemea kuiona kwenye maandamano haya, lakini hali imekuwa tofauti licha ya maandamano hayo kufana kwa wingi wa watu na shamla shamla za hapa na pale ni kama yamekuwa maandamano ya chama kimoja tu.

Nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu huku nikijiuliza maswali yafuatayo.

Wako wapi magwiji wa siasa kutoka vyama vingine vya upinzani wanaolilia uvunjifu wa kanuni za uchaguzi kila kukicha?

wako wapi wafanyabiashara wakubwa na maarufu wanaokumbana na changamoto ya kodi zisizo na msingi kila kukicha?

Wako wapi viongozi wa dini maarufu wanaohubiri haki za raia kila kukicha na kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa raia?

Wako wapi wasanii wanaoimba nyimbo za kulalamikia maisha mabovu kwa watanzania kila kukicha?

Je, wako wapi waandishi wa habari nguli wanaongoza kupinga mikataba mbalimbali ya kidharimu kwa nchi yetu?

Ina maana hawa wote hawajaona umuhimu wa haya maandamano, kuunga mkono na kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala, je kinachoonekana leo kinaleta picha ya utaifa?

Ninachokiona mimi, uoga, unafiki, uzandiki wa watu maarufu kutoka kila nyanja nchini ambao kila kukicha kazi kupiga midomo kwenye keyboard leo wameamua kuonyesha unafiki wao na kufanya maandamano haya yaonekane ni ajenda ya kisiasa ya chama kimoja na si jambo la kitaifa kama ilivyokusudiwa.

Wasalaam.
 
..wote uliowataja waliamini maandamano ni kitu kisichowezekana.

..naamini mbele ya safari wote uliowataja watashiriki ktk maandamano.
 
Tulikuwa tunamwambia Marehemu Magufuli kuwa hata kama anatubania HAKI yetu ya KIKATIBA ya kuandamana lakini Ukibana kumbuka UTAACHIA tu ili Mimba ya Demokrasia itunge.

Yako wapi sasa Dunia nzima imetishia kuikatia Misaada Serikali ya Kimabavu ya CCM.

PEEEPOOZ PAWAAA!!!✌️✌️✌️✌️
 
..wote uliowataja waliamini maandamano ni kitu kisichowezekana.

..naamini mbele ya safari wote uliowataja watashiriki ktk maandamano.
Watashiriki kufwata mkumbo na likes za instagram na twitter. Cowards
 
Wasalaam,

Kwanza nianze kwa kuwapongeza chama cha demokrasia na maendelea (CHADEMA) kwa uthubutu wao wa kuanzisha na kuratibu maandamano haya ya amani kama njia ya kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala na hata jamii ya kimataifa.

Kwa upekee sana nipende kuisifu serikali tawala na vyombo vya usalama hasa vya mkoa wa dar es salaam kwa ukomavu huu wa kuruhusu maandamano haya (japo najua ni kwa shingo upande na maelekezo maalum)

Lipo jambo moja lilikuwa likipigiwa chepuo wakati wa kunadi maandamano haya kuwa yatakuwa ya kitaifa pasi na kujali chama, dini na kadharika na viongozi wa chadema waliwakaribisha watanzania wote kushiriki na kufikisha ujumbe wa changamoto ya ugumu wa maisha na udharimu wa chama na serikali iliyokuwa madarakani.

Hiyo ndio picha niliyoiweka kichwani na kuamka nayo leo nikitegemea kuiona kwenye maandamano haya, lakini hali imekuwa tofauti licha ya maandamano hayo kufana kwa wingi wa watu na shamla shamla za hapa na pale ni kama yamekuwa maandamano ya chama kimoja tu.

Nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu huku nikijiuliza maswali yafuatayo.

Wako wapi magwiji wa siasa kutoka vyama vingine vya upinzani wanaolilia uvunjifu wa kanuni za uchaguzi kila kukicha?

wako wapi wafanyabiashara wakubwa na maarufu wanaokumbana na changamoto ya kodi zisizo na msingi kila kukicha?

Wako wapi viongozi wa dini maarufu wanaohubiri haki za raia kila kukicha na kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa raia?

Wako wapi wasanii wanaoimba nyimbo za kulalamikia maisha mabovu kwa watanzania kila kukicha?

Je, wako wapi waandishi wa habari nguli wanaongoza kupinga mikataba mbalimbali ya kidharimu kwa nchi yetu?

Ina maana hawa wote hawajaona umuhimu wa haya maandamano, kuunga mkono na kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala, je kinachoonekana leo kinaleta picha ya utaifa?

Ninachokiona mimi, uoga, unafiki, uzandiki wa watu maarufu kutoka kila nyanja nchini ambao kila kukicha kazi kupiga midomo kwenye keyboard leo wameamua kuonyesha unafiki wao na kufanya maandamano haya yaonekane ni ajenda ya kisiasa ya chama kimoja na si jambo la kitaifa kama ilivyokusudiwa.

Wasalaam.
Vinavyojiita vyama vya upinzani kwa nchi yetu ni vikundi vya ulalamishi hisipokuwa Chadema wanaoonyesha uthubutu na upinzani wa kweli. Hii imekuwa ikionekana muda mrefu mbali na haya maandamano. Nakumbuko kipindi cha tozo watu waliilia Chadema iwasemee hasa Lissu na Mbowe.
 
Wasalaam,

Kwanza nianze kwa kuwapongeza chama cha demokrasia na maendelea (CHADEMA) kwa uthubutu wao wa kuanzisha na kuratibu maandamano haya ya amani kama njia ya kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala na hata jamii ya kimataifa.

Kwa upekee sana nipende kuisifu serikali tawala na vyombo vya usalama hasa vya mkoa wa dar es salaam kwa ukomavu huu wa kuruhusu maandamano haya (japo najua ni kwa shingo upande na maelekezo maalum)

Lipo jambo moja lilikuwa likipigiwa chepuo wakati wa kunadi maandamano haya kuwa yatakuwa ya kitaifa pasi na kujali chama, dini na kadharika na viongozi wa chadema waliwakaribisha watanzania wote kushiriki na kufikisha ujumbe wa changamoto ya ugumu wa maisha na udharimu wa chama na serikali iliyokuwa madarakani.

Hiyo ndio picha niliyoiweka kichwani na kuamka nayo leo nikitegemea kuiona kwenye maandamano haya, lakini hali imekuwa tofauti licha ya maandamano hayo kufana kwa wingi wa watu na shamla shamla za hapa na pale ni kama yamekuwa maandamano ya chama kimoja tu.

Nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu huku nikijiuliza maswali yafuatayo.

Wako wapi magwiji wa siasa kutoka vyama vingine vya upinzani wanaolilia uvunjifu wa kanuni za uchaguzi kila kukicha?

wako wapi wafanyabiashara wakubwa na maarufu wanaokumbana na changamoto ya kodi zisizo na msingi kila kukicha?

Wako wapi viongozi wa dini maarufu wanaohubiri haki za raia kila kukicha na kupinga vitendo vya unyanyasaji kwa raia?

Wako wapi wasanii wanaoimba nyimbo za kulalamikia maisha mabovu kwa watanzania kila kukicha?

Je, wako wapi waandishi wa habari nguli wanaongoza kupinga mikataba mbalimbali ya kidharimu kwa nchi yetu?

Ina maana hawa wote hawajaona umuhimu wa haya maandamano, kuunga mkono na kufikisha ujumbe wao kwa serikali tawala, je kinachoonekana leo kinaleta picha ya utaifa?

Ninachokiona mimi, uoga, unafiki, uzandiki wa watu maarufu kutoka kila nyanja nchini ambao kila kukicha kazi kupiga midomo kwenye keyboard leo wameamua kuonyesha unafiki wao na kufanya maandamano haya yaonekane ni ajenda ya kisiasa ya chama kimoja na si jambo la kitaifa kama ilivyokusudiwa.

Wasalaam.
Mkuu nilichoona mimi hii ni teaser tu , next time itakua balaa , maana itagusa watu wote na hapo ndipo utasikia ' km tuliweza kipindi kile kwann sasa tushindwe ' hutoamini
 
Utamaduni wa maandamano ndiyo unaanza na huko mbele watu wengi watashiriki bila hofu. Kwa leo upande wa serikali haukuwa na uhakika na upande wa wananchi pia. imekuwa kama pilot study.Mwanzo huwa mgumu. wacha tuone maandamano yajayo.
Sawa sawa Mkuu
 
Back
Top Bottom